Saturday, June 18, 2016

CHIRWA ATUA JANGWANI KWA SH. MILIONI 240

Mshambuliaji raia wa Zambia, Obrey Chirwa amejiunga na Yanga kwa dau la sh. Milioni 240 akitokea katika klabu ya FC Platinum za Zimbabwe.

Chirwa ameifungia Platinum mabao matano katika mechi nane alizocheza kwenye ligi kuu ya Zimbabwe.
Mshambuliaji huyo pia yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia chini ya umri wa miaka 23.
Kiungo huyo mshambuliaji amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga na tayari Yanga wameshatuma jina la mchezaji huyo CAF ili wapate leseni itakayomwezesha mchezaji huyo kushiriki michuano ya kombe la shirikisho CAF CC.

Chirwa atashirikiana vizuri na mshambuliaji Donald Ngoma ambaye wamewahi kucheza wote katika klabu ya FC Platinum.

Yanga ilikuwa ikimuwania Winga Walter Musona lakini baadae walighairi na kuelekeza macho yao kwa Chirwa.

Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

Related Posts:

  • WACHEZAJI 10 MBADALA WA PAUL POGBA MAN U Klabu ya Manchester United ipo katika harakati za kuhakikisha wanainasa saini ya Kiungo wa Juventus Paul Pogba, lakini mbio hizo zinaweza kukumbwa na changamoto na hatimaye Man U kujikuta wakishindwa kupata huduma ya nyota h… Read More
  • SHIZA KICHUYA ATUA MSIMBAZI Klabu ya Mtibwa Sugar imethibitisha kukamilisha uhamisho wa mchezaji wao Shiza Kichuya kujiunga na klabu ya Simba. Kwa muda mrefu kichuya alikuwa akihusishwa na kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi lakini taarifa za hivi p… Read More
  • JAMES RODRIGUEZ AITAJA KLABU ANAYOTAKA KUHAMIA James Rodriguez amesema anataka kujiunga na wababe wa soka la Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain msimu ujao. Rodriguez alikuwa akihusishwa sana kutimkia ligi kuu ya Uingereza lakini amesema anatamani kujiunga na PSG. … Read More
  • MNIGERIA AHMED MUSA ATUA LEICESTER CITY Klabu ya Leicester City imemsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwa mkataba wa miaka 4 utakaogharimu pauni milioni 16. Southampton,Everton na West Ham walikuwa wakitafuta saini ya mchezaji huyo. M… Read More
  • TISA WAONGEZEWA MKATABA NDANDA FC Timu ya Ndanda Fc imewaongezea mkataba wa mwaka mmoja wachezaji tisa kwa ajili ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho msimu ujao wa Ligi Kuu Vodacom 2016/17. Msemaji wa Ndanda Fc, Idrisa Bandali aliwataja wachezaji walioon… Read More

0 comments:

Post a Comment