Friday, June 24, 2016

SAKATA LA KESSY YANGA HATIMA YAKE LEO

Suala la beki wa Kulia wa Yanga, Hassan Ramadhan "Kessy" kucheza mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya TP Mazembe  itafahamika leo baada ya kamati ya utendaji Simba kukutana.

Yanga iliwaandikia Simba barua kutaka kujua kama kuna pingamizi lolote juu ya mchezaji huyo baada ya kukataa kutoa kiasi cha fedha ambacho Simba walikihitaji, Yanga pia ilipeleka nakala ya barua hiyo TFF ili endapo Simba watashindwa kulitolea maamuzi hilo mapema ili TFF ichukue hatua.
Hali hiyo imewafanya Simba kupanga kukutana lengo likiwa ni kujadili masuala mbalimbali likiwemo na Suala la Kessy.

Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Simba, Haji Manara amesema uongozi wake haujajibu barua hiyo mpaka pale watakapokutana.

"Leo (Jana) baada ya kumaliza kufuturu tunakutana kwa ajiili ya kupanga vitu mbalimbali lakini suala la barua waliotuandikia Yanga pia itajulikana hapo" alisema Manara.

Aidha Manara alisema baada ya kikao hicho atazungumza na waandishi wa habari leo ili kuwajulisha kilichoamuliwa kwenye kikao hicho.

"Siwezi kusema chochote mpaka kikao kitakapomalizika na baada ya hapo kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari leo hivyo tusubiri" aliongeza Manara.

Yanga walishindwa kumtumia kessy katika mchezo wao wa kwanza waliocheza Algeria kutokana na kutopata ruhusa kutoka kwa klabu ya Simba, na iwapo Simba wataweka pingamizi kuhusu mchezaji huyo watatakiwa kuwa na hoja za msingi za pingamizi hilo ambalo litasikilizwa na kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

Related Posts:

  • Griezmann Kubaki Atletico Madrid Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amedokeza kwamba huenda asiihame klabu yake, licha ya kuwindwa na klabu  kubwa Ulaya ikiwemo Manchester United. Mfaransa huyo wa miaka 26 aliandika kwenye Twitter: "… Read More
  • Ozil, Sanchez Washusha Presha Ya Mashabiki Arsenal Washambuliaji machachari wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil na Alexis Sanchez wameshusha presha ya mashabiki wengi wa Arsenal baada ya uvumi kuenea kuwa nyota hao wataihama klabu hiyo. Taarifa za hivi punde zinadai kuwa wach… Read More
  • Tetesi Mpya Za Usajili Arsenal Ungana na Soka24, kwa habari za papo kwa papo za usajili katika klabu kubwa na pendwa zaidi duniani, hapa nimekuwekea yanayojiri katika klabu ya Arsenal hivi sasa. Arsenal katika mbio za Kumuwania Mbappe klabu ya Arsenal… Read More
  • PSG Wakubali Yaishe Kwa Aubameyang Vigogo wa soka nchini Ufaransa, PSG wamekubali kutoa paundi milioni 61 kuinasa saini ya mshambuliaji wa Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang. Licha ya gharama hizo za uhamisho PSG pia wamekubali kumlipa nyota huyo kutoka b… Read More
  • Simba Wapata Mbadala Wa Juuko Murshid Munezero Fiston ni Mnyarwanda ambaye yupo katika mipango ya Simba baada ya kocha Joseph Omog kupendekeza atafutiwe mchezaji mwingine. Munezero, anayekipiga katika klabu ya Rayon Sport anatarajiwa kutua Dar Es Salaam Juma… Read More

0 comments:

Post a Comment