Yanga Yainyoosha Azam Fc Chamanzi

Azam FC 1 - 2 Young Africans.

Kiungo Wa Everton James McCathy Avunjika Mguu

Kiungo James McCarthy wa Everton sasa atakaa nje na kuukosa msimu wote huh baada ya kuvunjika mifupa miwili ya mguu wake.

DRAW CAF CL And CC 2018

Draw Caf Cl and CC 2018

Yanga Yazinduka Yaambulia Ushindi Mwembamba

Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa goli moja kwa sifuri

Madrid Yaivurumisha Deportivo 7-1

Klabu ya Real Madrid leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono kwa jumla ya magoli 7-1 dhidi ya Klabu Deportivo la Coruna

Showing posts with label Kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Kitaifa. Show all posts

Sunday, January 28, 2018

Hiki Ndo Kikosi Cha Kocha Mfaransa Simba Ikiivaa Majimaji Leo Taifa


Ligi Kuu Vodacom, Tanzania Bara

Mechi:Simba V Majimaji
Mahali:Uwanja Wa Taifa
Muda: Saa 10:00 Jioni



Kikosi Cha Simba Leo


Sunday, January 21, 2018

Kikosi Cha Yanga Dhidi Ya Ruvu Shooting Leo


Wednesday, June 14, 2017

Usajili Wa Kwanza Wa Yanga Huu Hapa

Yanga imekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka katika klabu ya Taifa jang'ombe, Abdalla Haji Shaibu.


Beki  wa timu ya Taifa ya Jang"ombe Abdallah Haji Shaibu "Ninja" amesaini mkataba wa miaka 2 kuwatumikia mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Tanzania bara klabu ya Yanga.

Monday, June 5, 2017

Kikosi Cha Yanga Dhidi Ya Tusker Leo

SPORTPESA SUPER CUP

KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA TUSKER LEO
1.Deo Dida
2.Juma Abdull
3.Emanuel Kichiba
4.Andrew Vicent 
5.Nadir Canavaro
6.Babu Ally 
7.Yusuph Mhilu
8.Maka 
9.Obby Chirwa 
10.Juma Mahadhi 
11.Emanuel Martin

Sub; 
Bakary Osman. 
Mohamed Ally. 
Rahim Shea.
Said Mussa. 
Samuel Greyson 
Pato Ngonyani

Saturday, June 3, 2017

Yote Yanayoihusu Azam FC;Usajili, Waliotemwa Wanaoingia Na Mipango Msimu Ujao

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuwataarifu wapenzi na mashabiki wa soka nchini kuwa imebadilisha mfumo wa usajili uliokuwa ikiutumia awali wa kusajili wachezaji kwa gharama kubwa na sasa ikijikita kwenye kufanya matumizi ya wastani pamoja na kuwatumia ipasavyo nyota watakaozalishwa kutoka kituo chao ‘Azam Academy’.


Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd, leo imeeleza kuwa kuelekea msimu ujao na kuendelea, Azam FC itaweka msisitizo na kufanya uwekezaji ipasavyo kwenye kituo chake cha kukuza vipaji ‘Azam Academy’ ili kuvuna wachezaji bora watakaopandishwa katika kikosi cha timu kubwa.

Kwa kuanzia katika kutekeleza malengo hayo, kuelekea msimu ujao Azam FC imewapandisha wachezaji sita kutoka kwenye kituo chake, ambao ni mabeki Abbas Kapombe, Abdul Haji, Godfrey Elias, kiraka Ramadhan Mohamed, kiungo Stanslaus Ladislaus na mshambuliaji Yahaya Zaid, aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Daraja Kwanza (FDL) msimu uliopita kwa mabao tisa aliyofunga alipokuwa kwa mkopo Ashanti United.

