Thursday, April 14, 2016
Azam Fc Yazuiwa Kuvuka Barabara Mvomero Mkoani Morogoro
BARABARA ya Kijiji cha Mvomero, mkoani Morogoro ililazimika kutopitika kwa takribani dakika 15 kufuatia mashabiki wa soka wa kijiji hicho kujazana kwa wingi na kufunga barabara hiyo wakati wakiipokea Azam FC iliyotoka kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) jana jioni.
Tukio hilo lilitokea saa 1 usiku wakati kikosi cha Azam FC kilipokuwa kikishuka kwenye basi dogo la timu kuelekea kupanda basi kubwa la timu lililokuwa limepaki kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mvomero.
Azam FC ililazimika kuondoka na basi dogo la timu kutokea hapo Mvomero kutokana na miundombinu mibovu ya barabara kuelekea kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, hivyo mashabiki hao takribani 100 waliochanganyika rika na jinsia zote walilazimika kusubiria kwa takribani saa mbili hadi kikosi hicho kiliporejea tena hapo kupanda basi hilo kubwa mara baada ya mchezo huo.
Mara baada ya Azam FC kuwasili hapo mashabiki hao walishangilia kwa nguvu na kuwapongeza wachezaji kila walipopita na kupelekea magari yaliyopita njia hiyo kusimama na kusubiria tukio hilo liishe kutokana na kuwa na msongamano wa watu wengi walioziba barabara.
Mashabiki wengine waliokuwa na baiskeli na pikipiki walidaiwa kutokea vijiji vya karibu na hapo ili kuwaona nyota wa Azam FC watakapokuwa wakiwasili eneo hilo kupanda basi hilo na hata lilipoondoka kila sehemu timu hiyo ilipopita mashabiki walisikika kupiga miluzi na kuita majina ya baadhi ya wachezaji akiwemo John Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga bao hilo pekee jana.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB mpaka sasa imekuwa ikijizolea mashabiki wengi katika sehemu mbalimbali nchini kutokana na namna inavyoendesha timu kisasa na matokeo mazuri wanayopata uwanjani kwenye ligi na michuano ya Kimataifa.
Chanzo: Azam Fc Official Site
Related Posts:
George Lwandamina Aifungukia Simba SC Kocha wa mabingwa soka Tanzania bara Timu ya Yanga Mzambia George Lwandamina ametamba kwamba mechi dhidi ya timu ya Ngaya Club ya Comoro katika mchezo wa klabu bingwa afrika zitawapa taswira nzuri kabla ya kuvaana na maasimu… Read More
16 Bora Azam Federation Cup ratiba yatangazwa, michezo 8 kufanyika kwa siku tatu tofauti Michuano ya kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) hatua ya 16 bora kutimua vumbi February 24 na February 26 na march 7 katika mikoa sita ya Tanzania Bara. February 24 kutakuwa na michezo minne katika mikoa min… Read More
Mkwasa Arejea Yanga Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa kuwa katibu mkuu Yanga Afrika kwa mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa katibu mkuu Baraka Deusdedit anarejea katika nafasi yake ya awali ya utunza fedha. Akizungumza baada ya kurejea kik… Read More
Serengeti Boys hiyooo AFCON U17, 2017 Serengeti Boys … Read More
Rungu La TFF Latua Kwa Hemed Morocco Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Morocco kushiriki michezo mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000. atika mechi Na. 160 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu z… Read More
0 comments:
Post a Comment