Yanga Yainyoosha Azam Fc Chamanzi

Azam FC 1 - 2 Young Africans.

Kiungo Wa Everton James McCathy Avunjika Mguu

Kiungo James McCarthy wa Everton sasa atakaa nje na kuukosa msimu wote huh baada ya kuvunjika mifupa miwili ya mguu wake.

DRAW CAF CL And CC 2018

Draw Caf Cl and CC 2018

Yanga Yazinduka Yaambulia Ushindi Mwembamba

Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa goli moja kwa sifuri

Madrid Yaivurumisha Deportivo 7-1

Klabu ya Real Madrid leo imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono kwa jumla ya magoli 7-1 dhidi ya Klabu Deportivo la Coruna

Showing posts with label Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kimataifa. Show all posts

Wednesday, March 21, 2018

PICHA:CHANGAMSHA SIKU YAKO KISOKA

Uongo wa wachezaji; Vidal kapiga chini Mwenyewe anadai Penati!!! Lol

Kama Kweli Vile

Nadhani Hapa Mashabiki Walizuiwa kuingia Uwanjani: Jamaa Kafunga Goli Kaenda Kujishangilia Mwenyewe: Hahahahaaa

Sunday, January 21, 2018

Ronaldo, Bale, Nacho Watupia Madrid Ikiiangamiza Deportivo 7-1

Matokeo La Liga


VIDEO:Angalia James McCathy Wa Everton Alivyovunjwa Mguu

Kiungo wa Everton James McCathy amevunjika mguu katika mechi kati ya timu yake ya Everton dhidi ya West Brom katika harakati za kumzuia mchezaji wa West Brom Solomon Rondom.


Tazama video hapa chini jinsi tukio lilivyokuwa.


Tukio hilo limetokea katika mchezo huo wa ligi kuu soka nchini Uingereza ambapo mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1

Monday, June 5, 2017

Meseji Za Tiote Za Whatsapp Saa Chache Kabla Ya Kifo Chake


BAD NEWS: TIOTE AANGUKA GHAFLA NA KUPOTEZA MAISHA

kiungo wa zamani wa Newcastle, Cheick Tiote ameanguka ghafla na kupoteza maisha akiwa mazoezini katika timu yake ya Beijing Enterprises inayoshiriki ligi daraja la pili.


Kiungo huyo ambaye amewahi kuwa tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast anakutwa na umauti ikiwa ni miezi minne tu tangu ajiunge na klabu hiyo.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Ameen

Sunday, June 4, 2017

Zijue Rekodi 7 Zilizovunjwa Na Ronaldo Jana

Jina la Cristiano Ronaldo kwa sasa tayari limekwisha andikwa katika kila kitabu cha rekodi za mpira wa miguu Ulimwenguni.


Amefunga magoli mengi katika ligi kubwa Barani Ulaya kuliko mchezaji yeyote. Ni mchezaji wa kwanza na hakuna mwingine, kufikisha magoli 100 katika mashindao ya klabu bingwa barani Ulaya.

Ana rekodi pia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuingia katika kitabu cha rekodi za Dunia (The Guinness World Record) kwa kuwa mchezaji mwenye LIKES nyingi zaidi katika mtandao wa Facebook.

Hata hivyo, kwa magoli mawili aliyoyapachika katika mchezo wa fainali jana dhidi ya Juventus, Mtaliano huyo ameziweka rekodi mpya kabisa katika historia yake ya soka. 

Hapa Chini ni baadhi tu ya Rekodi ambazo kupitia mchezo wa fainali wa jana Ronaldo ameziweka.

1. Amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika fainali 3 za UEFA Champions League
Baada ya kufunga goli katika fainali ya mwaka 2008 akiwa na klabu ya Manchester United, na mkwaju aliopachika katika fainali ya mwaka jana, Ronaldo tena amefanikiwa kufunga goli la kwanza na la tatu katika fainali ya jana dhidi ya Juve.
Kabla Hujabisha: Messi amefunga katika fainali mbili tu, (2009 na 2011)

2. Amemfunika Messi kwa kuibuka Mfungaji Bora wa Klabu Bingwa Barani Ulaya msimu huu 2016/17 baada ya kuachwa nyuma kwa tofauti ya magoli 7 katik yake na Messi.

