Yanga Yainyoosha Azam Fc Chamanzi

Azam FC 1 - 2 Young Africans.

Kiungo Wa Everton James McCathy Avunjika Mguu

Kiungo James McCarthy wa Everton sasa atakaa nje na kuukosa msimu wote huh baada ya kuvunjika mifupa miwili ya mguu wake.

DRAW CAF CL And CC 2018

Draw Caf Cl and CC 2018

Yanga Yazinduka Yaambulia Ushindi Mwembamba

Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa goli moja kwa sifuri

Madrid Yaivurumisha Deportivo 7-1

Klabu ya Real Madrid leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono kwa jumla ya magoli 7-1 dhidi ya Klabu Deportivo la Coruna

Showing posts with label Euro. Show all posts
Showing posts with label Euro. Show all posts

Tuesday, July 12, 2016

VIDEO: TAZAMA URENO WALIVYOPOKELEWA KISHUJAA

Monday, July 11, 2016

ALICHOPOST MOURINHO INSTAGRAM BAADA YA URENO KUTWAA EURO

Katika kuonyesha furaha yake Jose Mourinho kufuatia ushindi walioupata Ureno katika fainali ya Euro 2016, Kocha huyo wa Man United amepost picha huku akiisindikiza na maneno yanasomeka hivi;  "Kama unataka kutembelea taifa la mabingwa wa Ulaya, tembelea Ureno"

Mourinho aliwahi kuingoza FC Porto mwaka 2004 kushinda taji la klabu bingwa barani ulaya (UEFA Champions League)  wakati ambao Porto ilikuwa ikichukuliwa kama kibonde kwenye mashindano hayo.

Ureno imeshinda mechi moja tu ndani ya dakika 90 za mchezo katika mechi zote walizocheza katika michuano ya Euro 2016, huku ikitoa sare tatu katika hatua ya makundi na ushindi ndani ya dakika 30 za nyongeza dhidi ya Crotia na Ufaransa pamoja na Penati dhidi ya Poland.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

Tuesday, July 5, 2016

SHABIKI WA RONALDO APIGWA FAINI

Shabiki aliyevamia uwanjani na kumkumbatia Christiano Ronaldo wakati wa mechi ya robo fainali kati Ureno na Poland amepigwa faini ya paundi 500.

Katika mechi ya robo fainali kati ya Ureno na Poland shabiki mmoja wa Ureno aliingia uwanjani na kumkumbatia Christiano Ronaldo kabla ya kutolewa nje na wanausalama uwanjani hapo.
Shamshir Karimi 22, amezuiwa pia kuingia Ufaransa mwezi ujao.

Akitoa utetezi wake mahakamani shabiki huyo alisema alivamia uwanjani hapo kwa kuwa anamapenzi makubwa na Ronaldo.

Tukio hilo lilitokea katika dakikaya 110 ya mchezo na hiyo si mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea kwa mashabiki kutaka kukutana na Ronaldo wakati mchezo unaendelea.

Shabiki mwingine alivamia uwanjani na kwenda kwa Ronaldo katika mchezo kati ya Ureno na Austria na kwa bahati nzuri lengo lake lilitimia baada ya kukubaliwa kupiga picha ya pamoja na Ronaldo.

Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook


FIFA YAKATAZA WACHEZAJI KUSHEREHEKEA NA FAMILIA ZAO UWANJANI

Fifa inapanga kuzuia kitendo cha wachezaji kusherehekea ushindi na familia zao uwanjani katika michuano ya Euro inayoendelea huko nchini Ufaransa.

Mkurugenzi wa mashindano hayo Martin Kallen amesema zuio hilo ni kutokana na sababu za kiusalama.

"Hatupingi suala hili moja kwa moja, bali tunatakiwa kuchukua tahadhari na kuhakikisha usalama" alisema Kallen.

"Ni mashindano ya Ulaya na sio ya sherehe za kifamilia, uwanjani sio sehemu salama kwa watoto wadogo,watu wenye vibali maalumu tu ndo wataruhusiwa kuingia uwanjani na sio mtu mwingine yoyote " aliongeza Mkurugenzi huyo.

Akizungumzia uwanja wa Stade de France ambao ndio utachezwa fainali ya michuano hiyo, Kallen alisema kila kitu kiko sawa na uwanja upo tayari kwa fainali hiyo.

