Friday, June 24, 2016

KAPOMBE,WAWA WATUA SAUZI KWA UCHUNGUZI

NYOTA wawili wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe na Pascal Wawa hivi sasa wapo jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya zao.

Mabeki hao waliondoka nchini tokea Jumanne iliyopita wakiongozana na Daktari wa Azam FC, Juma Mwimbe, ambapo watafanyiwa vipimo vya afya kwenye Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo jijini humo.

Daktari huyo ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz  kuwa wachezaji hao tayari leo wamekutana na madaktari watakaowafanyia uchunguzi na kesho watachukuliwa vipimo kabla ya kupewa majibu yao juu ya matatizo yanayowakabili.

“Wawa amekuja huku kufanyiwa uchunguzi wa goti lake la kushoto linalomsumbua, kama unavyojua Kapombe yeye alishaanza matibabu ya tatizo lake la Pulmonary Embolism alilopata msimu uliopita.

“Hivyo naye yuko hapa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kuangalia maendeleo yake baada ya kutumia dawa za awali alizopewa wakati wa mwanzo alipopata tatizo hilo, lakini afya yake inaendelea vizuri kabisa kwa sasa,” alisema.

Wachezaji hao wote walipata matatizo ya kiafya kuelekea mwishoni mwa msimu na kupelekea kukosa mechi zote za Azam FC zilizobakia kwa msimu huo.

Wawa alipata majeraha ya goti dakika za mwisho katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia, ambao Azam FC ilishinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Farid Mussa na Ramadhan Singano ‘Messi’.

Kapombe yeye alipata tatizo hilo la kiafya wakati Azam FC ikiwa mkoani Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Toto Africans, ulioisha kwa sare ya bao 1-1, bao la mabingwa hao likifungwa na nahodha John Bocco ‘Adebayor’ na Wazir Junior akiifungia Toto.

CHANZO: Azam FC Official Site

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa


Related Posts:

  • Al Ahly Waanza MbwembweKocha Mholanzi wa Al Ahly ya Misri ameiongoza timu yake katika mazoezi jioni ya leo Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, lakini Waandishi wa Habari wakazuiwa kuingia. Al Ahly waliweka walinzi wao pamoja na walinzi wa Gymkhana k… Read More
  • Hall: Tulishindwa Kutimiza Majukumu Yetu Uwanjani UKIACHILIA mbali malalamiko ya waamuzi, Kocha Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Stewart Hall, amesema kuwa wameporwa ushindi na Ndanda jana baada ya wachezaji kushindwa kutimiza ipasavyo majukumu ya… Read More
  • Kapombe Akimbizwa Sauzi Kwa MatibabuBEKI kisiki wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, ameondoka nchini leo saa 9.35 Alasiri akielekea Afrika Kusini kwa ajili ya kutibiwa kifua ambacho kinamsumbua. Kapombe aliyekosa mechi mbili… Read More
  • Kikosi Cha Esperance De Tunis Kutua Nchini Leo Kikosi Cha Esperance De Tunis Azam inatarajia kuvaana na Esperance katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, mechi ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, keshokutwa Jumapili. Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saadi Kawemb… Read More
  • Msaidizi Wa Jamali Malinzi Asimamishwa Kazi TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amemsimamisha Juma Matandika kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazohusiana na hadhi za wachezaji (players status). Hatua hii imechukuliwa kwa mujibu … Read More

0 comments:

Post a Comment