Kabla ya mechi kati ya Bayern na Madrid iliyopigwa Ujerumani April 12 mwaka huu, Ronaldo alikuwa amefunga magoli 2 tu huku Messi akiwa amekwishapachika magoli 10, hivyo kufanya tofauti kati ya Ronaldo na Messi kuwa ni magoli 7, lakini Ronaldo alifunga magoli 2 katika mechi ya kwanza dhidi ya Bayern kisha akapiga hat-trik katika mchezo wa marudiano na kumfanya afikishe magoli 7, na kupunguza gap la magoli kati yake na Mesi kutoka 7 hadi kuwa 3. Mesi aliongeza goli katika mchezo dhidi ya PSG na kufikisha magoli 11, lakini Katika mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid, CR7 alipiga hat-trik na kumfanya afikishe idadi ya magoli 10, goli moja nyuma ya Mesi.

Hata hivyo kabla ya mechi ya fainali ya jana Ronaldo alikuwa amekwisha pachika magoli 10 akizidiwa goli 1 na Messi ambaye klabu yake iliondolewa katika hatua ya Nusu fainali na Juventus.

CR7 jana alifanikiwa kuweka kambani magoli mawili na kumfanya afikishe idadi ya magoli 12 goli moja zaidi mbele ya Messi, Hivyo Ubingwa jana ulifurahiwa mara mbili na Ronaldo, kwanza alikuwa anafurahia kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo rekodi ambayo haijawahi kuwekwa na klabu yoyote tangu kuanzishwa kwa klabu bingwa Ulaya, Pili kuibuka mfungaji bora katika michuano hiyo huku akimpiku mpizani wake wa karibu Lionel Messi.

3. Amekuwa Mfungaji Bora wa UEFA Champions League Mara Nyingi zaid kuliko mchezaji mwingine yoyote.

Ronaldo na Messi kabla ya mechi ya fainali ya jana wote walikuwa sawa katika kutwaa zawadi ya ufungaji bora klabu Bingwa ulaya, wote wakichukua tuzo hiyo mara tano. Lakini baada ya kuibuka tena mfungaji bora msimu huu uliomalizika kwa fainali ya jana CR7 anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mfungaji bora mara 6.

4. Amefikisha magoli 600 katika maisha yake ya soka.

5. Amefikisha magoli 500 akiwa na klabu ya Real Madrid

Goli lake la kwanza limeifanya Real Madrid kuwa timu ya kwanza kufikisha magoli 500 katika michunao ya UEFA Champions.

6. Amekuwa Mchezaji wa 20 katika historia ya soka kushinda makombe 4 au zaidi ya Ulaya.

Ushindi wa jana Cardiff umempa taji la 3 Ronaldo katika makombe ya Ulaya akiwa na Madrid, ukiongezea na Moja aliloshinda mwaka 2008 akiwa na Manchester United. Ni wachezaji 19 tu ambao wameweza kufanikiwa kufanya hivyo na kati ya hao, wachezaji 11 wanatoka katika klabu ya Real Madrid kuanzia miaka ya 1950s.

7. Amefikia rekodi ya Raul ya kucheza mechi 144 za UEFA Champions League akiwa katika nafasi ya 4 katika list ya wachezaji wa muda wote waliocheza mechi nyingi zaidi za UEFA Champions League.

CR7 kwa sasa yuko nyuma ya Ryan Giggs aliyecheza mechi 151, Xavi mechi 157 na Iker Casillas mechi 168, katika list ya UEFA ya wachezaji wa muda wote waliocheza mechi nyingi zaidi za michuano hiyo.

Huyo Ndio Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro

Ulipitwa Na Fainali UEFA?, Hivi Ndivyo Mambo Yalivyokuwa

Saturday, June 3, 2017

Tetesi Mpya Za Usajili Liverpool

Klabu ya Liverpool imefuzu kushiriki michuano ya klabu Bingwa Barani Ulaya UEFA Champions League msimu ujao wa 2017/18. Kuelekea katika michuano hiyo na ligi kuu nchini England, klabu hiyo imeshaanza kuziwania saini za wachezaji mbalimbali kama ambavyo Soka24 inakuletea kiundani yote yanayoendelea katika klabu hiyo.


Roma wakataa Ofa ya Liverpool
Majogoo wa London Liverpool, waliweka mezani kitita cha paundi milioni 28 kuitaka saini ya Winga Mohamed Salah lakini ofa hiyo imekataliwa, kwa mujibu wa Daily Mail.
Wababe hao wa Seria A wanadai gharama ya kuipata saini ya Salah ni paundi milioni 40.

