Yanga Yainyoosha Azam Fc Chamanzi

Azam FC 1 - 2 Young Africans.

Kiungo Wa Everton James McCathy Avunjika Mguu

Kiungo James McCarthy wa Everton sasa atakaa nje na kuukosa msimu wote huh baada ya kuvunjika mifupa miwili ya mguu wake.

DRAW CAF CL And CC 2018

Draw Caf Cl and CC 2018

Yanga Yazinduka Yaambulia Ushindi Mwembamba

Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa goli moja kwa sifuri

Madrid Yaivurumisha Deportivo 7-1

Klabu ya Real Madrid leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono kwa jumla ya magoli 7-1 dhidi ya Klabu Deportivo la Coruna

Showing posts with label Vpl. Show all posts
Showing posts with label Vpl. Show all posts

Sunday, January 28, 2018

Hiki Ndo Kikosi Cha Kocha Mfaransa Simba Ikiivaa Majimaji Leo Taifa


Ligi Kuu Vodacom, Tanzania Bara

Mechi:Simba V Majimaji
Mahali:Uwanja Wa Taifa
Muda: Saa 10:00 Jioni



Kikosi Cha Simba Leo


Sunday, January 21, 2018

Kikosi Cha Yanga Dhidi Ya Ruvu Shooting Leo


Sunday, May 7, 2017

Kikosi Cha Simba Leo Dhidi ya African Lyon



  1. Agyei
  2. Bukungu
  3. Zimbwe Jr
  4. Kotei
  5. Murshid
  6. mkude
  7. Kichuya
  8. Mzamiru
  9. Mavugo
  10. Ajib
  11. Mo Ibrahim


Wachezaji wa Akiba
Novati,Manyika, Vicent, Kazimoto, Luizio, Blagnon, Paschal

Safari ya Simba kuishtaki TFF FIFA imeiva ni baada ya jana kupewa barua yao rasmi ya kupokwa pointi 3 na bodi ys ligi.


Bodi ya ligi nchini ‘TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARDS(TPLB)’ jana imeshindilia kaa la moto katika maamuzi yake ya kipoka timu ya Kagera Sugar pointi 3 na magoli 3 kwa kosa la kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi kwa kusema Fakhi wakati anaichezea Kagera Sugar hakuwa na kadi tatu za njano.
Vionjo vilivyo kwenye Barua hiyo ni kama ifuatavyo ”TFF ndio yenye dhamana ya usimamizi wa mpira nchini na ambayo ndio iliyokasimu madaraka kwa TPLB kuendesha ligi kuu” barua iliiendelea kwa sema “baada ya uchunguzi wao ambao ulihoji watu mbalimbali wamebaini kuwa mchezaji Mohamed Fakhi alielalamikiwa na Simba hakuwa na kadi 3 za njano siku ya mchezo wa Kagera sugar na Simba, kwa mantiki hiyo maamuzi yaliyofanywa na kamati ya kuipoka pointi Kagera hayakuwa sahihi na hivyo Matokeo ya uwanjani ambayo yalikuwa ni ushindi wa 2 – 1 kwa Kagera sugar yabaki kama yalivyo.”
Barua hiyo pia imeiruhusu simba kukata rufaa huku ikifuata taratibu za mchezo wa soka.
Kwa mantiki hiyo simba imepewa rungu la kuingilia FIFA.


Saturday, May 6, 2017

Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi Ya Tanzania Prisons


Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Prisons- VPL
1. Beno Kakolanya
2. Hassan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Juma Said
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Geofrey Mwashuiya

Akiba

Deogratius Munishi, Juma Abdul, Vicent Andrew, Mateo Antony, Deusi Kaseke, Emanuel Martin na Haruna Niyonzima.

Sunday, March 5, 2017

Kikosi cha Yanga leo dhidi ya Mtibwa Sugar


GK-Deogratias Msunishi-30
2. Hassan Hamis-25
3.Oscar Joshua-3
4. Nadir Haroub-23
5.Vincent Bossou-9
6.Kelvin Yondani-5
7.Saimon Msuva-27
8.Justine Zulu-14
9.Obrey Chirwa-7
10.Malimi Busungu-16
11.Emmanuel Martin-18
Sub:
Gk-Ali Mustafa-1
Mwinyi Haji-20
Andrew Vicent-28
Said Juma-22
Deus Kaseke-4

Geoffrey Mwashiuya-19

Friday, March 3, 2017

BREAKING NEWS: Hans Van Pluijm afungashiwa virago yanga.


