Yanga Yainyoosha Azam Fc Chamanzi

Azam FC 1 - 2 Young Africans.

Kiungo Wa Everton James McCathy Avunjika Mguu

Kiungo James McCarthy wa Everton sasa atakaa nje na kuukosa msimu wote huh baada ya kuvunjika mifupa miwili ya mguu wake.

DRAW CAF CL And CC 2018

Draw Caf Cl and CC 2018

Yanga Yazinduka Yaambulia Ushindi Mwembamba

Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa goli moja kwa sifuri

Madrid Yaivurumisha Deportivo 7-1

Klabu ya Real Madrid leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono kwa jumla ya magoli 7-1 dhidi ya Klabu Deportivo la Coruna

Showing posts with label SerieA. Show all posts
Showing posts with label SerieA. Show all posts

Saturday, October 22, 2016

RATIBA YA MICHEZO MBALIMBALI DUNIANI LEO OCTOBER 22



RATIBA LIGI KUU MBALIMBALI DUNIANI
TANZANIA Vpl october 22
16:00       Kagera Sugar  vs Young Africans
16:00       African Lyon vs Mbeya City
16:00       Ndanda Fc vs Mwadui
16:00       Mtibwa Sugar vs Stand United
16:00      Majimaji vs Ruvu Shooting
19:00      Azam FC vs JKT Ruvu
ENGLAND EPL October 22
14:30      AFC Bournemouth vs Tottenham Hotspur
17:00      Arsenal vs Middlesbrough
17:00      Burnley vs Everton
17:00      Hull City vs Stoke City
17:00      Leicester City vs Crystal Palace
17:00      Swansea City vs Watford
17:00     West Ham United vs Sunderland
19:30      Liverpool vs West Bromwich Albion
ITALY - Serie A October 22
19:00       Sampdoria vs Genoa
21:45        AC Milan vs Juventus
SPAIN - LaLiga Santander October 22
14:00          Espanyol vs Eibar
17:15         Valencia vs Barcelona
19:30         Real Sociedad vs Alaves
21:45         Granada vs Sporting Gijon
GERMANY - Bundesliga October 22
16:30            Bayer Leverkusen vs Hoffenheim
16:30            Darmstadt vs Wolfsburg
16:30            Freiburg vsAugsburg
16:30            Hertha Berlin vs FC Cologne
16:30            Ingolstadt vs Borussia Dortmund
19:30            Bayern Munich vs Borussia Moenchengladbach         
FRANCE - Ligue 1 October 22
18:00         Lyon vs Guingamp
21:00        Angers vs Toulouse
21:00        Bordeaux vs Nancy
21:00        Dijon vs Lorient
21:00        Lille vs SC Bastia
21:00       Nantes vs Rennes
KENYA - Premier League October 22
14:00       Mathare United vs Bandari

15:00      Kakamega Homeboyz vs SoNy Sugar

Saturday, August 6, 2016

AC MILAN YAUZWA KWA WACHINA

Katika hali ya kushangaza aliyekuwa Mmiliki wa klabu ya AC Milan, Silvio Berlusconi amewauzia wachina hisa zake zote ambazo ni asilimia 99.93.

Ripoti ya Gazzetta World inasema, Meneja uwekezaji Changxing, pamoja na wafanya biashara wengine wakubwa raia wa china, Li Yonghong wamelipa kiasi cha Euro milioni 740 kuinunua klabu hiyo, kiasi hicho cha fedha kikijumuisha deni ambalo klabu hiyo ilikuwa inadaiwa la Euro milioni 220.

Asilimia 0.07 ya hisa iliyobaki itakuwa inamilikiwa na familia ya Berlusconi, baada ya miaka 30 ya Waziri mkuu huyo wa zamani wa Italy kuimiliki klabu hiyo.
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

Wednesday, July 27, 2016

VIDEO: MASHABIKI WA NAPOLI WALIVYOCHOMA MOTO JEZI YA HIGUAN

Mashabiki wa Napoli wamechukizwa na kitendo cha Gonzalo Higuan kujiunga na Mabingwa wa Seria A, klabu ya Juventus kwa kile walichodai kuwa kitendo hicho ni usaliti.
Katika kuonyesha kukerwa kwao na taarifa hiyo waliamua kuchoma moto Jezi ya mchezaji huyo pamoja na Magazeti yote ambayo yaliandika habari hiyo.


