Showing posts with label Usajili. Show all posts
Showing posts with label Usajili. Show all posts
Wednesday, June 14, 2017
Saturday, June 3, 2017
Yote Yanayoihusu Azam FC;Usajili, Waliotemwa Wanaoingia Na Mipango Msimu Ujao
UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuwataarifu wapenzi na mashabiki wa soka nchini kuwa imebadilisha mfumo wa usajili uliokuwa ikiutumia awali wa kusajili wachezaji kwa gharama kubwa na sasa ikijikita kwenye kufanya matumizi ya wastani pamoja na kuwatumia ipasavyo nyota watakaozalishwa kutoka kituo chao ‘Azam Academy’.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd, leo imeeleza kuwa kuelekea msimu ujao na kuendelea, Azam FC itaweka msisitizo na kufanya uwekezaji ipasavyo kwenye kituo chake cha kukuza vipaji ‘Azam Academy’ ili kuvuna wachezaji bora watakaopandishwa katika kikosi cha timu kubwa.
Kwa kuanzia katika kutekeleza malengo hayo, kuelekea msimu ujao Azam FC imewapandisha wachezaji sita kutoka kwenye kituo chake, ambao ni mabeki Abbas Kapombe, Abdul Haji, Godfrey Elias, kiraka Ramadhan Mohamed, kiungo Stanslaus Ladislaus na mshambuliaji Yahaya Zaid, aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Daraja Kwanza (FDL) msimu uliopita kwa mabao tisa aliyofunga alipokuwa kwa mkopo Ashanti United.
Azam FC imekuwa na utaratibu mzuri wa kulea wachezaji wake vijana kwa kuwapandisha kwenye timu kubwa, ambao wamekuwa wakifanya vizuri na kuibeba timu, ambapo wengine waliopo katika kikosi cha wakubwa ni makipa Aishi Manula, Metacha Mnata, mabeki Gadiel Michael, Ismail Gambo, kiungo Mudathir Yahya, Abdallah Masoud, Himid Mao, Joseph Mahundi na mshambuliaji Shaaban Idd.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, aliyeongezewa mkataba wa mwaka mmoja, anaamini ya kuwa wachezaji hao vijana watazidi kukiimarisha kikosi chake kwa kushirikiana na wachezaji wazoefu waliopo kikosini, hadi anafikia uamuzi huo wa kuwapandisha aliwafuatilia katika mechi mbalimbali za timu ya vijana ikiwemo na baadhi ya siku kuwajumuisha katika mazoezi ya timu kubwa.
Aidha kuhusiana na wachezaji waliomaliza mikataba yao, Azam FC imethibitisha rasmi kuachana na winga wake Khamis Mcha ‘Vialli’ na Ame Ally, aliyekuwa kwa mkopo Kagera Sugar, wote mikataba yao ikiwa imemalizika.
Mabadiliko kwenye mfumo wa uongozi
Katika hatua nyingine, Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC imefanya mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi ya timu hiyo kwa kukifuta cheo cha Ofisa Mtendaji Mkuu, na sasa cheo cha juu kitakuwa ni Meneja Mkuu, nafasi inayoshikiliwa na Abdul Mohamed.
Kutokana na mabadiliko hayo ya kiutendaji, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, amemaliza mkataba wake na pande zote mbili zimekubaliana kuachana, na sasa majumuku yake yote yatafanywa na Abdul Mohammed, akiwa ndio Meneja Mkuu wa klabu.
Chanzo: Azam FC Official Site
Tetesi Mpya Za Usajili Liverpool
Klabu ya Liverpool imefuzu kushiriki michuano ya klabu Bingwa Barani Ulaya UEFA Champions League msimu ujao wa 2017/18. Kuelekea katika michuano hiyo na ligi kuu nchini England, klabu hiyo imeshaanza kuziwania saini za wachezaji mbalimbali kama ambavyo Soka24 inakuletea kiundani yote yanayoendelea katika klabu hiyo.
Roma wakataa Ofa ya Liverpool
Majogoo wa London Liverpool, waliweka mezani kitita cha paundi milioni 28 kuitaka saini ya Winga Mohamed Salah lakini ofa hiyo imekataliwa, kwa mujibu wa Daily Mail.
Wababe hao wa Seria A wanadai gharama ya kuipata saini ya Salah ni paundi milioni 40.
