Yanga Yainyoosha Azam Fc Chamanzi

Azam FC 1 - 2 Young Africans.

Kiungo Wa Everton James McCathy Avunjika Mguu

Kiungo James McCarthy wa Everton sasa atakaa nje na kuukosa msimu wote huh baada ya kuvunjika mifupa miwili ya mguu wake.

DRAW CAF CL And CC 2018

Draw Caf Cl and CC 2018

Yanga Yazinduka Yaambulia Ushindi Mwembamba

Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa goli moja kwa sifuri

Madrid Yaivurumisha Deportivo 7-1

Klabu ya Real Madrid leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono kwa jumla ya magoli 7-1 dhidi ya Klabu Deportivo la Coruna

Showing posts with label All. Show all posts
Showing posts with label All. Show all posts

Monday, May 16, 2016

WINGA WA ARSENAL ATUPWA NJE KIKOSI CHA ENGLAND



Theo Walcott anayecheza kama Winga/Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal ameachwa katika kikosi cha England kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa.
Walcott amesema hajafurahishwa na kuachwa kwake huku akisema ameongea na Roy Hodgson na anaheshimu maamuzi yake.

Hiki ndo alichoandika Walcott katika akaunti yake ya Twitter.

HIKI NDO KIKOSI CHA ENGLAND KITAKACHOSHIRIKI UERO 2016


KIKOSI CHA WANAUME 26 WATAKAOIWAKILISHA ENGLAND KATIKA MICHUANO YA EURO 2016

KINDA WA MAN U AITWA KIKOSI CHA ENGLAND UERO 2016



MARCUS Rashford kijana anayecheza katika kikosi cha Man United ameitwa na Kocha Roy Hodgson katika kikosi cha  wachezaji 26 cha timu ya Taifa ya England kitakachoshiriki mashindao ya Euro yatakayofanyika nchini Ufaransa.

KIKOSI CHA SIMBA CHAPEWA LIKIZO FUPI


SIMBA iliyotoka kucheza na Mtibwa Sugar jana na kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila goli lililofungwa na Abdi Banda, imepewa mapumziko mafupi kabla ya kuanza kujiandaa na mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya JKT Ruvu.

Simba kwa sasa wanashika nafasi ya 3 wakiwa wamejikusanyia pointi 62 wakizidiwa pointi moja tu na Azam FC wanaoshika nafasi ya 2 kwa pointi 63, wote wakiwa wamecheza michezo 29.

YANGA WALIVYOIACHA ARDHI YA TANZANIA (PICHA)

 KIKOSI CHA YANGA KIMESAFIRI KUELEKEA NCHINI ANGOLA AMBAKO WATACHEZA NA TIMU YA GD SAGRADA ESPERANCA KATIKA MCHEZO WA PILI WA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA HATUA YA MTOANO







VICENT BOSSOU AITWA TIMU YA TAIFA YA TOGO


Kocha mpya wa Togo Mfaransa Claude LeRoy amemuita Vicent Bossou katika kikosi cha timu yake ya Taifa .Bossou ameitwa kutokana na kiwango kizuri alichokionyesha akiwa na klabu ya Yanga.

Tayari barua ya mualiko wa kujiunga na timu ya taifa lake imeshafika Yanga katika ofisi ya katibu wao Baraka Deusdedit kwa beki huyo kujiunga na timu hiyo itakayoingia kambini wiki chache zijazo kuumana na Liberia.

“Kweli nimeitwa kujiunga na timu ya taifa, Yanga wameshapokea barua hiyo ya mualiko na kunijulisha, kwangu ni taarifa nzuri kwa kuwa nakwenda kulisaidia taifa langu baada ya kuisaidia klabu yangu kutwaa ubingwa sasa najiunga na taifa langu,” amesema Bossou.

Mara ya mwisho kwa Bossou kuitwa Togo ni wakati kikosi hicho kikicheza na Uganda wakati huo ikifundishwa na kocha Mbelgiji Torm Saintfiet ambaye hata hivyo hakumchezesha hata mara moja.

Sunday, May 15, 2016

HIZI NDO MBWEMBWE ZA KOCHA MPYA AZAM FC

Zeben Hernandez Kocha Mpya Azam FC

KOCHA Mkuu mtarajiwa wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Zeben Hernandez, ameweka wazi kuwa malengo yake makubwa ni kuifanya timu hiyo kuwa timu kubwa barani Afrika msimu ujao.

Kocha huyo raia wa Hispania aliyekuwa akiinoa Club Deportivo Santa Ursula ya Ligi Daraja la Tatu nchini humo, ametua nchini juzi pamoja na Kocha wa Viungo Jonas Garcia kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa timu hiyo kabla ya kusaini mkataba wa kuinoa Azam FC msimu ujao.

