Showing posts with label Azam Sports Federation Cup. Show all posts
Showing posts with label Azam Sports Federation Cup. Show all posts
Sunday, March 19, 2017
Tuesday, March 7, 2017
Ratiba robo fainali Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)
Ratiba hiyo iliyotelewa mapema leo imepangwa kama ifuatvyo:
March 18 Madini fc wataikaribisha Simba Sc katika dimba la Sheikh
Amri Abeid, Arusha, siku hiyohiyo ya Tarehe march 18 Kagera Sugar itaialika
Mbao ndani ya Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Michezo miwili iliyobaki ni kati ya Azam FC watakapoikaribisha
Ndanda fc toka Mtwara katika dimba la chamanzi.
Yanga wataikaribisha Tanzania Prisons katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Michezo kati ya Azam na Ndanda, Yanga na Prisons
haijapangiwa ni lini itafanyika Kutokana na Yanga kushiriki michuano ya kilabu
bingwa barani Afrika huku Azam wao wakishiriki michuano ya kombe la shirikisho
barani Afrika.
Mshindi wa michuano hiyo kikanuni anatarajia kujishindia
kombe pamoja na kitita cha Sh. milioni 50 na kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye
Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Madini vs Simba
Kagera vs Mbao
Yanga vs Prisons
Azam vs Ndanda
Monday, March 6, 2017
Yanga vs Kiluvya fc kesho Taifa 16 bora ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Sports Federation Cup)
Kilvya na Yanga kesho kuamua ni timu gani iingie robo
fainali kuungana na timu saba ambazo zimefuzu kwa hatua hiyo.
Bingwa wa michuano hii ndie anaeiwakilisha nchi katika
michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, pia hujinyakulia kitita cha
shilingi milion 50 za kitanzania.
Timu saba ambazo zimefuzu kwa hatua ya robo fainali ni Tanzania
Prisons ya Mbeya, Ndanda FC ya Mtwara, Azam FC ya Dar es Salaam, Madini ya
Arusha, Simba ya Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba.
Monday, February 6, 2017
16 Bora Azam Federation Cup ratiba yatangazwa, michezo 8 kufanyika kwa siku tatu tofauti

Michuano ya
kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) hatua ya 16 bora kutimua vumbi
February 24 na February 26 na march 7 katika mikoa sita ya Tanzania Bara.
February 24
kutakuwa na michezo minne katika mikoa minne tofauti
Mkoani Arusha
Katika dimba
la Sheikh Amri Abeid wenyeji timu ya Madini Fc watawakaribisha maafande
wa JKT Ruvu
Mkoani Dar es Salaam
Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati Azam Fc watailika timu
ngumu ya Mtibwa Sugar katika dimba lao la nyumbani (Azam Complex, Chamaz).
Azam ndio makamu
bingwa wa michuano hiyo kwa msimu uliopita baada ya kupokea kichapo cha goli 3 –
1 kutoka kwa Yanga.
Mkoani Kagera
Timu ya
Kagera sugar wataikaribisha timu ya Stand United katika dimba Kaitaba.
Mkoani
Ruvuma
Timu za Mighty Elephant mkoani humo itawaalika wanakuchele Ndanda
kutoka Mtwara katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Raundi hiyo ya 16 itaendelea tena siku ya jumapili February 26
katika mikoa mitatu.
Mkoani Dar
es Salaam
Timu ya Simba
itavaana na timu African Lyon katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Mkoani Mwanza
Kutakuwa na
Mwanza derby wakati Mbao FC itakapoonyeshana ubabe na kaka zao Toto
Africans katika Uwanja wa CCM Kirumba
Mkoani
Mbeya
Derby nyingine
itakuwa mkoani Mbeya wakati timu mbili za mkoani humo Tanzania Prisons
na Mbeya City zitakapomenyana kuwania kuingia roba fainali ya michuano hiyo
March 7
Mabingwa wa michuano hiyo kwa msimu uliopita timu ya Yanga
wao wataialika timu ya Kiluvya kutoka mkoani pwani katika dimba kuu la Uwanja wa
Taifa jiji Dar es Salaam
bingwa wa michuano hii ndie atakaeiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika 2018.
Thursday, January 26, 2017
Rufaa ya polisi Dar es Salaam dhidi ya mchezaji wa simba Novalty Lufunga kucheza huku akiwa na kadi nyekundu yagonga mwamba

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania limeitupilia
mbali rufaa ya timu ya polisi Dar es salaam waliokata kutaka wapewe ushindi
katika mchezo wao wa raundi ya tano ambao simba ilishinda kwa 2 -0,
Mchezaji Novalty Lufunga aliekatiwa rufaa alipata kadi nyekundu
katika mchezo wa mwisho kwa simba wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016 ambapo
simba ililala katika mchezo huo wa 11april 2016 kuondoshwa mashindanoni.
Kanuni za Azam Sports
Federation Cup zinaweka wazi kuwa kadi ya njano au nyekundu inaisha pale tu
mashindano husika yanapoisha labda itokee kadi hiyo imeongezewa na adhabu nyingine,
kama itakuwa imeongezewa adhabu basi klabu na mchezaji watataarifiwa kwa maandishi.
Hivyo basi kwa kanuni hiyo ya mashindano polisi Dar itakuwa
imetupwa nje rasmi katika mashindano hao ya Azam Sports Federation Cup