Tetesi Mpya Za Usajili Manchester United
Tetesi za usajili katika klabu ya Manchester United.
klabu ya Manchester United ipo mbioni kuhakikisha inamsajili straika wa Lyon Alexandre Lacazette, kwa mujibu wa L'Equipe
Man United Yatupilia Mbali Ofa ya Paundi Milioni 60 ya Real Madrid Kumtaka De Gea
Manchester United imekataa ofa ya paundi milioni 60 iliyotolewa na klabu ya Real Madrid ikihitaji kupata huduma ya mlinda mlango David De Gea, kwa mujibu wa Sky Sports News
Mourinho Amfukuzia Morata Kimyakimya
Jose Mourinho amekuwa katika mawasiliano binafsi na straika wa Real Madrid Alvaro Morata, kwa mujibu wa OkDiario
Bale katika Rada ya Man U
Man U inaendelea kumfuatilia kwa ukaribu Winga wa Real Madrid Gareth Bale, kwa mujibu wa Mundo Deportivo Reports
Lindelof Kuigharimu Man Utd paundi milioni 52
Man U wameambiwa wanatakiwa kutoa kitita cha paundi milioni 52 kumnasa beki wa Benifica Victor Lindelof, kwa mujibu wa A Bola
Man Utd Yaongoza Mbio Za Kumuwania Rose
Man Utd inaongoza katika mbio za kuipata saini ya Beki wa Tottenham Danny Rose, kwa mujibu wa Daily Mirror.
Herrera Kutupilia Mbali Dili la Barcelona
Inaonekana wazi kuwa Ander Herrea atalikataa dili la Barcelona na kuendelea kusalia katika klabu ya Man U.
Lukaku katika Rada za Mourinho
Straika wa Everton Romelu Lukaku anawaniwa na klabu za Chelsea na Man United kwa mujibu wa Express.
Tetesi Mpya Za Usajili Arsenal
Ungana na Soka24, kwa habari za papo kwa papo za usajili katika klabu kubwa na pendwa zaidi duniani, hapa nimekuwekea yanayojiri katika klabu ya Arsenal hivi sasa.
Arsenal katika mbio za Kumuwania Mbappe
klabu ya Arsenal imeingia katika vita ya kuiwania saini ya nyota wa Monaco Kylian Mbappe, kwa mujibu wa L'Equipe
Juve Yamtolea Macho Szczesny
Wojchiech Szczesny anaweza kuendelea kubaki katika ligi ya Italia Serie A baada ya Juve kutenga kitita cha paundi milioni 14 kwa mlinda mlango huyo wa Arsenal aliyepo kwa mkopo, kwa mujibu wa Daily Mail.
Wenger Aonywa kuhusu Usajili
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger huenda akaonywa aache kusitasita katika kufanya usajili kuelekea kikao cha bodi cha klabu hiyo, kwa mujibu wa Daily Mail.
Wenger Aahidiwa Paundi Milion 100
Arsene Wenger atakabidhiwa kitita cha paundi milioni 100 azitumie katika kuimarisha kikosi chake kwenye kipindi hiki cha usajili endapo atasaini mkataba mpya, kwa mujibu wa Daily Star.
Arsenal Yaongoza Mbio za kumuwania Belotti.
klabu ya Arsenal imeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya Andrea Belotti akitokea Torino, kwa mujibu wa The Sun.
Arsenal Yampa Ofa Nono Sanchez
klabu ya Arsenal imempa ofa ya mkataba mpya nyota wake Alexis Sanchez wenye thamani ya paundi 270,000 kwa wiki endapo atakuwa tayari kubaki klabuni hapo, huku Bayern Munich ikiwa imeshaonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo, kwa mujibu wa Daily Mail.
Friday, June 2, 2017
PSG Wakubali Yaishe Kwa Aubameyang
Vigogo wa soka nchini Ufaransa, PSG wamekubali kutoa paundi milioni 61 kuinasa saini ya mshambuliaji wa Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang.
Licha ya gharama hizo za uhamisho PSG pia wamekubali kumlipa nyota huyo kutoka barani Afrika kitita cha paundi 168,000 kwa wiki.
Usipitwe na taarifa yoyote ya Kimichezo hususani kipindi hiki cha Usajili, Ungana na Soka24 muda wote kuwa wa kwanza kupata habari za papo kwa papo za Usajili na mengineyo yote ya kimichezo kote ulimwenguni.
