Saturday, May 21, 2016

DENIS KITAMBI KATIKA MTIHANI MZITO AZAM FC

Kocha Msaidizi wa Azam FC  Denis Kitambi Ataiongoza klabu hiyo katika mchezo wa mwisho wa Ligi katika kuwania nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.


Ligi Kuu Tanzania Bara inaelekea ukingoni na mechi za mwisho zitachezwa Jumapili hii Mei 22. Azam FC itashuka dimbani Mei 22 katika uwanja wao wa Chamanzi Complex wakiikaribisha Mgambo JKT. Itakumbukwa kuwa Azam Fc ilishaachana na makocha wao wote waliokuja pamoja na kocha Stewart Hall na hivyo timu sasa kubaki chini ya kocha Denis Kitambi, kwani Makocha wapya waliosaini hivi karibuni wataanza majukumu ya kuiongoza Azam katika michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kutimua vumbi hivi karibuni.
Azam Fc Wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Mgambo JKT

Azam Inashika nafasi ya pili kwa kujikusanyia alama 63 huku wakiwazidi Simba inayoshika nafasi ya 3 kwa pointi 1 tu, hivyo kufanya mchezo wa mwisho kati yao na Mgambo kuwa mtihani mzito kwa kocha Kitambi kuhakikisha anaipa Azam nafasi ya pili katika ligi kuu Tanzania Bara Msimu huu kwa kushinda mechi hiyo.

Kabla ya kuwa kocha Msaidizi hapo Azam FC Kitambi alishawahi kuwa kocha mkuu baada ya aliyekuwa kocha mkuu wakati huo kutimuliwa na uongozi wa Azam na alikuja kushushwa na kuwa kocha msaidizi baada ya kuwasili kwa kocha muingereza Stewart Hall ambae ameacha kibarua hicho kwa kile alichodai amechoka kufundisha soka la Tanzania na sasa anataka kwenda kujaribu kwingine.

0 comments:

Post a Comment