Thursday, June 23, 2016

SUALA LA YANGA KUTAKA MECHI NA MAZEMBE ISOGEZWE MBELE

TFF imesema kuwa imepokea maombi ya Yanga ya kutaka shirikisho hilo kuiandikia CAF wakitaka mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika(CAF-CC) dhidi ya TP Mazembe uchezwe Juni 29 badala ya Juni 28.

“Yanga walipewa nafasi ya kuchagua tarehe tatu za mchezo huo kufanyika ambapo ni tarehe 28, 29 na 30 na CAF na walitakiwa wachague moja ya tarehe hizo na kuthibitisha CAF, lakini hawakufanya hivyo na CAF kuamua mechi hiyo ichezwe tarehe 28 saa 10:00 jioni. “Sasa wamekuja wakitaka tuwasaidie kuwaombea CAF ili mchezo wao uchezwe Juni 29 saa 7:30 usiku kwa hoja ya kutoa nafasi kwa baadhi ya mashabiki wao ambao baadhi yao ni waumini wa dini ya Kiislamu kuweza kushuhudia mechi hiyo na tayari tumeshawaandikia CAF na tunasubiri majibu yao,” alisema Lucas Ofisa Habari wa TFF.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

Related Posts:

  • WANAOWANIA TUZO ZA LIGI KUU VODACOM 2015/16 Utoaji wa tuzo za washindi ligi kuu Vodacom msimu wa 2015/16 utafanyika Julai 17 jijini Dar es Salaam. Wanaowania Tuzo Hizo Ni Kama Ifuatavyo: MCHEZAJI BORA WA KIMATAIFA SH. MILIONI 5.7 Wanaowania Ni; 1. Thaban Kamusoka … Read More
  • PICHA: SIMBA WALIVYOAGWA TAYARI KWENDA KUJIANDAA NA MSIMU UJAO Uongozi wa klabu ya Simba pamoja na wanachama na mashabiki wamekiaga kikosi cha Simba tayari kwenda kuanza mazoezi katika kambi itakayowekwa mkoani Morogoro kujiandaa na kuanza kwa msimu mpya wa ligi Kuu. … Read More
  • NYOTA WATATU YANGA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MEDEAMA Klabu ya Yanga inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya Medeama kutoka nchini Ghana lakini huenda wachezaji wake watatu wakaukosa mchezo huo kutokana na sababu … Read More
  • JERRY MURO ATAKIWA KUWA NA ADABU Sakata la Ofisa habari wa Yanga Jerry Muro kufungiwa mwaka mmoja kutojihusisha na maswala ya soka pamoja na kupigwa faini ya sh. Milioni tatu limechukua sura mpya baada ya viongozi wa TFF kujibu kauli za Msemaji huyo. Kati… Read More
  • CANNAVARO AIPANIA MEDEAMA Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" amesema Ushindi kwenye mechi dhidi ya Medeama ni lazima. Yanga inashiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC) hatua ya makundi na tayari imeshacheza me… Read More

0 comments:

Post a Comment