Ozil, Sanchez Washusha Presha Ya Mashabiki Arsenal
Washambuliaji machachari wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil na Alexis Sanchez wameshusha presha ya mashabiki wengi wa Arsenal baada ya uvumi kuenea kuwa nyota hao wataihama klabu hiyo.
Taarifa za hivi punde zinadai kuwa wachezaji hao wapo tayari kubaki klabuni hapo lakini wanataka wapewe nyongeza ya paundi 350,000 katika mishahara yao.
Simba Wapata Mbadala Wa Juuko Murshid
Munezero Fiston ni Mnyarwanda ambaye yupo katika mipango ya Simba baada ya kocha Joseph Omog kupendekeza atafutiwe mchezaji mwingine.
Munezero, anayekipiga katika klabu ya Rayon Sport anatarajiwa kutua Dar Es Salaam Jumamosi hii kwa lengo la kufanya mazungumzo na wekundu hao wa Msimbazi.
Hatua hii inakuja baada ya taarifa za kuomba kuondoka kwa beki Juuko Murshid pamoja na hali ya majeraha inayomsumbua Method mwanjali hivyo kuonekana kuna kila sababu ya kupata mbadala wa nyota hao.
“Munezero atawasili rasmi Jumamosi hii. Tunaweza kumtumia kwenye michuano ya Super Cup, mashabiki wetu watapata nafasi ya kumuona hapo,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
Pamoja na beki huyo, Simba ina mpango wa kusajili wachezaji wengine watatu, ambao ni kiungo, mshambuliaji na beki mwingine kujenga ukuta imara kwenye kikosi hicho.
Griezmann Kubaki Atletico Madrid
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amedokeza kwamba huenda asiihame klabu yake, licha ya kuwindwa na klabu kubwa Ulaya ikiwemo Manchester United.
Mfaransa huyo wa miaka 26 aliandika kwenye Twitter: "Sasa zaidi ya zamani! #atleti #alltogether (sote pamoja)."
Alisema hayo saa chache baada ya marufuku ya kuzuia klabu hiyo kununua wachezaji kudumishwa.
Hii ina maana kwamba huenda klabu hiyo isiweze kumnunua mchezaji mwingine iwapo itamuuza.
Mnamo Alhamisi, ilibainika kwamba Manchester United nao pia wanaonekana kupunguza hamu ya kutaka kumnunua.
Kwa kuwa Atletico haiwezi kununua wachezaji wengine hadi Januari, inatarajiwa kwamba Griezmann atapewa mkataba mpya.
United walitaka sana kumnunua mshambuliaji huyo na walikuwa wanatafakari uwezekano wa kufikisha euro 100m (£87m) kumfungua kutoka kwa mkataba wake.
Lakini duru zinasema ununuzi wa Griezmann sasa si kipaumbele kwa United.
Hata hivyo endapo dili la Griezmann litashindwa kutimia bado wapo wachezaji wengine ambao United inawafukuzia akiwemo Romelu Lukaku wa Everton, Andrea Belotti wa Torino na Alvaro Morata wa Real Madrid.
Thursday, June 1, 2017
USAJILI: Yaya Toure Kimeeleweka Man City
Kiungo wa klabu ya Manchester City, raia wa Ivory Coast Yaya Toure amesaini mkataba mpya utakaoendelea kumuweka mchezaji huyo klabuni hapo kwa mwaka mmoja zaidi.
Hatua hiyo inafikiwa baada ya Pep Guardiola kuridhika na kiwango cha mchezaji huyo achilia mbali tofauti waliwahi kuwa nazo mwanzoni kabisa mwa msimu.
Kiungo huyo 34, ambaye mkataba wake wa zamani umemalizika mwezi huu, alianza msimu uliomalizika kwa kuingia katika mtafaruku na kocha Guardiola hali iliyopelekea hadi kuondolewa katika kikosi cha Manchester City kilichoshiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya, na hatimaye Guardiola kusema kama Toure angependa kuendelea kuwepo kikosini basi alitakiwa kumuomba yeye msamaha, hali hiyo iliendelea ya Toure kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha City hadi pale ambapo Toure aliamua kuweka tofauti zake pembeni na kuomba msamaha na hatimaye kurudishwa kikosini na leo anaongezewa tena muda wa kuendelea kuitumikia City.