Tetesi Mpya Za Usajili Manchester United

Tetesi za usajili katika klabu ya Manchester United.


Man United Kukamilisha Uhamisho Wa Lacazette
klabu ya Manchester United ipo mbioni kuhakikisha inamsajili straika wa Lyon Alexandre Lacazette, kwa mujibu wa L'Equipe

Man United Yatupilia Mbali Ofa ya Paundi Milioni 60 ya Real Madrid Kumtaka De Gea
Manchester United imekataa ofa ya paundi milioni 60 iliyotolewa na klabu ya Real Madrid ikihitaji kupata huduma ya mlinda mlango David De Gea, kwa mujibu wa Sky Sports News

Mourinho Amfukuzia Morata Kimyakimya
Jose Mourinho amekuwa katika mawasiliano binafsi na straika wa Real Madrid Alvaro Morata, kwa mujibu wa OkDiario

Bale katika Rada ya Man U
Man U inaendelea kumfuatilia kwa ukaribu Winga wa Real Madrid Gareth Bale, kwa mujibu wa Mundo Deportivo Reports

Lindelof Kuigharimu Man Utd paundi milioni 52
Man U wameambiwa wanatakiwa kutoa kitita cha paundi milioni 52 kumnasa beki wa Benifica Victor Lindelof, kwa mujibu wa A Bola

Man Utd Yaongoza Mbio Za Kumuwania Rose
Man Utd inaongoza katika mbio za kuipata saini ya Beki wa Tottenham Danny Rose, kwa mujibu wa Daily Mirror.

Herrera Kutupilia Mbali Dili la Barcelona
Inaonekana wazi kuwa Ander Herrea atalikataa dili la Barcelona na kuendelea kusalia katika klabu ya Man U.

Lukaku katika Rada za Mourinho
Straika wa Everton Romelu Lukaku anawaniwa na klabu za Chelsea na Man United kwa mujibu wa Express.

Tetesi Mpya Za Usajili Arsenal

Ungana na Soka24, kwa habari za papo kwa papo za usajili katika klabu kubwa na pendwa zaidi duniani, hapa nimekuwekea yanayojiri katika klabu ya Arsenal hivi sasa.


Arsenal katika mbio za Kumuwania Mbappe
klabu ya Arsenal imeingia katika vita ya kuiwania saini ya nyota wa Monaco Kylian Mbappe, kwa mujibu wa L'Equipe

Juve Yamtolea Macho Szczesny
Wojchiech Szczesny anaweza kuendelea kubaki katika ligi ya Italia Serie A baada ya Juve kutenga kitita cha paundi milioni 14 kwa mlinda mlango huyo wa Arsenal aliyepo kwa mkopo, kwa mujibu wa Daily Mail.

Wenger Aonywa kuhusu Usajili
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger huenda akaonywa aache kusitasita katika kufanya usajili kuelekea kikao cha bodi cha klabu hiyo, kwa mujibu wa Daily Mail.

Wenger Aahidiwa Paundi Milion 100
Arsene Wenger atakabidhiwa kitita cha paundi milioni 100 azitumie katika kuimarisha kikosi chake kwenye kipindi hiki cha usajili endapo atasaini mkataba mpya, kwa mujibu wa Daily Star.

Arsenal Yaongoza Mbio za kumuwania Belotti.
klabu ya Arsenal imeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya Andrea Belotti akitokea Torino, kwa mujibu wa The Sun.

Arsenal Yampa Ofa Nono Sanchez
klabu ya Arsenal imempa ofa ya mkataba mpya nyota wake Alexis Sanchez wenye thamani ya paundi 270,000 kwa wiki endapo atakuwa tayari kubaki klabuni hapo, huku Bayern Munich ikiwa imeshaonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo, kwa mujibu wa Daily Mail.

Friday, June 2, 2017

PSG Wakubali Yaishe Kwa Aubameyang

Vigogo wa soka nchini Ufaransa, PSG wamekubali kutoa paundi milioni 61 kuinasa saini ya mshambuliaji wa Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang.


Licha ya gharama hizo za uhamisho PSG pia wamekubali kumlipa nyota huyo kutoka barani Afrika kitita cha paundi 168,000 kwa wiki.


