Friday, June 24, 2016

JKT OLJORO YAMIMINIWA MAMILIONI

Timu ya maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayojiandaa na michuano ya ligi daraja la pili (SDL) msimu wa 2016/17 imekabidhiwa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Shi. Milioni 3.4 kutoka kwa kampuni ya Sanlam.

Vifaa hivyo ni pamoja na Jozi 30, Jezi za mazoezi Jozi 30, soksi za michezo na kofia za jua.
Meneja kanda za juu kaskazini kutoka katika kampuni hiyo, Charles Mwamulenga alisema vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa timu hiyo ikiwa ni moja ya kuwaunga mkono katika mashindao yanayowakabili.

Amos Mwita aliyepokea vifaa hivyo kwa niaba ya mkuu wa kikosi cha Jeshi 833 Oljoro, amesema wanashukuru kampuni hiyo kwa moyo waliouonyesha kwa timu yao na kwamba ni wakati sasa umefika kwa timu hiyo kujipanga ili iweze kufanya vizuri.

"Kama timu hivi sasa itawekeza hamasa yake katika maadalizi ya hali ya juu vile vile itahakikisha inatoa hamasa kwa wapenzi wa soka Arusha ili kuiunga mkono iweze kusonga mbele katika michuano inayoikabili ya SDL" alisema Mwita.

Aidha katibu mkuu wa timu hiyo, Hussein Nalinga amesema kuwa tayari timu yao imeanza kambi kwa takribani wiki mbili sasa na kwamba matarajio yao ni kufanya vizuri.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

0 comments:

Post a Comment