"Toure amekuwa mchezaji mzuri sana katika kikosi cha City na ameendelea kuwa na mchango muhimu sana katika kikosi cha Guardiola" alisema mkurugenzi wa klabu hiyo Tixiki Begiristain akiiambia Mancity.com
Kwa taarifa za papo kwa papo za Usajili na yote yanayohusu Soka, Ni hapahapa Soka24
Atletico Madrid Yaangukia Pua Tena Usajili
Klabu ya Atletico Madrid imeshindwa katika rufani yao waliyokata katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kupinga adhabu ya kuzuiwa kusajili na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA.
Hatua hiyo sasa inamaanisha kuwa klabu hiyo haitaruhusiwa kusajili mpaka itakapofika usajili wa dirisha doko Januari mwaka 2018.
Atletico walifungiwa kusajili kwa vipindi viwili vya usajili kwa kosa la kukiuka sheria ya usajili wachezaji wa kigeni wenye umri wa chini ya miaka 18.
Baada ya kushindwa rufani yao FIFA, Atletico walitumikia adhabu ya kutosajili katika dirisha la Januari mwaka huu kabla ya kuamua kukata rufani CAS. Kutokana na matokeo ya rufani yao Atletico sasa watakuwa. wameshindwa kufanya usajili wowote kwa mwaka huu.
Asante Kwasi Kujiunga Na Yanga SC
Beki wa timu ya Mbao FC, Asante Kwasi amesema angetamani kuichezea Yanga katika msimu ujao wa ligi.
Beki huyo wa kati wa Mbao ameyasema hayo kutokana na kuvutiwa na kiwango na mafanikio ya klabu ya Yanga mabingwa mara tatu mfululizo wa ligi soka Tanzania Bara.
Kwasi kwa sasa amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliokuwa nao katika klabu yake ya Mbao FC na ameweka wazi kuwa anapenda kujiunga na timu nyingine kubwa kama Yanga au Azam FC. Mghana huyo amedai kwa kipindi ambacho ameishi nchini amegundua kuwa Yanga ndiyo klabu yenye mafanikio hivyo kumfanya yeye kuvutiwa kucheza katika klabu hiyo.
“Yanga nimeambiwa ndiyo timu inayoongoza kwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu, mara nyingi lakini pia ndiyo timu ambayo imeshiriki mara nyingi michuano ya kimataifa ukweli nimevutiwa na hilo na siku zote natamani kucheza timu yenye mafanikio kwasababu naamini ndiyo njia nyepesi ya kufika ninapopataka,”amesema Kwasi.
Beki huyo aliyeonyesha uwezo mkubwa katika msimu wa ligi uliomalizika amedai kuwa mpaka sasa bado hajajua ni timu gani ataichezea msimu ujao lakini angefurahi sana kama angetua Jangwani.
Usipitwe na habari za papo kwa papo za Usajili, Ungana na Soka24 kupata kila kinachojiri katika ulimwengu wa Soka Ulimwenguni.
Man City Yaweka Rekodi Ya Dunia Kwa Usajili Huu
Klabu ya Manchester City imefikia makubaliano ya kumsajili mlinda mlango Ederson Moraes kutoka katika klabu ya Benfica ya nchini Ureno kwa kitita cha paundi milioni 35.
Uhamisho wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 wa thamani hiyo ya fedha unamfanya Ederson kuwa kipa ghali zaidi kuwahi kusajiliwa kwa thamani hiyo ya pesa katika historia ya mpira wa miguu baada ya Gianliugi Buffon aliposajiliwa na Juventus akitokea Parma mnamo mwaka 2001.
Ederson alisafiri kwenda Manchester Jumatatu na Jumanne alitua katika uwanja wa mazoezi wa City kukamilisha vipimo vya afya na kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya klabu.
City sasa wanakuwa wameshatumia kitita cha paundi milioni 78, baada ya klabu hiyo kumsajili kumnasa kiungo Bernardo Silva kwa kitita cha paundi milioni 43 kutoka Monaco.
Historia yake kwa ufupi;
TAARIFA ZA USAJILI: Barani Ulaya
Mancini Atua Zenit
Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amekabidhiwa rasmi mikoba ya kuinoa klabu ya Zenit ya nchini Urusi. Mancini anachukua nafasi ya Mircea Lucescu.