Tazama video hapa chini Uone wakati mashabiki hao wakichoma moto jezi ya Higuan
Like Ukurasa Wetu Wa Facebook, Bonyeza  HAPA 

Sunday, May 15, 2016

JUVENTUS YAISHUSHIA KIPIGO KIKALI SAMPDORIA


Mabingwa wa ligi kuu nchini Italia Juventus, jana wametoa kipigo kikali kwa timu ya Sampdoria kwa kuichapa magoli 5 – 0, Juventus tayari walishakuwa mabingwa hata kabla ya mchezo wao dhidi ya Sampdoria na sasa wamefikisha jumla ya pointi 91 katika nafasi ya kwanza huku wakifuatiwa na Napoli katika nafasi ya pili waliojikusanyia pointi 82 kwenye michezo 38 waliyocheza.
Magoli ya Juve yalipachikwa nyavuni na Patrick Evra aliyefunga dakika ya 5, Paul Dybala akifunga magoli mawili dakika ya 15  na 37, magoli mengine yalifungwa na Chiellini dakika ya 77 na Bonucci akafunga karamu hiyo ya magoli alipofunga goli la 5 dakika ya 85.

Sunday, May 8, 2016

INTER MILANI YAFUZU KUSHIRIKI EUROPA LEAGUE 2016/17


Inter Milan imetinga katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu nchini Italia, Serie A, baada ya ushindi wa 2 – 1 walioupata dhidi ya Empoli. Vijana hao wa Roberto Mancini walishindwa kufuzu nafasi ya kucheza UEFA Champions League baada ya kukubali kipigo cha magoli 2 – 0 dhidi ya Lazio wikiendi iliyopita lakini ushindi wao dhidi ya Empoli  jana umewafanya wajihakikishie nafasi yao ya kushiriki michuano ya UEFA EUROPA League Msimu Ujao. Magoli ya Inter yalifungwa na Icard dakika ya 12 na Perisic 40 na lile la Empoli lilifungwa na Pucciarelli dakika ya 37.

Sunday, May 1, 2016

UJUMBE WA PAUL POGBA KWA MASHABIKI WA SOKA DUNIANI


Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba amekuwa ni miongoni mwa ma Midfielders wazuri zaidi duniani tangu ajiunge na vigogo wa Italia Juventus.
Superstaa huyo wa Juve na timu ya Taifa ya Ufaransa anaamini atayafikia mafanikio makubwa katika Career yake hiyo kama Pele na Diego Maradona.

Baada ya kuachwa na Man United mwaka 2012 Pogba amekuwa ni Midfielder bora zaidi barani Ulaya, huku vilabu vingi Barani humo vikionyesha kumuhitaji Nyota huyo vikiwemo Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich.

Mfaransa huyo mwenye miaka 23 kwa sasa ameshinda mataji 4 ya Serie A na kombe la Copa Iitalia akiwa pia ni miongoni mwa wachezaji wa Juve waliocheza fainali ya Uefa Champions mwaka 2015 na kufungwa na  Barcelona. Lakini kwa sasa Pogba amekuwa na matarajio makubwa zaidi na kusema ni matumaini yake kuwa  atakuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi Ulimwenguni katika historia ya Mpira wa miguu.

“Nataka kuwa Legend kama Pele au Maradona” alisema Pogba alipozungumza na Gazeti la La Repubblica.

“Au hata zaidi ya hao, sio kwamba nasema mimi ni bora zaidi, ni kwamba nataka niwe bora zaidi” aliongeza Pogba.

“Nina tatizo moja, Nachukia kushindwa, na napenda kuwa tofauti na wengine, nataka kufanya vitu ambavyo hakuna aliewahi kuvifanya. Najituma kwasababu nina lengo la kuwa bora na ni kwa sababu nafurahi pale ninaposhinda” alisema Pogba

“Naweza nisiwe miongoni mwa wachezaji wanaopendwa sana, lakini hilo sio lengo langu, najitahidi ili nije kuwa bora”.



Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com