Usipitwe na taarifa yoyote ya Kimichezo hususani kipindi hiki cha Usajili, Ungana na Soka24 muda wote kuwa wa kwanza kupata habari za papo kwa papo za Usajili na mengineyo yote ya kimichezo kote ulimwenguni.

Ozil, Sanchez Washusha Presha Ya Mashabiki Arsenal

Washambuliaji machachari wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil na Alexis Sanchez wameshusha presha ya mashabiki wengi wa Arsenal baada ya uvumi kuenea kuwa nyota hao wataihama klabu hiyo.


Taarifa za hivi punde zinadai kuwa wachezaji hao wapo tayari kubaki klabuni hapo lakini wanataka wapewe nyongeza ya paundi 350,000 katika mishahara yao.

Griezmann Kubaki Atletico Madrid

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amedokeza kwamba huenda asiihame klabu yake, licha ya kuwindwa na klabu  kubwa Ulaya ikiwemo Manchester United.


Mfaransa huyo wa miaka 26 aliandika kwenye Twitter: "Sasa zaidi ya zamani! #atleti #alltogether (sote pamoja)."

Alisema hayo saa chache baada ya marufuku ya kuzuia klabu hiyo kununua wachezaji kudumishwa.

Hii ina maana kwamba huenda klabu hiyo isiweze kumnunua mchezaji mwingine iwapo itamuuza.

Mnamo Alhamisi, ilibainika kwamba Manchester United nao pia wanaonekana kupunguza hamu ya kutaka kumnunua.

Kwa kuwa Atletico haiwezi kununua wachezaji wengine hadi Januari, inatarajiwa kwamba Griezmann atapewa mkataba mpya.

United walitaka sana kumnunua mshambuliaji huyo na walikuwa wanatafakari uwezekano wa kufikisha euro 100m (£87m) kumfungua kutoka kwa mkataba wake.

Lakini duru zinasema ununuzi wa Griezmann sasa si kipaumbele kwa United.
Hata hivyo endapo dili la Griezmann litashindwa kutimia bado wapo wachezaji wengine ambao United inawafukuzia akiwemo Romelu Lukaku wa Everton, Andrea Belotti wa Torino na Alvaro Morata wa Real Madrid.

FA Yailipa Chelsea Paundi Milioni 150.8

Chama cha soka nchini Uingereza FA, kimeilipa klabu ya Chelsea kitita cha paundi milioni 150.8 ikiwa ni baada ya kushinda ubingwa ligi kuu nchini humo kwa msimu wa 2016/17.


Kutokana na mkataba wa matangazo ya televisheni, msimu wa 2016-17 kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la fedha ukitoa takriban Paundi bilioni 2.4 kwa timu 20 zaidi ya msimu uliopita zilipolipwa Paundi bilioni 1.6.

Klabu ya Sunderland nayo licha ya kushuka daraja imepata kitita cha paundi milioni 93.471, fedha hizo zikitokana na matangazo ya Televisheni, mikataba ya kibiashara pamoja na zawadi.

Ianze Siku Yako Kwa Kucheka Na Hivi Vituko Vya Uwanjani

Mchezo wa soka ni moja kati ya michezo inayopendwa zaidi ulimwenguni, umejikusanyia mashabiki na wafuatiliaji wengi zaidi kuliko michezo mingine yote.


Hata hivyo ndani ya uwanja yapo mengi ya kushangaza yanayotokea na kukuacha mdomo wazi. Tazama hapa chini video ya matukio ya kustaajabisha yakijiri uwanjani.


Ulipitwa na Hii: List Ya Wanamichezo Maarufu Zaidi Duniani 2017

Ushawahi kujiuliza kuwa ni mwanamichezo gani maarufu zaidi duniani kwa sasa?? na Ukakosa majibu au hukuwa na uhakika wa majibu uliyoyapata??


Ben Alamar, Mkurugenzi wa uchambuzi wa ESPN ametuletea orodha ya wanamichezo wanaopendwa na maarufu zaidi duniani baada ya kuchukua takwimu mbalimbali zilizohusisha mitandao ya kijamii na kupata idadi ya wanamichezo 100 wenye umaarufu zaidi kwa sasa.

Hii Hapa List Ya Klabu Tajiri Zaidi Duniani 2017/18

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Forbes kuhusu klabu zinazoingiza pesa nyingi zaidi duniani, klabu ya Manchester United inayonolewa na Kocha Mreno Jose Mourinho imeibuka namba moja ikizipiku klabu za Real Madrid na Barcelona.


