Sunday, May 8, 2016

MECHI 2 KALI ZA KUZITAZAMA LEO LIGI KUU TANZANIA BARA


SIMBA SC VS MWADUI FC

Simba leo wanawakaribisha Mwadui FC katika mchezo wa 27 wa Ligi kuu Tanzania Bara, Simba wanaingia katika mechi hii wakiwa na rekodi mbaya katika mechi za hivi karibuni, kwanii hutakiwi kukosa kuitazama mechi hii: Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwelu Julio amewahi kuifundisha klabu ya Simba, hivi karibuni Julio ameutuhumu uongozi wa Simba kuwa ni wabinafsi, waroho na wakorofi ndio kisa Simba haifanyi vizuri kwa sasa, kama hiyo haitoshi, Simba wanaingia katika mchezo huu wakiwa katika nafasi ya 2 wakiwa na pointi 58 katika msimamo wa ligi baada ya Azam kunyang’anywa pointi tatu kwa kosa la kumchezesha Erasto Nyoni katika mechi na Mbeya City huku akiwa ana kadi 3 za njano, Simba wanahitaji kushinda mchezo wa leo ili kuizuia Yanga kutotangaza ubingwa wa Ligi kuu Msimu huu mapema, lakini kinachoongeza ladha zaidi katika mechi hii ni kauli ya Julio kocha wa Mwadui aliyosema hivi karibuni kuwa anataka Mwadui wafanye kama walivyofanya Chelsea nchini England baada ya kutoa sare na Tottenham na kuifananya Leicester City kuwa mabingwa wa Ligi kuu nchini humo.

AZAM FC VS KAGERA SUGAR

Azam FC wamesafiri kuifuata Kagera Sugar katika mchezo wao wa ligi leo, Hivi karibuni Azam FC wamepokwa pointi 3 kwa uzembe wa kumchezesha Nyoni aliyekuwa na kadi 3 za njano, katika mchezo huu Azam FC wanahitaji ushindi ili kurudisha matumaini kwa waajiri wao kutokana na mwenendo wao mbovu katika ligi huku pia wakisemwa kuwa hawalipi fadhila wanazofanyiwa na waajiri wao, ili kuleta hali ya utulivu katika klabu hiyo wanahitaji kushinda mchezo wa leo, lakini kwa upande mwingine Kagera Sugar wao hawatakubali kufungwa kirahisi hivyo kwani nafasi yao katika Msimamo wa ligi ni mbaya, wanashika nafasi ya 3 kutoka mwishoni wakiwa na tofauti ya pointi 2 tu na Mgambo JKT ambao wapo katika nafasi ya kushuka Daraja, hivyo kuna kila sababu kwa Kagera Sugar kupambana vilivyo katika mechi hii ili kujihakikishia usalama wao wa kubaki katika ligi kuu.


0 comments:

Post a Comment