"Hakutakuwa na tatizo lolote na kwa mechi zilizochezwa hivi karibuni tumeona kwamba uwanja wa Stade de France unaubora mzuri sana" alisema Kallen

Aidha Mkurugenzi huyo alilitolea ufafanuzi suala la timu kuzuiwa kufanya mazoezi katika viwanja vinavyochezwa baadhi ya mechi Kallen alisisitiza kwamba kulikuwa na suala la nyasi kutumiwa sana na ndio sababu iliyopelekea kuweka katazo hilo.

Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

Tuesday, June 28, 2016

VIDEO:WALES WALIVYOSHANGILIA BAADA YA UINGEREZA KUTOLEWA EURO 2016

Tazama Video hii hapa chini

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa


ROY HODGSON AJIUZULU TIMU YA TAIFA UINGEREZA

Kocha wa England Roy Hodgson amejiuzulu nafasi yake kufuatia kutolea kwa timu yake katika michuano ya Euro walipokubali kipigo cha goli 2 - 1 kutoka kwa Iceland.

Hodgson 68 amekuwa kocha wa Uingereza kwa muda wa miaka minne baada ya kuchukua nafasi ya Fabio Capello na amefanikiwa kushinda mechi 3 tu kati ya 11 alizoshiriki katika fainali za michuano mbalimbali.
Iceland yenye idadi ya watu 330,000 ilikuwa ni miongoni mwa timu ambazo hazikupewa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hiyo.

"Sasa ni muda wa mtu mwingine kuangalia maendeleo ya kundi la wachezaji wenye njaa ya ubingwa na vipaji vikubwa" alisema Hodgson.
"Wamefanya kazi kubwa na kila nilichowaambia wafanye. Ni matumaini yangu kuwa mutaendelea kuiona Uingereza katika fainali za michuano mikubwa zaidi hivi karibuni" aliongeza kocha huyo ambaye amefanikiwa kushinda mechi 33 tu kati ya mechi 56 ambazo Uingereza imecheza yeye akiwa kocha mkuu.

Wanaodhaniwa kuchukua mikoba ya Hodgson ni kocha wa timu ya vijana ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 aliyekuwa kocha wa zamani wa Middlesbrough Gareth Southgate, Wengine ni Gary Neville, Meneja wa Crystal Palace Alan Pardew, Meneja wa Bournemouth Eddie Howe na kocha mpya wa Celtic Brendan Rodgers, Arsene Wenger pamoja na Jose Mourinho wote wanahusishwa kurithi mikoba ya Roy Hodgson.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

Wednesday, June 22, 2016

RATIBA EURO 2016 HATUA YA MTOANO


Match 1: Switzerland v Poland – Jumamosi 25 June, 15:00 (Saint-Etienne)
Match 2: Wales v third place A/C/D – Jumamosi 25 June, 18:00 (Paris)
Match 3: Croatia v third place B/E/F – Jumamosi 25 June, 21:00 (Lens)
Match 4: France v third place C/D/E – Jumapili 26 June, 15:00 (Lyon)
Match 5: Germany v third place A/B/F – Jumapili 26 June, 18:00 (Lille)
Match 6: winner F v runner-up E – Jumapili 26 June, 21:00 (Toulouse)
Match 7: Italy v Spain – Jumatatu 27 June, 18:00 (Saint-Denis)
Match 8: England v runner-up F – Jumatatu 27 June, 21:00 (Nice)


Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa




ZILIZOTINGA HATUA YA MTOANO HADI SASA EURO 2016


ZILIZOTINGA HATUA YA 16 BORA

1.Switzerland
2.Poland
3.Wales
4.Croatia
5.Ufaransa
6.Ujerumani
7.Italy
8.Hispania
9.England
10. Uturuki

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

Tuesday, June 21, 2016

BALE,RAMSEY NDIO VINARA WA MABAO NA ASSISTS HADI SASA EURO 2016



MSIMAMO MAKUNDI YOTE EURO 2016


Sunday, June 19, 2016

MAMBO YAZIDI KUMWENDEA KOMBO RONALDO EURO 2016




Wednesday, June 15, 2016

MSIMAMO MAKUNDI YOTE EURO 2016


MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA EURO 2016



Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

Tuesday, June 14, 2016

VIDEO: UJUMBE WA ROY HODGSON NA ROONEY KWA MASHABIKI WA UINGEREZA




Tazama Video Hii Hapa Chini
Roy Hodgon "kama meneja ni wazi kuwa nina wasiwasi kuhusu usalama na vikwazo vinavyoweza kuwekwa juu ya timu yetu ya Uingereza, tumefanya kazi ngumu sana kufika hapa na tunataka kubaki katika mashindano, hivyo ninawaomba mashabiki wetu kuachana na vurugu,tunatambua sapoti yenu katika mechi zetu, hivyo nawaombeni muepuke vurugu na na musijaribu kufanya tena, sisi pia tutajitahidi kadri tuwezavyo kuhakikisha hali hii haiendelei, tunaweza kubaki katika mashindano haya kwa njia ya Soka"