Azam FC imekuwa na utaratibu mzuri wa kulea wachezaji wake vijana kwa kuwapandisha kwenye timu kubwa, ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuibeba timu, ambapo wengine waliopo katika kikosi cha wakubwa ni makipa Aishi Manula, Metacha Mnata, mabeki Gadiel Michael, Ismail Gambo, kiungo Mudathir Yahya, Abdallah Masoud, Himid Mao, Joseph Mahundi na mshambuliaji Shaaban Idd.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, aliyeongezewa mkataba wa mwaka mmoja, anaamini ya kuwa wachezaji hao vijana watazidi kukiimarisha kikosi chake kwa kushirikiana na wachezaji wazoefu waliopo kikosini, hadi anafikia uamuzi huo wa kuwapandisha aliwafuatilia katika mechi mbalimbali za timu ya vijana ikiwemo na baadhi ya siku kuwajumuisha katika mazoezi ya timu kubwa.

Aidha kuhusiana na wachezaji waliomaliza mikataba yao, Azam FC imethibitisha rasmi kuachana na winga wake Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ame Ally, aliyekuwa kwa mkopo Kagera Sugar, wote mikataba yao ikiwa imemalizika.

Mabadiliko kwenye mfumo wa uongozi

Katika hatua nyingine, Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC imefanya mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi ya timu hiyo kwa kukifuta cheo cha Ofisa Mtendaji Mkuu, na sasa cheo cha juu kitakuwa ni Meneja Mkuu, nafasi inayoshikiliwa na Abdul Mohamed.

Kutokana na mabadiliko hayo ya kiutendaji, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, amemaliza mkataba wake na pande zote mbili zimekubaliana kuachana, na sasa majumuku yake yote yatafanywa na Abdul Mohammed, akiwa ndio Meneja Mkuu wa klabu.

Chanzo: Azam FC Official Site

Friday, June 2, 2017

Wachezaji Yanga Kujazwa Mamilioni

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameahidi kuwalipa wachezaji wake mishahara yao ya miezi minne wanayodai kabla ya kuanza kwa michuano ya Sportspesa Super Cup.


Kauli hiyo inakuja baada ya kuwepo kwa taarifa za wachezaji wa Yanga kutaka kususia michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi jumatatu Juni 5/17.

Mkwasa amesema kamati ya utendaji ya timu hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha malipo ya mishahara ya miezi minne ambayo wachezaji pamoja na wafanyakazi wa timu hiyo hawajalipwa hadi hivi sasa.

“Ni kweli kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale, lakini kabla ya kuanza michuano ya Super Cup kila kitu kitakuwa kimemalizika,” alisema Mkwasa.

“Mwalimu amekabidhi ripoti yake juzi, kipindi hiki tunaipitia na baadaye tutaanza makeke yetu ya usajili,” alisema Mkwasa.

Hadi hivi sasa wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao katika kikosi hicho cha Yanga ni Vicent Bossou, Mwinyi Haji, Donald Ngoma, Deus Kaseke, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima pamoja na Amisi Tambwe.

Simba Wapata Mbadala Wa Juuko Murshid

Munezero Fiston ni Mnyarwanda ambaye yupo katika mipango ya Simba baada ya kocha Joseph Omog kupendekeza atafutiwe mchezaji mwingine.


Munezero, anayekipiga katika klabu ya Rayon Sport anatarajiwa kutua Dar Es Salaam Jumamosi hii kwa lengo la kufanya mazungumzo na wekundu hao wa Msimbazi.

Hatua hii inakuja baada ya taarifa za kuomba kuondoka kwa beki Juuko Murshid pamoja na hali ya majeraha inayomsumbua Method mwanjali hivyo kuonekana kuna kila sababu ya kupata mbadala wa nyota hao.


“Munezero atawasili rasmi Jumamosi hii. Tunaweza kumtumia kwenye michuano ya Super Cup, mashabiki wetu watapata nafasi ya kumuona hapo,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

Pamoja na beki huyo, Simba ina mpango wa kusajili wachezaji wengine watatu, ambao ni kiungo, mshambuliaji na beki mwingine kujenga ukuta imara kwenye kikosi hicho.