Makocha hao wametua kufuatia Kocha Mkuu wa sasa wa Azam FC, Stewart Hall, kutangaza kuachia ngazi mwishoni mwa msimu huu kufuatia kutoridhishwa na matokeo ya hivi karibuni ya timu hiyo.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz leo asubuhi mara baada ya kuwasili mkoani Tanga kushuhudia mchezo wa timu hiyo dhidi ya African Sports jioni ya leo, Hernandez amewaambia mashabiki wa Azam FC kuwa watarajie ubora wa timu msimu ujao utakaoifanya kuwa timu bora Afrika.

“Ninafuraha kubwa, Azam itakuwa timu bora msimu ujao, tutafanya kazi kwa bidii kila mara na kuifanya Azam kuwa timu kubwa Afrika,” alisema.

Aifurahia Tanzania

Hernandez hakusita kuelezea furaha yake kutokana na watu aliokutana nao Tanzania, ambapo amesema kuwa: “Ninafuraha kubwa, watu wa hapa ni wazuri na waliojipanga, na mpira wa hapa una vipaji vingi, wachezaji wengi kuwa na vipaji ni jambo muhimu kwa mpira wa Tanzania, Tanzania kama nchi ni sehemu nzuri sana na ninafuraha sana kwa hilo.”

Ujio wao ndani ya Azam FC

“Malengo yetu ni kuifanya Azam kuwa na mfumo mpya wa soka la kisasa kuanzia utambulisho kama timu, mbinu zetu za kufanya kazi na pia katika mechi…Kwangu mimi na mwenzangu kufanya kazi Afrika ni uzoefu mzuri na tunafuraha sana,” alisema.

Kwa upande wake Jonas Garcia aliyeambatana naye alionyesha furaha kubwa kuja Azam FC huku akisema kuwa watafanya kazi kwa bidii sana kwa ajili ya kuipa ubora timu hiyo.

C.E.O afafanua ujio wao

Akizungumzia ujio wa makocha hao, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema kuwa mara baada ya kuwasili juzi tayari wameanza nao mazungumzo jana kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho msimu ujao.

“Tumewapokea juzi Dar es Salaam tunamshukuru Mungu, jana tulikuwa nao na tumeanza mazungumzo, leo wako hapa Tanga kuangalia mchezo (African Sports vs Azam FC) na watafanya tathimini yao, kwa hiyo mazungumzo bado yanaendelea na katika hali ya kawaida tukifanikiwa kwa maana yake watakuwa wanachukua timu yetu ya Azam kwa msimu unaokuja, jambo jema kwetu ni kwamba makocha hao bado ni vijana na wanadhamira ya kupata mafanikio, hivyo hiko ni kitu ambacho tunajivunia.

“Lakini bado tunasema kwamba bado tunazungumza nao hatujafika nao muafaka mpaka mwisho, lakini tunachopenda kusema ni kwamba tunawaomba mashabiki wetu wawe watulivu timu ipo na kocha bado yupo (Stewart Hall) na anamalizia muda wake na kuhakikisha ya kuwa kila kitu kinakwenda sawasawa kabla ya msimu haujaisha,” alisema.

Bosi huyo aliyebobea kwenye mambo ya uongozi wa soka na kutambulika na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Duniani (FIFA), alimalizia kwa kusema kuwa wanatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari kesho Jumatatu mara baada ya kumalizia mazungumzo ya mwisho na makocha hao, ambapo ataweka wazi kila kitu kuhusu muundo wa benchi la ufundi msimu ujao.

SOURCE: AZAM FC OFFICIAL SITE

AZAM FC YAICHAPA AFRICAN SPORTS


Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati Azam FC ilikuwa ugenini jijini Tanga kupambana na African Sports katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom. Azam FC wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa jumla ya magoli 2 - 1. Magoli ya Azam FC yamefungwa na  Allan Wanga dakika ya 10 na Erasto Nyoni dakika ya 74, huku goli pekee la African Sports likiwekwa kimiani na Omary Ibrahim katika dakika ya 11.

Matokeo haya yameifanya Azam FC kuendelea kushikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kwa kufikisha pointi 63 katika michezo yao 29.

SIMBA SC WAIDUNGUA MTIBWA SUGAR NYUMBANI KWAO


SIMBA ilishuka dimbani hivi leo kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wao wa 29 wa ligi kuu Tanzania bara,Mchezo uliopigwa mjini Morogoro.
Mchezo huo umemalizika kwa Simba SC kushinda kwa goli 1 - 0 goli lililofungwa na Abdi Banda dakika ya 60 ya mchezo.
Simba sasa inafikisha pointi 62 katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi baada ya Azam FC nao kushinda katika mchezo wao dhidi ya African Sports.

CARLO ANCELOTTI AMTABIRIA MABAYA PEP GUARDIOLA


Kocha anayechukua mikoba ya Pep Guardiola katika klabu ya Bayern Munich Carlo Ancelotti amesema ipo siku Guardiola atatimuliwa kama mbwa katika maisha yake ya ukocha.

Ancelotti amemuonya Pep kwamba katika maisha yake ya ukocha atakuja kutimuliwa siku moja akisisitiza kuwa ni kitu ambacho hakuna kocha yoyote duniani anaweza akakikwepa.
Ancelotti anayeonekana kuwa miongoni mwa makocha bora duniani kwa sasa ameshinda taji la UEFA Champions league akiwa na AC Milan na Real Madrid. Carlo pia ameshinda kombe la Serie A, English Premier League, FA Cup na Ligue 1 lakini hata hivyo ameshawahi kutimuliwa mara kadhaa katika maisha yake ya ukocha.

Alitimuliwa na Chelsea licha  ya kushinda ligi kuu mara 2 sawasawa na kilichomtokea akiwa Real Madrid akiipa Madrid ubingwa wa 10 wa UEFA Champions League.

Ancelotti ameyasema hayo kufuatia rekodi za Guardiola, Pep ni miongoni mwa mameneja wachache waliopata mafanikio makubwa akiwa na klabu zote za Barcelona na Bayern Munich na katika klabu hizo zote mbili Guardiola aliondoka kwa kupenda kwake na sio kutimuliwa.

Lakini akiwa anajiandaa kukabiliana na kibarua kizito zaidi cha kuinoa Manchester City, Ancelotti amemuonya Guardiola kwamba itakuja itokee Guardiola nae kuwa katika orodha ya makocha waliowahi kuonja machungu ya kutimuliwa na klabu kubwa.

Akiwa katika mahojiano na The Times Ancelotti alisema “ Nikiwa Chelsea nilishinda mara 2 ligi kuu, ila niliishia kutimuliwa, Madrid nako nimewapa taji la 10 UEFA Champions bado wakanitimua”

“Kocha ambaye hajawahi kutimuliwa ni Guardiola pekee, Sir Alex Ferguson alishatimuliwa, Marcelo Lipi kafukuzwa, Fabio Capello kafukuzwa, Jose Mourinho kafukuzwa, Rafa Benitez kafukuzwa”

“Ni Guardiola tu ndiye ambae hajawahi kufukuzwa, lakini bado ni mdogo na ana muda mwingi wa kufanya kazi, siku moja atakuja katika klabu yetu, klabu ya makocha waliowahi kutimuliwa”

HATIMA YA VAN GAAL MAN UNITED YAWEKWA WAZI


Louis Van Gaal amehakikishiwa na mabosi wa United kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba wake kwa mujibu wa ripoti ya Daily Star.
Mdachi huyo anayeinoa United amekuwa akisemwa sana juu ya uwezo wake kufuatia matokeo mabaya ya klabu hiyo na hasa baada ya kutolewa mapema katika michuano ya UEFA Champions League.

Van Gaal bado ana mwaka mmoja umebaki katika mkataba wake lakini Jose Mourinho amekuwa akimnyima usingizi Gaal kutokana na kuhusishwa mara kwa mara na kujiunga na klabu hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Star, Mabosi wa United wamemuhakikishia Van Gaal kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi utakapomalizika mkataba wake.

“Niko hapa na napambana” alinukuliwa Van Gaal
“Licha ya lawama zote ninazotupiwa na vyombo vya habari, lawama nzito kutoka kwa wakongwe wa soka, na zingine kutoka kwa watu wa aina mbalimbali mimi naamini katika uwezo wangu, naamini katika uwezo wa Manchester na naamini pia katika wachezaji wangu” aliongeza Van Gaal.

Manchester United wana nafasi ya kuvaa medali za dhahabu endapo tu watafanikiwa kuifunga Crystal Palace katika fainali ya FA Cup itakayopigwa Wembley May 21.