Hans Van Pluijm afungashiwa virago yanga.
Hali ya ukata ndani ya kilabu ya Yanga imeingia sura mpya baada ya mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo kuachisha kazi rasmi leo.

Alipohojiwa Hans Van Pluijm alisema ““Nimepewa barua asubuhi hii na yanga juu ya mkataba wangu kuwa umesitishwa, kikubwa walichokisema ni kuwa klabu kwa sasa inakabiliwa na ukata hivyo hawana uwezo wa kuendelea kunilipa”.


Aliongeza kusema “Kwa sasa nipo huru kujiunga na klabu yeyote itakayoonyesha nia na mimi basi nitafanya nao kazi”
Hans Van Pluijm amekuwa Kocha wa YAnga na amedumu tangu 2014–2016 na amefanikiwa kuifikisha timu hiyo katika hatua ya makundi kombe la washindi barani Afrika msimu wa 2015/2016 kabla ya hivi karibuni kuja kwa kocha Lwandamina na kufanya yeye kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Thursday, March 2, 2017

ENGLAND: ratiba yote ya EPL march 4 2017


Manchester United vs AFC Bournemouth   15:30


Leicester City vs Hull City    18:00

Stoke City vs Middlesbrough   18:00

Swansea City vs Burnley   18:00

Watford vs Southampton    18:00

West Bromwich Albion vs Crystal Palace 18:00


Liverpool vs Arsenal    20:30

Saturday, February 25, 2017

Simba 2 - 1 Yanga, kichuya na Mavugo waleta furaha msimbazi


Magoli mawili ya Mavugo 67' na Kichuya 81' yameiwezesha timu ya simba kuibuka na ushindi wa goli 2 - 1 dhidi ya watani wao wajadi simba.

Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata goli 5' ya mchezo kufuatia uzembe wa beki wa simba Lufunga kuzembea kuhamisha mpira na kuzidiwa ujanja Chirwa wakati chirwa anaenda kufunga lufunga alimkwatua na kusababisha pigo la penati na kuzawadiwa kadi ya njano.

Msuva alipiga penati kiufundi na kuiandikia yanga goli la kuongoza.

simba walionekana kupotea na kushindwa kabisa kufika langoni mwa Yanga na Yanga walifika zaidi langoni mwa Simba lakini kukosa umakini kwa Safu ya ushambuliaji ya yanga kuliwanyima uongozi wa goli nyingi.

mpaka mapumziko yanga 1 - 0 simba na umilikaji wa mchezo ukiwa 49 kwa simba 51 kwa yanga.
kipindi cha pili dakika ya 51 simba walifanya mabadiliko yaliyoshtua baada ya kumtoa beki wa kati Lufunga na kuingia mshambuliaji Shiza Kichuya.

55' chirwa alimzidi ujanja beki Bukungu na kumzidi mbio lakini beki huyo alikubali yaishe alimkwatua  chirwa na kuzawadiwa kadi nyekundu.Yanga walipata faulo ambayo haikuzaa matunda.
mabadiliko ya kumtoa Ibram Mo na kuingia Mkude yaliwarudisha simba mchezoni na kusababisha kulimiliki vilivyo eneo la katikati na kuifanya yanga kupotea kabisa.

Mavugo alimalizia kazi nzuri toka wingi ya kulia iliyochongwa na shujaa wa mchezo wa leo Shiza Kichuya kwa kuunganisha kwa kichwa na kuifanya Simba kusawazisha goli hilo.

dakika ya 81 Shiza kichuya alishindilia msumari wa mwisho baada ya juhudi binafsi na kumchungulia kipa wa yanga Munish kisha kuupiga mpira upande wa kulia na kumshinda mlinda mlango huyo na kuipa simba ushindi huo mnono kwenye ligi ambao haijawi kuupata tangu 2015.