Rasmi: Huntelaar arudi Ajax
Mshambuliaji huyo anarudi katika klabu yake ya zamani ya Ajax huku akisaini dili la mwaka mmoja baada ya kuachana na Bundesliga alikokuwa anakipiga na klabu ya Schalke 04
Tetesi: Real Madrid yatenga pauni milioni 100 kuinasa saini ya Eden Hazard
Tetesi: Kruse ni miongoni mwa wanaowindwa na klabu ya Man United kwa muda na safari hii imedhamiria kuinasa saini ya straika huyo anayeitumikia klabu ya Werder Bremen.
Rasmi: Man City yakamilisha dili la pauni milioni 35 kumnasa Mlinda mlango wa Brazil Ederson
Rasmi: Villareal wakamilisha usajili wa Unal akitokea Man City kwa mkataba wa miaka mitano.
Ungana na Soka24 kwa habari za papo kwa papo za usajili kote ulimwenguni
Friday, December 16, 2016
VIKOSI SIMBA, YANGA BAADA YA USAJILI DIRISHA DOGO
Dirisha Dogo la Usajili limefungwa rasmi jana Alhamisi Disemba 15 majira ya Saa 6:00 usiku.
Soka24 imefanikiwa kuvinasa vikosi vya miamba ya soka Tanzania Bara, Yanga na Simba baada ya kufungwa kwa dirisha hilo la usajili hapo jana.
Hivi hapa vikosi vya timu za Yanga na Simba
YANGA SC:
Makipa
-Ali Mustafa
- Deogratius Munishi
- Beno Kakolanya
Walinzi
- Nadir Haroub
- Vicent Andrew
- Vicent Bossou
- Pato Ngonyani
- Mwinyi Haji
- Juma Abdul
- Hassani Kessy
- Oscar Joseph
- Kelvin Yondani
Viungo
- Saidi Juma
- Saimoni Msuva
- Yusuph Mhilu
- Haruna Niyonzima
- Thabani Kamusoko
- Juma Mahadhi
- Deusi Kaseke
-Justin Zullu
- Geofrey Mwashuiya
Washambuliaji
- Donald Ngoma
- Obrey Chirwa
- Mateo Anthony
- Malimi Busungu
- Amisi Tambwe
- Emanuel Martin
° BENCHI LA UFUNDI.
Kocha Mkuu.
George Lwandamina
Msaidizi Maalum.
Noel Mwandila.
Kocha Msaidizi.
Juma Mwambusi.
SIMBA SC:
MAKIPA
Daniel Agyei
Dennis Richard
Peter Manyika
MABEKI
Mohamed Hussein
Abdi Banda
Hamad Juma
Janvier Bokungu
Method Mwanjali
Juuko Murshid
Novatus Lufunga
Vicent Costa
VIUNGO
Said Ndemla
Muzammil Yassin
Jonas Mkude
James Kotei
Mohamed Ibrahim
Mwinyi Kazimoto
MAWINGA
Shiza Kichuya
Jamal Mnyate
Hija Ugando
WASHAMBULIAJI
Ibrahim Ajibu
Juma Luizo
Frederic Blagnon
Laudit Mavugo
Pastory Athanas
Moses Kitandu
MAKOCHA
Joseph Omog
Jakson Mayanja
Idd Salim Abdul
MENEJA
Mussa H. Mgosi
Soka24 imefanikiwa kuvinasa vikosi vya miamba ya soka Tanzania Bara, Yanga na Simba baada ya kufungwa kwa dirisha hilo la usajili hapo jana.
Hivi hapa vikosi vya timu za Yanga na Simba
YANGA SC:
Makipa
-Ali Mustafa
- Deogratius Munishi
- Beno Kakolanya
Walinzi
- Nadir Haroub
- Vicent Andrew
- Vicent Bossou
- Pato Ngonyani
- Mwinyi Haji
- Juma Abdul
- Hassani Kessy
- Oscar Joseph
- Kelvin Yondani
Viungo
- Saidi Juma
- Saimoni Msuva
- Yusuph Mhilu
- Haruna Niyonzima
- Thabani Kamusoko
- Juma Mahadhi
- Deusi Kaseke
-Justin Zullu
- Geofrey Mwashuiya
Washambuliaji
- Donald Ngoma
- Obrey Chirwa
- Mateo Anthony
- Malimi Busungu
- Amisi Tambwe
- Emanuel Martin
° BENCHI LA UFUNDI.