Thursday, June 1, 2017

Asante Kwasi Kujiunga Na Yanga SC

Beki wa timu ya Mbao FC, Asante Kwasi amesema angetamani kuichezea Yanga katika msimu ujao wa ligi.


Beki huyo wa kati wa Mbao ameyasema hayo kutokana na kuvutiwa na kiwango na mafanikio ya klabu ya Yanga mabingwa mara tatu mfululizo wa ligi soka Tanzania Bara.

Kwasi kwa sasa amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliokuwa nao katika klabu yake ya Mbao FC na ameweka wazi kuwa anapenda kujiunga na timu nyingine kubwa kama Yanga au Azam FC. Mghana huyo amedai kwa kipindi ambacho ameishi nchini amegundua kuwa Yanga ndiyo klabu yenye mafanikio hivyo kumfanya yeye kuvutiwa kucheza katika klabu hiyo.

“Yanga nimeambiwa ndiyo timu inayoongoza kwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu, mara nyingi lakini pia ndiyo timu ambayo imeshiriki mara nyingi michuano ya kimataifa ukweli nimevutiwa na hilo na siku zote natamani kucheza timu yenye mafanikio kwasababu naamini ndiyo njia nyepesi ya kufika ninapopataka,”amesema Kwasi.

Beki huyo aliyeonyesha uwezo mkubwa katika msimu wa ligi uliomalizika amedai kuwa mpaka sasa bado hajajua ni timu gani ataichezea msimu ujao lakini angefurahi sana kama angetua Jangwani.

Usipitwe na habari za papo kwa papo za Usajili, Ungana na Soka24 kupata kila kinachojiri katika ulimwengu wa Soka Ulimwenguni.

Sunday, May 7, 2017

Kikosi Cha Simba Leo Dhidi ya African Lyon



  1. Agyei
  2. Bukungu
  3. Zimbwe Jr
  4. Kotei
  5. Murshid
  6. mkude
  7. Kichuya
  8. Mzamiru
  9. Mavugo
  10. Ajib
  11. Mo Ibrahim


Wachezaji wa Akiba
Novati,Manyika, Vicent, Kazimoto, Luizio, Blagnon, Paschal

VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO UPANDE WA MICHEZO JUMAPILI MAY 7 2017

















Safari ya Simba kuishtaki TFF FIFA imeiva ni baada ya jana kupewa barua yao rasmi ya kupokwa pointi 3 na bodi ys ligi.


Bodi ya ligi nchini ‘TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARDS(TPLB)’ jana imeshindilia kaa la moto katika maamuzi yake ya kipoka timu ya Kagera Sugar pointi 3 na magoli 3 kwa kosa la kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi kwa kusema Fakhi wakati anaichezea Kagera Sugar hakuwa na kadi tatu za njano.
Vionjo vilivyo kwenye Barua hiyo ni kama ifuatavyo ”TFF ndio yenye dhamana ya usimamizi wa mpira nchini na ambayo ndio iliyokasimu madaraka kwa TPLB kuendesha ligi kuu” barua iliiendelea kwa sema “baada ya uchunguzi wao ambao ulihoji watu mbalimbali wamebaini kuwa mchezaji Mohamed Fakhi alielalamikiwa na Simba hakuwa na kadi 3 za njano siku ya mchezo wa Kagera sugar na Simba, kwa mantiki hiyo maamuzi yaliyofanywa na kamati ya kuipoka pointi Kagera hayakuwa sahihi na hivyo Matokeo ya uwanjani ambayo yalikuwa ni ushindi wa 2 – 1 kwa Kagera sugar yabaki kama yalivyo.”
Barua hiyo pia imeiruhusu simba kukata rufaa huku ikifuata taratibu za mchezo wa soka.
Kwa mantiki hiyo simba imepewa rungu la kuingilia FIFA.