ikumbukwe 2016 simba ilikubali kupoteza michezo yote miwili na msimu huu mchezo wa kwanza waligawana pointi baada ya goli lililoleta utata la Amis Tambe na Kichuya kuiokoa simba dakika za lala salama.
Simba sasa imefikisha point 54 baada ya michezo 23 wakati Yanga wao wanapoint 49 baada ya mechi 22.
Yanga iliwakilishwa na:
1. Deogratius Munishi
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Vicent Andrew
5. Kelvin Yondani
6. Justine Zulu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Haruna Niyonzima
Akiba
- Ali Mustafa
- Hassani Kessy
- Nadir Haroub
- Geofrey Mwashuiya
- Deusi Kaseke
- Juma Mahadhi

Simba iliwakilishwa na:
1. Daniel Agyei
2. Besala Janvier Bkungu
3. Mohammed.Hussein
4. Novati Lufunga
5. Abdi Banda
6. James Kotei
7. Yassin Muzamiru
8. Mohammed Ibrahim
9. Ibrahim Ajib
10. Laudit Mavugo
11. Juma Liuzio

#Akiba
- Peter Manyika
- Hamad
- Saidi Ndemla
- Jonas Mkude
- Mwinyi Kazimoto

- Pastory Athanas

kikosi cha yanga dhidi ya simba leo hiki hapa


1. Deogratius Munishi

2. Juma Abdul

3. Mwinyi Haji

4. Vicent Andrew

5. Kelvin Yondani

6. Justine Zulu

7. Saimoni Msuva

8. Thabani Kamusoko

9. Amisi Tambwe

10. Obrey Chirwa

11. Haruna Niyonzima

#Akiba

- Ali Mustafa

- Hassani Kessy

- Nadir Haroub

- Geofrey Mwashuiya

- Deusi Kaseke


- Juma Mahadhi

kikosi cha simba dhidi ya yanga leo hiki hapa


Daniel Agyei

Besala Janvier Bkungu

Mohammed.Hussein

Novati Lufunga

Abdi Banda

James Kotei

Yassin Muzamiru

Mohammed Ibrahim

Ibrahim Ajib

Laudit Mavugo

Juma Liuzio

#Akiba
Peter Manyika

Hamad

Saidi Ndemla

Jonas Mkude

Mwinyi Kazimoto


Pastory Athanas

Friday, February 24, 2017

Simba Vs Yanga:Lwandamina, Omog Watambiana

Februari 25, ni siku inayosubiriwa kwa hamu kubwa kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla, ambapo watani wa jadi, klabu za Simba na Yanga zinatarajia kumenyana katika uwanja wa taifa katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League (VPL) Msimu wa 2016/17.


Ukubwa wa mechi hiyo si tu unatokana na utani uliopo baina ya timu hizo bali pia, hali halisi ya msimamo wa ligi hivi sasa, ambapo tofauti ya pointi kati ya klabu hizo ni pointi moja tu, Simba wakiwa kileleni baada ya kujikusanyia alama 51 katika michezo 22 waliyocheza, huku mahasimu wao Yanga wakishika nafasi ya pili kwa kujikusanyia jumla ya alama 49 katika michezo 21 waliyocheza.

Kuelekea mchezo huo kumekuwa na majigambo mengi kutoka kwa mashabiki wa kila timu wakiamini timu yao ndio itaibuka na ushindi katika mchezo huo, na kwa jinsi hali ilivyo na ushindani mkubwa uliopo katika ligi msimu huu wa 2016/17, mechi hiyo inasemwa kuwa ndio inayoweza kutoa mwangaza wa nani anaweza kuibuka bingwa wa ligi kuu kwa msimu huu, hali ambayo inaongeza ugumu wa pambano hilo.

Makocha wa timu zote mbili wametoa kauli zao kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho Jumamosi, Feb. 25 katika uwanja wa Taifa jijini Dar.

“Ukweli kwamba ubingwa wetu msimu huu upo kwenye mchezo dhidi ya Yanga, na tumejipanga kuhakikisha tunashinda hatupo tayari kuona tuna tunafungwa au kutoka sare kwasababu huo ndiyo mchezo pekee mgumu kwetu na endapo tutawafunga itakuwa tumewaacha idadi kubwa ya pointi,”amekaririwa Omog.