Rooney "Napenda kuwashukuru mashabiki wetu wote kwa sapoti waliyotupa katika mechi dhidi ya Urusi na sasa tuna mchezo mkubwa mbele yetu dhidi ya Wales"
Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

VIDEO:TAZAMA HALI ILIVYO MBAYA VURUGU ZA MASHABIKI HUKO UFARANSA


Tazama Video Hii Hapa Chini



DARREN RODGERS AFARIKI DUNIA HUKO UFARANSA EURO 2016

Shabiki wa Ireland ya Kaskazini Darren Rodgers 25, amefariki dunia baada ya kuanguka kutoka kwenye kingo za Beach ya Promenade des Anglais na kudondokea kwenye mwamba uliopembezoni mwa Beach hiyo huko Nice, Ufaransa.


Tukio hilo ni ajali tu na halikupangwa na mtu yeyote.
Polisi nchini Ufaransa wamewasiliana na ndugu wa marehemu ili kuwakabidhi mwili wa mpendwa wao.


Darren (Kushoto), Mwonekano wa Sehemu Alipoanguka (Kulia)

Hapa Ndipo Darren Alipoanguka

Polisi Wakiwa Eneo Darren alipoanguka
Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

Friday, June 10, 2016

VIDEO: MASHABIKI WA UINGEREZA WALIVYOANZISHA VURUGU UFARANSA

Mashabiki Wawili Wa Uingereza Wanashikiliwa Na Polisi Baada Ya Kuingia Katika Mzozo Na Baadhi Ya Vijana Wa Kifaransa.

Polisi 4 wa nchini humo wamejeruhiwa katika ghasia hizo. Inasemekana mashabiki hao wa England walioanzisha vurugu walikuwa wamelewa, lakini hakuna mali zozote zilizoharibiwa kutokana na vurugu hizo.

Thursday, June 9, 2016

CHEKI KIKOSI CHA HISPANIA KILIVYOTUA UFARANSA TAYARI KWA EURO 2016

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA HISPANIA KIKIWASILI JIJINI PARIS TAYARI KWA MICHUANO YA EURO INAYOTARAJIWA KUANZA KESHO IJUMAA JUNI 10, 2016
Cesc Fabregas (Chelsea)

De Gea (Man Utd)

Del Bosque (Kocha Timu ya Taifa ya Hispania)

Wednesday, June 1, 2016

HII NDO TOP 20 YA WACHEZAJI WAKALI WANAOENDA KUCHEZA EURO 2016

Michuano ya Euro 2016 inatarajiwa kutimua vumbi Juni 10 huko nchini Ufaransa, Hapa kuna List ya wachezaji 20 wanaoonekana kuwa tishio zaidi katika michuano hiyo.


The top 20 and stars:

1. Cristiano Ronaldo – Portugal

2. Zlatan Ibrahimovic – Sweden

3. Antoine Griezmann – France

4. Dimitri Payet – France

5. James Milner – England

6. Saul Niguez – Spain

7. Koke – Spain

8. Sergio Ramos – Spain

9. Toni Kroos – Germany

10. Juanfran – Spain

11. Marek Hamsik – Slovakia

12. Gareth Bale – Wales

13. Manuel Neuer – Germany

14. Hakan Calhanoglu – Turkey

15. Dele Alli – England

16. Paul Pogba – France

17. Mats Hummels – Germany

18. N’Golo Kante – France

19. Thiago Alcantara – Spain

20. Jordi Alba – Spain

WALIOACHWA KIKOSI CHA SPAIN MICHUANO YA EURO 2016

Hawa ndo wachezaji ambao wataikosa michuano ya Euro 2016 baada ya kocha Del Bosque kutowajumuisha katika kikosi chake kitakachokwenda Ufaransa kuwania kombe hilo.