Kocha wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Hans Van Pluijm amesema Yanga bado ni timu bora zaidi Tanzania Licha ya kuondolewa katika michuano ya kimataifa.
Yanga imetupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC) baada ya kumaliza mechi zake zote sita wakiwa wameambulia pointi 4 tu na kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi A.
Katika mchezo wao wa kwanza katika ligi kuu Vodacom, Yanga imefanikiwa kuichabanga klabu ya African Lyon kwa jumla ya magoli 3-0 kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam.
Kufuatia kipigo hicho walichokitoa kwa African Lyon kocha wa Yanga, amesema licha ya kuondolewa katika kombe la shirikisho Africa bado klabu yake inabaki kuwa bora katika kampeni zake za kutetea taji la ligi kuu kwa mara ya tatu msimu huu wa 2016/17.
“Yanga bado ni timu bora Tanzania licha ya kwamba tupo nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho, cha msingi tumepanga kutetea ubingwa wetu ingawa wachezaji wangu hawakupata muda wa kupumzika lakini tutajitahidi kupambana ili tuweze kutetea ubingwa wetu,” alisema Kocha huyo.
Mholanzi huyo aliendea kusema kuwa licha ya kutupwa nje ya kombe la shirikisho, kitendo chao cha kushiriki katika kombe hilo hadi kufika hatua ya makundi kimewajenga na kuwaimarisha wachezaji wake na anaamini kuwa uwezo wao wa kupambana umeongezeka mara dufu hivyo kuvionya vilabu ambavyo vitakutana na Yanga kuwa Makini kwani vinaweza vikajikuta vikiambulia vipigo vizito vizito, Pluijm alisema kuwa watu wanawabeza kwa kutolewa kwao kwenye michuano hiyo lakini kwake yeye ameona faida kubwa kwani amepata elimu kubwa ambayo ataitumia kwenye mashindano yajayo pamoja na ligi kuu Tanzania Bara.
===========
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
Aubameyang Aitamani Real Madrid
Nyota Wa Zamani Wa Man U Aitabiria Ubingwa Chelsea
Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi
Simba Yabadili Gia Angani
Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza HAPA

0 comments:
Post a Comment