Kwa upande wake nae kocha mkuu wa Yanga amesema kitu kikubwa kwao na cha msingi zaidi ni kuiondoa Simba katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

“Kitu cha msingi kwetu kabla ya kuwaza ubingwa ni kuiondoa Simba, kwenye nafasi ya kwanza na hilo nina uhakika tunaweza kulitimiza katika mechi tatu zijazo, kutokana na ari tuliyokuwa nayo hivisasa na idadi ndogo ya pointi tuliyokuwa nayo kati yetu na wao,” alikaririwa Lwandamina.

Thursday, February 23, 2017

Kwa Heri Claudio Ranieri


Claudio Ranieri afungashiwa virago Kutokana na mwenendo mbovu wa Matokeo kwenye kilabu ya Leicester City.
Msimu huu kila timu imecheza michezo 25, na anaeongoza ligi Chelsea ana pointi 60, wakati bingwa mtetezi akiwa na pointi 21 tu. Yaani amezidiwa jumla pointi 42 na kinara wa ligi.

Kwa mwenendo huo mbovu kuanzia leo rasmi Ranieri sio kocha tena wa Leicester City.

Makamu mwenyekiti wa Leicester City Aiyawatt Srivaddhanaprabha amesema”yamekuwa maamuzi ya kwanza magumu kuyafanya ndani ya kipindi cha miaka saba”.

Jedwali lifuatalo linaonyesha Matokeo ya  Leicester City chini ya kocha Claudio Ranieri baada ya  25
Msimu
Nafasi
Kushinda
Kufungwa
Magoli Kufunga
Magoli kufungwa
pointi
2015/2016
1
15
2
47
27
53
2016/2017
17
5
14
24
43
21





Kaseja mchezaji bora ligi kuu Tanzania Bara mwezi January

                                                                    kaseja

Golikipa wa timu ya Kagera sugar ya mkoani Kagera Juma Kaseja ametwaa tuzo ya mchezaji bora ya mwezi January ambayo hutolewa kila mwezi na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.

Katika kinyang’anyiro hicho Kaseja aliwashinda Jamal S. Mtengeta wa Toto Africans ya Mwanza na Mbaraka Abeid wa Kagera Sugar.

Kaseja atakabidhiwa kitita cha shilingi milioni moja ya kitanzania na wadhamini Vodacom.

Katika mwezi January Kagera imecheza michezo mitatu na kushinda yote na kuweza kutoka nafasi ya tano hadi ya 3.


Katika michezo yote mitatu kaseja alisimama langoni na kuruhusu goli moja pekee huku Kagera wakifunga jumla ya goli 6.

Saturday, February 18, 2017

Simba yajifua Zanzibar kuelekea february 25


Timu ya Simba jana imeondoka kwenda visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wake wa February 25 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.

Simba ambayo ndio inayoongoza ligi kwa kujikusanyia point 51 katika michezo 22, watani zao Yanga wao wapo nafasi ya pili baada ya kushuka uwanjani mara 21 na kujikusanyia pointi 49.

Simba ambayo inajiwinda pengine iweze kuondoa mkosi wa kukaa nje ya mashindani ya kimataifa yanayotambuliwa na shirikisho la soka barani Afrika kwa takribani miaka minne mfululizo, wanafanya mazoezi asubuhi na jioni kwa kusuduo la kuwaweka sawa wachezaji wao kisaikolojia na kimbinu ili kuhakikisha wanaimaliza Yanga.

Simba ambayo jana imetoka kuitoa Africans Lyon katika kuwania kombe la shirikisho Tanzania na badae walianza safari ya kuelekea Kisiwani.

Huenda mchezo huo ukatoataswira ya timu gani itakuwa bingwa msimu huu.

Yanga na Azam ndio timu ambazo kwa miaka minne mfululizo zinapata tiketi ya kupanda ndege kwenda kwenye mashindano makubwa ya bara la Afrika yaani Kombe la shirikisho na kombe la mabingwa kwa ngazi ya vilabu.

Msimu uliopita timu ya Yanga ilibahatika kutinga katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho na kushika mkia katika kundi lake.

Kitu kizuri kwa upande wa simba nikuwa Hakuna majeruhi.