ACACIA KUSITISHA UDHAMINI NA STAND UNITED


KAMPUNI ya ACACIA inayoidhamini timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga imesema itaondoa udhamini wake na klabu ya Stand kama Stand itaendeshwa kama kampuni. Taarifa hizo zimekuja mara baada ya Stand kutangaza kuwa kwa sasa itaendeshwa kama kampuni tofauti na ilivyokuwa awali.Baada ya taarifa hizo kuifikia kampuni hiyo ya ACACIA, uongozi wa kampuni umeiandikia uongozi wa klabu ya Stand United barua inayowataarifu Stand juu ya ACACIA kutaka kusitisha udhamini wao na klabu hiyo kama Stand itaendeshwa kama kampuni.

Mwenyekiti wa Stand United Amani Vicent amethibitisha kupokea barua hiyo kutoka katika kampuni ya ACACIA huku akikiri kuwa ni kweli kwamba Stand kwa sasa itaendeshwa kama kampuni huku akidai kuwa uongozi wa Stand utakaa na Mabosi wa ACACIA ili kuweka mambo sawa lengo likiwa ni kuwaomba wasisitishe udhamini wao licha ya ukweli kuwa Stand ni kampuni na itabaki kuwa hivyo.

Itakumbukwa kuwa kampuni ya ACACIA iliingia udhamini na klabu ya Stand United mara baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi wa mwaka 2014/15, udhamini wenye thamani ya  shilingi bilioni 2.4 kwa muda wa miaka miwili.

AMIS TAMBWE AMWOMBEA MABAYA KIIZA



MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Dar Young Africans Amis Tambwe, amemaliza mchezo wa jana dhidi ya Ndanda FC bila ya kufunga goli, Tambwe anayeongoza katika orodha ya wafungaji bora katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu wa 2015/16 ameshafunga magoli 21.

Akizungumza jana baada ya mechi yao na Ndanda FC iliyoisha kwa sare ya 2 - 2 Tambwe alisema siku zote yeye anapenda kuwa juu ya wengine na ndio maana anapambana sana ili kutimiza azima yake hiyo katika kila mchezo anaopata nafasi ya kucheza, akizungumzia mchezo huo Tambwe alisema amepambana kwa uwezo wake ila hajafanikiwa kupata goli, huku akimwombea mabaya mpinzani wake Hamisi Kiiza anayemnyemelea kwa karibu katika chati hiyo ya ufungaji akiwa ameshafunga magoli 19. Tambwe aliongeza kwa kusema anaomba kwa mungu Kiiza asifunge goli lolote katika michezo yote miwili iliyobaki ili yeye afanikiwe kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu.
"Nataka asifunge goli lolote katika mechi zao zilizobaki, adui yako lazima umuombee mabaya" yalikuwa maneno ya Tambwe alipozungumza baada ya mechi jana katika uwanja wa taifa.

Yanga wamebakiwa na mechi moja wakati Simba wao wakiwa na mechi mbili, hivyo kumfanya Tambwe kuwa na wasiwasi na Kiiza kwamba huenda akaongeza idadi yake ya magoli katika mechi 2 zilizobaki na kumpiku katika tuzo ya mfungaji bora wa msimu ambapo mshindi huondoka na kitita cha zaidi ya shilingi milioni 5 za kitanzania.

VITA YA KUWANIA NAFASI YA PILI VPL KUENDELEA TENA LEO


LIGI kuu Tanzania bara inatarajia kuendelea tena leo katika viwanja viwili. Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa watawakaribisha vijana wa Msimbazi Simba SC wakati huko Tanga Azam FC itachuana na African Sports.
Simba wanashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi 59 katika michezo 28 waliyocheza, wakati Azam FC wao wapo katika nafasi ya 2 kwa jumla ya pointi 63 walizozipata katika michezo 28 waliyocheza.

Timu hizi zitashuka viwanjani leo zote zikiwa na dhamira ya kupata ushindi ili kuweza kuzipata milioni 40 anazopewa mshindi wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League, endapo Azam FC watashinda mchezo wa leo basi moja kwa moja watakuwa washindi wa pili kwa kuibwaga Simba SC kwani watakuwa wamefikisha pointi 66 huku wakibakiwa na mchezo mmoja, wakati huo Simba wao wakishinda mechi ya leo watafikisha pointi 62 na kubakiwa na mchezo mmoja ambao hata wakishinda watafikisha pointi 65 wakiachwa kwa pointi 1 na Azam FC.

Hali hii ndo inazifanya mechi za leo kuwa ni za kuvutia licha ya kuwa bingwa tayari alishapatikana na kukabidhiwa kombe lake. Azam FC watakuwa wanapambana kupata ushindi katika mchezo wake leo, Simba nao watapigana vikali kuhakikisha wanashinda huku wakiwaombea wapinzani wao Azam FC kupoteza katika mchezo wao dhidi ya African Sports.