Kocha Mkuu.
George Lwandamina
Msaidizi Maalum.
Noel Mwandila.
Kocha Msaidizi.
Juma Mwambusi.
SIMBA SC:
MAKIPA
Daniel Agyei
Dennis Richard
Peter Manyika
MABEKI
Mohamed Hussein
Abdi Banda
Hamad Juma
Janvier Bokungu
Method Mwanjali
Juuko Murshid
Novatus Lufunga
Vicent Costa
VIUNGO
Said Ndemla
Muzammil Yassin
Jonas Mkude
James Kotei
Mohamed Ibrahim
Mwinyi Kazimoto
MAWINGA
Shiza Kichuya
Jamal Mnyate
Hija Ugando
WASHAMBULIAJI
Ibrahim Ajibu
Juma Luizo
Frederic Blagnon
Laudit Mavugo
Pastory Athanas
Moses Kitandu
MAKOCHA
Joseph Omog
Jakson Mayanja
Idd Salim Abdul
MENEJA
Mussa H. Mgosi
Wednesday, August 31, 2016
Rasmi:Samir Nasri Atua Sevilla
Manchester City imetangaza kuwa Samir Nasri amejiunga na klabu ya Sevilla kwa Mkopo.
Endelea Kuungana Na Soka24 kwa habari za papo kwa papo za Soka kote Ulimwenguni.............
==================
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
Rasmi:Arsenal Yakamilisha Usajili wa Mustafi
Rasmi: Torino Yamnasa Joe Hart
Rasmi:Wilfred Bony Atua Stoke City
Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Endelea Kuungana Na Soka24 kwa habari za papo kwa papo za Soka kote Ulimwenguni.............
==================
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
Rasmi:Arsenal Yakamilisha Usajili wa Mustafi
Rasmi: Torino Yamnasa Joe Hart
Rasmi:Wilfred Bony Atua Stoke City
Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Rasmi: Torino Yamnasa Joe Hart
Mlinda Mlango namba moja wa Uingereza Joe Hart amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Klabu ya Torino inayoshiriki ligi kuu nchini Italia kwa mkopo akitokea Manchester City.
Hart alijikuta akiwa chaguo la pili la kocha Pep Guardiola katika nafasi hiyo ya golikipa huku Willy Cabellero akionekana kuchukua nafasi yake.
Kuwasili kwa aliyekuwa mlinda mlango wa Barcelona Claudio Bravo pia kumezika matumaini ya Joe Hart kuendelea kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, hivyo kuamua kutimkia zake Torino ambako amekwanda kwa mkopo wa mwaka mmoja.
==================
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Hart alijikuta akiwa chaguo la pili la kocha Pep Guardiola katika nafasi hiyo ya golikipa huku Willy Cabellero akionekana kuchukua nafasi yake.
Kuwasili kwa aliyekuwa mlinda mlango wa Barcelona Claudio Bravo pia kumezika matumaini ya Joe Hart kuendelea kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, hivyo kuamua kutimkia zake Torino ambako amekwanda kwa mkopo wa mwaka mmoja.
==================
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Rasmi: Wilfred Bony Atua Stoke City
Klabu ya Stoke City imekamilisha uhamisho wa Wilfred Bony kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester City.
Bony aliyefeli kumshawishi kocha mpya wa City, Mhispania Pep Guardiola amefanikiwa kufunga magoli 11 katika michezo 46 aliyocheza akiwa na Manchester City.
Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Bony aliyefeli kumshawishi kocha mpya wa City, Mhispania Pep Guardiola amefanikiwa kufunga magoli 11 katika michezo 46 aliyocheza akiwa na Manchester City.
=====================
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi
Klabu ya Arsenal imetangaza rasmi kumsajili beki wa kati wa Valencia Shkodran Mustafi kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi.
Licha ya thamani ya uhamisho wa mchezaji huyo kutowekwa wazi lakini habari za chini chini zinasema mchezaji huyo ameigharimu Arsenal kiasi cha pauni milioni 41.
Alipohojiwa baada ya kukamilisha usajili huo kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger alisema Mustafi ni mchezaji mzuri, yupo katika umri sahihi pia utakaomuwezesha kucheza soka kwa muda mrefu.