Wednesday, February 8, 2017

George Lwandamina Aifungukia Simba SC

Kocha wa mabingwa soka Tanzania bara Timu ya Yanga Mzambia George Lwandamina ametamba kwamba mechi dhidi ya timu ya Ngaya Club ya Comoro katika mchezo wa klabu bingwa afrika zitawapa taswira nzuri kabla ya kuvaana na maasimu wao Timu ya Simba Februari 25, mwaka huu katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Yanga inatarajia kuchuana na Simba Februari 25, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam .
Kwa sasa Yanga wapo kileleni mwa Ligi hiyo kwa alama 49, wakifuatiwa na Simba yenye alama 48 baada ya timu zote kucheza michezo 21.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Januari 10, mwaka huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar na Simba ikashinda kwa penalty 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90

Rungu La TFF Latua Kwa Hemed Morocco

Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Morocco kushiriki michezo mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000.

atika mechi Na. 160 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu za JKT Ruvu na Stand United iliyochezwa Januari 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Morocco aliondolewa kwenye benchi (Ordered off) kwa kosa la kupinga maamuzi ya mwamuzi na kutoa lugha chafu.

Kamati hiyo ya Saa 72 imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 40 (11) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Makocha.

Morocco hata kama atakuwa amemaliza mechi tatu nje ya benchi, hataruhusiwa kukaa kwenye benchi hadi awe amelipa faini hiyo.

Adhabu hiyo ya Morocco itaendelea kumhusu hata kama utakuwa umehamia kwenye timu nyingine na katika msimu mwingine wowote

Jamhuri Kihwelu "Julio" Aomba Kibarua Simba

Kocha mkuu wa zamani wa klabu ya Mwadui ya mjini Shinyanga, Jamhuri Kihwelu, ameweka bayana kuwa yupo tayari kurudi kuitumikia Simba katika nafasi ya ukatibu mkuu.

Julio amesema kuwa hana wasiwasi na yupo tayari kuitumikia klabu hiyo endapo tu uongozi wa Simba utaridhia kumpa nafasi hiyo.

"Siyo kama najipigia chapuo lakini kama viongozi wa Simba wakiamua kunipa nafasi ya ukatibu sitaweza kukataa kwa sababu naipenda timu hiyo na kila mmoja anajua na kama nikiwepo naamini nitaongezea kitu fulani na kuifanya timu ipate matokeo mazuri"

Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Patrick Kahemela ambaye kwa sasa amekuwa mkurugenzi wa michezo katika kituo cha runinga cha Azam. Aidha, Julio ameongeza kuwa, uzuri wake yeye ni kwamba hakufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na mpira wa miguu isipokuwa ni yeye mwenyewe tu ndiye aliamua kukaa pembeni kutojihusisha na maswala hayo.

“Uzuri wangu kwangu kwamba sikufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na soka hivyo hata nikirejea hakuna ambaye atashtuka na niwaahidi kwamba nitaitumikia nafasi hiyo kuleta mabadiliko yaliyoshindikana kwa kipindi kirefu,” alisema Julio akizungumza na Championi

Tuesday, January 31, 2017

Kocha Mwadui Aitabiria Ubingwa Yanga

Kocha wa klabu ya Mwadui FC, Ali Bushiri ameitabiria ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara (VPL 2016/17) klabu ya Yanga kufuatia kandanda safi liliopigwa na vijana hao wa Jangawani wakati timu yake ya Mwadui FC ilipolala kwa jumla ya mabao 2-0 katika uwanja wa taifa jijini Daresalaam.

Kocha huyo alisema kikosi chake kilizidiwa katika sehemu kubwa na mabingwa hao watetezi kitu kilichowalazimu kucheza kwa kujilinda zaidi kwa kuhofia kufungwa mabao mengi.

“Ukweli tuliingia kwenye mchezo huu tukihitaji angalau sare, lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda wenzetu walizidi kuja kutushambulia hatimaye wakapata walichokuwa wanakitaka,” amesema Bushiri ambaye ameichukua timu hiyo kwenye mzunguko wa pili akiziba nafasi ya Jamhuri Kihwelo.

Aidha kocha huyo alieleza kuwa, katika mchezo huo, timu yake ilizidiwa kimbinu na kibaya zaidi asilimia kubwa ya wachezaji wake hawana uzoefu mkubwa ukilinganisha na wale wa kikosi cha Yanga.