List Kamili hii hapa Chini;

1. Manchester United – $2.235bn (£1.396bn)

2. Real Madrid – $1.877bn (£1.17bn)

3. Barcelona – $1.307bn (£816m)

4. Arsenal – $1.292bn (£807m)

5. Bayern Munich – $1.235bn (£770m)

6. AC Milan – $989m (£615m)

7. Chelsea – $761m (£473m)

8. Liverpool – $619m (£385m)

9. Juventus – $591m (£367m)

10. Schalke 04 – $587m (£365m)

11. Tottenham Hotspur –$564m (£351m)

13. Manchester City – $443m (£275m)

Thursday, June 1, 2017

UEFA Yapitisha Sheria Mpya Kuelekea Fainali Juve & Real Madrid

Kwa lengo la kulinda utimamu wa wachezaji shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya UEFA imepitisha sheria mpya ambayo itaziwezesha timu kufanya mabadiliko (substitution) mara nne badala ya mara tatu ambayo ilikuwepo awali endapo tu mechi itaenda hatua ya dakika 30 za nyongeza.


Kwa sasa timu inaruhusiwa kufanya mabadiliko (Sub) kwa wachezaji watatu tu bila kujali ni kwa muda gani mechi itachezwa kwa maana iwe ni dakika 90 za kawaida au dakika 120, lakini kwa sheria hii mpya ni kwamba makocha hawatakuwa tena na hofu ya kufanya mabadiliko wakihofia kumaliza mapema idadi ya wachezaji inayoruhusiwa ikiwa matokeo yatakuwa ni ya sare kwa muda wa kawaida wa dakika tisini.

Sheria hii itaanza kufanya kazi katika mchezo wa fainali kati ya Juventus dhidi ya Real Madrid itakayopigwa jijini Cardiff huko nchini Wales Juni 2 mwaka huu.

USAJILI: Yaya Toure Kimeeleweka Man City

Kiungo wa klabu ya Manchester City, raia wa Ivory Coast Yaya Toure amesaini mkataba mpya utakaoendelea kumuweka mchezaji huyo klabuni hapo kwa mwaka mmoja zaidi. 


Hatua hiyo inafikiwa baada ya Pep Guardiola kuridhika na kiwango cha mchezaji huyo achilia mbali tofauti waliwahi kuwa nazo mwanzoni kabisa mwa msimu. 

Kiungo huyo 34, ambaye mkataba wake wa zamani umemalizika mwezi huu, alianza msimu uliomalizika kwa kuingia katika mtafaruku na kocha Guardiola hali iliyopelekea hadi kuondolewa katika kikosi cha Manchester City kilichoshiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya, na hatimaye Guardiola kusema kama Toure angependa kuendelea kuwepo kikosini basi alitakiwa kumuomba yeye msamaha, hali hiyo iliendelea ya Toure kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha City hadi pale ambapo Toure aliamua kuweka tofauti zake pembeni na kuomba msamaha na hatimaye kurudishwa kikosini na leo anaongezewa tena muda wa kuendelea kuitumikia City.

"Toure amekuwa mchezaji mzuri sana katika kikosi cha City na ameendelea kuwa na mchango muhimu sana katika kikosi cha Guardiola" alisema mkurugenzi wa klabu hiyo Tixiki Begiristain akiiambia Mancity.com

Kwa taarifa za papo kwa papo za Usajili na yote yanayohusu Soka, Ni hapahapa Soka24

Atletico Madrid Yaangukia Pua Tena Usajili

Klabu ya Atletico Madrid imeshindwa katika rufani yao waliyokata katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kupinga adhabu ya kuzuiwa kusajili na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.


Hatua hiyo sasa inamaanisha kuwa klabu hiyo haitaruhusiwa kusajili mpaka itakapofika usajili wa dirisha doko Januari mwaka 2018.

Atletico walifungiwa kusajili kwa vipindi viwili vya usajili kwa kosa la kukiuka sheria ya usajili wachezaji wa kigeni wenye umri wa chini ya miaka 18.

Baada ya kushindwa rufani yao FIFA, Atletico walitumikia adhabu ya kutosajili katika dirisha la Januari mwaka huu kabla ya kuamua kukata rufani CAS. Kutokana na matokeo ya rufani yao Atletico sasa watakuwa. wameshindwa kufanya usajili wowote kwa mwaka huu.