Thursday, April 14, 2016

Legendari wa Chelsea Didier Drogba Kulishitaki Gazeti La Daily Mail.


Didier Drogba anaecheza katika ligi ya MLS (Major League Soccer) akiitumikia klabu ya Montreaal atalifungulia mashitaka gazeti la Daily Mail kufuatia tuhuma ambazo gazeti hilo limezitoa zikimuhusisha Nyota huyo wa Ivory Coast.



Licha ya kucheza dakika 20 pekee katika klabu yake ya Montreal tangu mwaka 2016 uanze Drogba anarekodi nzuri inayombeba zaidi katika ligi hiyo.

Alhamisi iliyopita gazeti la Daily Mail lilichapisha habari inayohusisha taasisi ya Didier Drogba inayojulikana kama Didier Drogba Foundation, taasisi ambayo ilianzishwa na Didier Drogba mwenyewe.

Gazeti hilo limeripoti kuwa Taasisi hiyo ya Didier Drogba imekula pesa zaidi ya Paundi Milioni 1.5 ambazo zilichangishwa kwa lengo la kuwasaidi Waafrika wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali, pia kwa lengo la kujenga hospitali pamoja na kusaidia kuwasomesha Waafrika ambao wanaishi katika mazingira magumu. Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti hilo kiasi cha paundi elf 14,115/- tu ndo kimefika kwa walengwa.

Harambee hiyo ambayo ilifanywa na mastaa wa soka, viongozi mbalimbali na wafanyabiashara Nchini Uingereza wakiwemo Bono, Frank Lampard na Christian Bleakley ilitegemewa kwenda kusaidia Waafrika wanaoteseka Barani Afrika.

Hii ni kashfa kubwa zaidi kuwahi kumkuta Drogba na Foundation yake, lakini Drogba amekanusha tuhuma hizo na kupanga kulipeleka gazeti hilo mbele ya sheria. Katika post yake ya instagram Drogba aliliponda gazeti hilo kwa kusema linalengo la kuhatarisha maisha ya maelfu ya watoto wa kiafrika ambao wanasaidiwa kupitia Foundation hiyo.

0 comments:

Post a Comment