Friday, April 15, 2016

Wachezaji Tano Waliofariki Uwanjani


Mpira wa miguu ni moja kati ya michezo inayopendwa zaidi duniani. Mashabiki na wapenzi wa mchezo huo hufurahia pale wanapowaona wachezaji wao wakifanya vitu vizuri uwanjani, wengine furaha zao hupitiliza hadi kuwa vilio. Hakika soka limeiteka dunia.

Licha ya burudani yote tunayoipata katika mchezo huo, yapo matukio pia ambayo yanatokea katika mchezo huo wa mpira wa miguu ambayo yanatukosesha raha kabisa na hata kufikia hatua ya kututoa machozi, hii hutokea hasa pale tunapoona wale tunaowatazama kwa maana ya wachezaji hupatwa na vitu ambavyo machoni kwetu vinakuwa sio vya kawaida.

Soka24 inakuletea orodha ya wachezaji 5 ambao kwa bahati mbaya vifo vyao vilitokana na huu mchezo wa mpira wa miguu wakati wakipambana kuzisaidia timu zao kuibuka mabingwa. Najua itakuhudhunisha hasa kama ukiwa mdau hasa wa soka ila hatuna budi kumwachia mungu huku tukiwaombea wapumzishwe mahali salama Ameen.

5. Peter Biaksangzuala- India



Mchezaji huyo aliefariki akiwa na umri wa miaka 23 raia wa nchini India, alipata umauti baada ya kusawazisha goli dhidi ya wapinzani wao timu ya Chnmari West Fc. Baada ya kusawazisha goli hilo alikimbia kwa furaha akishangilia goli alilofunga, kwa bahati mbaya akaanguka vibaya, wachezaji wenzie walipoona hali hiyo walimkimbilia kumpa msaada lakini Peter aliaga dunia baada ya kukimbizwa hospitalini.

4. Miklos Feher- Ureno



Beki huyo wa timu ya Sao Caetano alikimbizwa hospitalini akiwa katika hali mbaya baada ya kuanguka peke yake uwanjani wakicheza dhidi ya klabu ya Sao Paula October 27 mwaka 2004. Taarifa kutoka kwa daktari wa timu hiyo zilionyesha Miklos alipatwa na Ugonjwa wa moyo ( Heart Attack ) uliopelekea kifo chake. Taarifa za kifo chake ziliacha majonzi makubwa kwa wapenzi na mashabiki wa soka ulimwenguni.

3. Serhiy Perkhun- Russia


Serhiy Golikipa wa timu ya CSKA Moscow alikutwa na umauti kufuatia kugongana maeneo ya kichwani na mchezaji mwenzake uwanjani katika Mchezo wa Ligi kuu nchini Urusi ( Russian Premier Division ) August 29 mwaka 2001. Golikipa huyo raia wa Ukraine alipata kazia hiyo baada ya kugongana na straika wa Anzhi Makhachkala katika kipindi cha pili cha mechi hiyo ambayo iliisha kwa suluhu ya 0 – 0. Serhiy alifariki siku 8 baadae baada ya kupelekwa hospitali ambako hali yake ilizidi kuwa mbaya kadri siku zikivyozidi.

2. Albert Ebosse- Cameroon


Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon alifariki saa chache hospitalini baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani akichezea klabu ya JS Kabylie ya Nchini Algeria. Kitu hicho kizito kilichorushwa na shabiki kilimpiga kichwani dakika chache baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza, ilikuwa ni mwaka 2014.

1. Marc-Vivien Foe- Cameroon


Mkameruni huyo ambae alishawahi kuichezea Man Utd msimu wa 2002-2003 alifariki kutokana na kufeli kwa mapigo yake ya moyo. Tukio hilo lilitokea June 26 mwaka 2003 katika mchezo wa Robo fainali ya kombe la mabara wakati Cameroon ilipokuwa ikicheza na Colombia dakika ya 72 ya mchezo.

Mwenyezi Mungu azilaze mahala pema roho za wachezaji hawa Ameen.

0 comments:

Post a Comment