Saturday, May 6, 2017

MSOLOPA Kulipiga Mnada Jengo La Yanga


KAMPUNI ya udalali ya MSOLOPA imepewa jukumu la kusimamia mchakato wa kuuzwa kwa jengo la Yanga SC endapo klabu hiyo itashindwa kulipa deni la kodi milioni 300, deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo.

"Ni kweli kesi iko katika Mahakama ya Ardhi na tumeshaanza kuifanyia kazi, lakini tunaamini tutalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo haujafanyika" alisema Mkwasa.

Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi Ya Tanzania Prisons


Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Prisons- VPL
1. Beno Kakolanya
2. Hassan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Juma Said
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Geofrey Mwashuiya

Akiba

Deogratius Munishi, Juma Abdul, Vicent Andrew, Mateo Antony, Deusi Kaseke, Emanuel Martin na Haruna Niyonzima.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea leoJumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, 2017


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea leoJumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, mwaka huu kwa jumla ya michezo sita kupigwa mikoa tofauti
Jumamosi hii itapigwa michezo mitano katika mikoa minne tofauti.
Dar es salaam.
Yanga vs Tanzania Prisons  Uwanja wa Taifa
Azam vs Mbao Fc   Azam Uwanja Complex Chamanzi
Pwani
Ruvu Shooting vs Kagera Sugar  Uwanja Mabatini
Mwanza
Toto African vs JKT Ruvu Uwanja CCM Kirumba
Ruvuma
Majimaji vs Mwadui Uwanja wa Majimaji
Kesho jumapili 7 may
Simba SC vs African Lyon Uwanja wa Taifa


Tuesday, March 28, 2017

Tambwe wa Yanga Morris wa Azam fit kwa pambanano April 1


Wakati zikiwa zimebakia siku 4  jumamosi April 1, kwa mchezo unaosubiriwa kwa hamu kati ya mabingwa wa ligi kuu Tanzania timu ya Yanga na mabingwa wa Afrika mashariki na kati timu ya Azam  habari njema ni kupona kwa wachezaji muhimu wa timu hizo.

Wednesday, March 15, 2017

Tuesday, March 7, 2017

Ratiba robo fainali Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)



Ratiba hiyo iliyotelewa mapema leo imepangwa kama ifuatvyo:

March 18 Madini fc wataikaribisha Simba Sc katika dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha, siku hiyohiyo ya Tarehe march 18 Kagera Sugar itaialika Mbao ndani ya Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

Michezo miwili iliyobaki ni kati ya Azam FC watakapoikaribisha Ndanda fc toka Mtwara katika dimba la chamanzi.

Yanga wataikaribisha Tanzania Prisons katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Michezo kati ya Azam na Ndanda, Yanga na Prisons haijapangiwa ni lini itafanyika Kutokana na Yanga kushiriki michuano ya kilabu bingwa barani Afrika huku Azam wao wakishiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.


Mshindi wa michuano hiyo kikanuni anatarajia kujishindia kombe pamoja na kitita cha Sh. milioni 50 na kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Madini vs Simba 
Kagera vs Mbao
Yanga vs Prisons
Azam vs Ndanda

Monday, March 6, 2017

Yanga vs Kiluvya fc kesho Taifa 16 bora ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Sports Federation Cup)


Kilvya na Yanga kesho kuamua ni timu gani iingie robo fainali kuungana na timu saba ambazo zimefuzu kwa hatua hiyo.

Bingwa wa michuano hii ndie anaeiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, pia hujinyakulia kitita cha shilingi milion 50 za kitanzania.


Timu saba ambazo zimefuzu kwa hatua ya robo fainali ni Tanzania Prisons ya Mbeya, Ndanda FC ya Mtwara, Azam FC ya Dar es Salaam, Madini ya Arusha, Simba ya Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba.