Thursday, April 14, 2016

Wachezaji 5 Matajiri Zaidi Duniani

Kama ulikuwa hujui mpira wa miguu ni moja kati ya michezo inayopendwa zaidi duniani. Inaweza ikakushangaza lakini ukweli ndio uko hivyo. Na kutokana na ukweli huo, wachezaji bora wanapata pesa nyingi sana, kama ulishawahi kutamani kuwa kama mmoja wa miongoni mwa masupastaa wa soka duniani ndivyo leo utakavyotamani mamilioni ya pesa wanazopata mastaa hao.

Soka24 inakuletea orodha ya wachezaji watano matajiri zaidi duniani, utajiri wao ukihusisha mishahara yao wanayopata, pesa zinazotokana na mikataba wanayosaini na makampuni mbalimbali na malupulupu mengine yanayotokana na kazi yao hiyo ya uchezaji mpira.

Hii ndio orodha ya wachezaji 5 matajiri katika sayari hii ya Dunia.

5.  Wayne Rooney
      Wayne Rooney anacheza kama straika katika klabu yake ya Man Utd na timu yake ya taifa ya Uingereza, na ni mchezaji tajiri zaidi katika ligu kuu soka nchini Uingereza, anajulikana kwa ustadi wake akiwa uwanjani. Staa huyo wa soka ana utajiri wenye thamani ya Dola Milioni 112.

4.  Zlatan Ibrahimovic
    Zlatan Ibrahimovic ni mshambuliaji Supastaa wa Paris Saint-Germain katika ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Utajiri wa Ibrahimovic unatokana pia na mikataba ya makumpuni makubwa yanayomdhamini ikiwemo Nivea, Xbox, Volvo na Dressman. Cadabra ana utajiri wenye thamani ya Dola Milioni 114.

3.  Neymar
      Neymar ni kioo cha Wabrazili na ni moja kati ya  wachezaji tegemeo katika kikosi cha Barcelona. Uwezo wake wa kuchezea mpira uwanjani umemfanya kuwa mchezaji maarufu zaidi ulimwenguni. Mshahara wake kwa mwaka ni paundi milioni 8.8, ni mshahara mdogo ukilinganisha na pesa anazovuna kutokana na kuingia mikataba na makampuni makubwa kama vile Nike, Panasonic, Volkswagen, Red Bull na mengine mengi. Kijana huyo ana utajiri wa Dola za kimarekani Milioni 148.

2.     Lionel Messi
        Lionel Messi sio tu mkali akiwa uwanjani lakini pia Mfanyabiashara mzuri wa kazi yake hiyo. Mkataba wake mnono na Barcelona unamlipa jumla ya Dola milioni 50 kwa mwaka na ana mikataba lukuki inayomuingizia pesa. Anafanya kazi na makampuni ya Adidas, Samsung, Gillete, Gatorade na Dolce & Gabbana. Messi ni kati ya wachezaji wawili bora Duniani na kufikia hivi sasa ameshashinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 5. Raia huyo wa kiagentina ana utajiri wa Dola milioni 218.

1 Christiano Ronaldo
Hakitakuwa kitu cha kushangaza kwa CR7 kuwa namba moja katika list hii. Kwa mtu yoyote anaefuatilia michezo vizuri, atajua Ronaldo ni Mchezaji bora wa mabora duniani yani kwa kimombo ( Best Of the Best). Anafunga magoli mengi, ana kasi ya ajabu ya kukimbia na mpira na ana uwezo wa ajabu wa kumiliki mpira yani Ball control, mkataba wake na Real Madrid unamlipa paundi milioni 18.2 kwa mwaka na kiwango hicho cha pesa hakihusishi malupulupu mengine. Ronaldo ana nguo zake zenye nembo ya CR7. Licha ya pesa nyingi anazotengeneza mchezaji huyo kupitia makampuni mbalimbali yanayomdhamini ili kuwatangazia bidhaa zao, inamlipa pesa nyingi yeye kuwa Christiano Ronaldo. Mkali huyo kutoka nchini Ureno ana utajiri wa Dola za kimarekani milioni 230.

0 comments:

Post a Comment