“Yupo katika umri sahihi. Ana uzoefu mkubwa,” Wenger aliiambia tovuti ya Arsenal. “Ni mchezaji ambaye anajua nini anapaswa kufanya na kwa wakati gani anayejua kuchezea mpira pia.”
“Tumepata mchezaji mzuri sana lakini mwenye matarajio ya muda mrefu.”
Awali Mustafi aliwahi kuichezea klabu ya Everton japo hakupata nafasi sana ya kucheza na hii inakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo kucheza ligi kuu nchini Uingereza.
===============
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
Rasmi:Wilfred Bony Atua Stoke City
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Licha ya thamani ya uhamisho wa mchezaji huyo kutowekwa wazi lakini habari za chini chini zinasema mchezaji huyo ameigharimu Arsenal kiasi cha pauni milioni 41.
Alipohojiwa baada ya kukamilisha usajili huo kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger alisema Mustafi ni mchezaji mzuri, yupo katika umri sahihi pia utakaomuwezesha kucheza soka kwa muda mrefu.
“Yupo katika umri sahihi. Ana uzoefu mkubwa,” Wenger aliiambia tovuti ya Arsenal. “Ni mchezaji ambaye anajua nini anapaswa kufanya na kwa wakati gani anayejua kuchezea mpira pia.”
“Tumepata mchezaji mzuri sana lakini mwenye matarajio ya muda mrefu.”
Awali Mustafi aliwahi kuichezea klabu ya Everton japo hakupata nafasi sana ya kucheza na hii inakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo kucheza ligi kuu nchini Uingereza.
===============
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
Rasmi:Wilfred Bony Atua Stoke City
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Tuesday, August 30, 2016
AUBAMEYANG AITAMANI REAL MADRID
Hakuna ubishi kuwa Nyota wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang anatamani kujiunga na miamba ya soka ya nchini Hispania klabu ya Real Madrid.
Aubameyang amewahi kumuahidi babu yake kuwa ipo siku atakuja kucheza katika klabu ya Real Madrid na hayo matumaini yake yanakaribia kutimia.
Mazungumzo ya uhamisho wa Supasta huyo raia wa Gabon kujiunga na Los Blancos yamekuwa yakitawala sana tangu kuisha kwa msimu wa ligi mwaka 2015/16,lakini siku za hivi karibuni Aubameyang ameifungukia klabu yake ya Dortmund kuwa Moyo wake unatamani kujiunga na Real Madrid.
Licha ya kwamba Madrid tayari ilishamnasa Alvaro Morata lakini mshambuliaji huyo wa Dortmund anadai anataka kujiunga na Mabingwa hao wa kihistoria wa kombe la UEFA Champions league kwani anaamini ndio itakuwa sehemu yake ya mwisho na ya ndoto zake hivyo kuitaka Madrid kama itakuwa tayari kwa Uhamisho huo kukaa mezani na uongozi wa Dortmund.
===========
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Nyota Wa Zamani Wa Man U Aitabiria Ubingwa Chelsea
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA
Aubameyang amewahi kumuahidi babu yake kuwa ipo siku atakuja kucheza katika klabu ya Real Madrid na hayo matumaini yake yanakaribia kutimia.
Mazungumzo ya uhamisho wa Supasta huyo raia wa Gabon kujiunga na Los Blancos yamekuwa yakitawala sana tangu kuisha kwa msimu wa ligi mwaka 2015/16,lakini siku za hivi karibuni Aubameyang ameifungukia klabu yake ya Dortmund kuwa Moyo wake unatamani kujiunga na Real Madrid.
Licha ya kwamba Madrid tayari ilishamnasa Alvaro Morata lakini mshambuliaji huyo wa Dortmund anadai anataka kujiunga na Mabingwa hao wa kihistoria wa kombe la UEFA Champions league kwani anaamini ndio itakuwa sehemu yake ya mwisho na ya ndoto zake hivyo kuitaka Madrid kama itakuwa tayari kwa Uhamisho huo kukaa mezani na uongozi wa Dortmund.
===========
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm
Nyota Wa Zamani Wa Man U Aitabiria Ubingwa Chelsea
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA



