PICHA ZA MATUKIO YANGA WALIVYOSHEREHEKEA UBINGWA TAIFA






STUTTGART 3 ZASHUKA DARAJA MSIMU HUU


Msimu wa ligi wa 2015/16 umekuwa msimu mbaya kwa wakazi wa jiji la Stuttgart  katika tasnia ya mpira wa miguu. Timu tatu za Stuttgart zimeshuka daraja katika ligi zote 3 zikizoshiriki, Stuttgart iliyokuwa inashiriki ligi kuu kwa maana Bundesliga, Stuttgart II ya ligi daraja la kwanza na Stuttgarter Kickers waliokuwa katika ligi daraja la pili.

Timu  hizo zote zimejikuta zikishuka daraja katika ligi walizokuwa wanashiriki, Stuttgart iliyokuwa katika ligi kuu wameshuka daraja rasmi baada ya mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu waliokubali kipigo cha magoli 3 – 1, mabingwa hao wa Bundesliga msimu wa 2007 wameshuka daraja baada ya kudumu katika ligi kuu kwa takribani miaka 39 bila kushuka daraja.
Stuttgart II tayari wao walishashuka daraja hata kabla ya mchezo wao wa mwisho na Stuttgarter Kickers wao wameshuka daraja baada ya kukubali kichapo katika uwanja wao wa nyumbani cha goli 1 – 0 kutoka kwa Cheminitzer FC .

JUVENTUS YAISHUSHIA KIPIGO KIKALI SAMPDORIA


Mabingwa wa ligi kuu nchini Italia Juventus, jana wametoa kipigo kikali kwa timu ya Sampdoria kwa kuichapa magoli 5 – 0, Juventus tayari walishakuwa mabingwa hata kabla ya mchezo wao dhidi ya Sampdoria na sasa wamefikisha jumla ya pointi 91 katika nafasi ya kwanza huku wakifuatiwa na Napoli katika nafasi ya pili waliojikusanyia pointi 82 kwenye michezo 38 waliyocheza.
Magoli ya Juve yalipachikwa nyavuni na Patrick Evra aliyefunga dakika ya 5, Paul Dybala akifunga magoli mawili dakika ya 15  na 37, magoli mengine yalifungwa na Chiellini dakika ya 77 na Bonucci akafunga karamu hiyo ya magoli alipofunga goli la 5 dakika ya 85.

LEWANDOWSKI AIFIKIA REKODI ILIYOWEKWA MIAKA 39 ILIYOPITA


MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Borrusia Dortmund anayekipiga katika klabu ya Bayern Munich kwa sasa Robert Lewandowski amefikia rekodi iliyowekwa miaka 39 iliyopita katika ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Robert Lewandowski amethibitisha ubora wake katika ligi ya Ujerumani Bungesliga akifanikiwa kufunga magoli 30 baada ya mchezo ambao Bayern walicheza na Hannover siku ya jumamosi na kuibuka na ushindi wa magoli 3 - 1.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland amempiku staa wa Dortmund Pierre-emerick Aubameyang katika mbio za kuwania tuzo ya mfungaji bora wa ligi kwa kufikisha magoli 30 akifikia pia rekodi iliyowekwa mwaka 1977 ya mchezaji asiye Mjerumani kufikisha idadi ya magoli 30 katika msimu mmoja wa ligi kuu nchini Ujerumani,  huku Aubameyang akiwa na magoli 25.
Koln’s Dieter Muller alilkuwa mchezaji wa mwisho kufikisha idadi ya magoli 30 akifunga magoli 34 katika msimu wa 1976/77 huku timu yake ikimaliza katika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi

Gerd Muller yeye ndo anashikilia rekodi ya ufungaji katika ligi ya Ujerumani akifanikiwa kufunga jumla ya magoli 40 katika msimu mmoja.

ANGEL DI MARIA AWEKA REKODI MPYA LIGUE 1


Mchezaji wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria amevunja rekodi iliyowekwa na Marvin Martin ya kutoa pasi za magoli (assists) 17 katika msimu wa 2010/11 baada ya ushindi wa magoli 4 – 0 walioupata PSG jana walipocheza na Nantes.

Di Maria amevunja rekodi hiyo kwa kufikisha pasi za magoli (assists) 18 katika msimu uliomalizika hivi punde wa 2015/16.

Katika mchezo wa wao dhidi ya Nantes Di Maria alitoa pasi zilizozaa magoli akimpasia Zlatan Ibrahimovic na Lucas Moura katika ushindi huo wa 4 – 0.

Rekodi iliyovunjwa ya assists 17 iliwekwa na Marvin Martin akiwa na FC Sochaux’s msimu wa 2010/11