Friday, April 15, 2016

Liverpool Warudia Maajabu Waliyoyafanya Mwaka 2005 Ilipocheza Na AC Milan

Majogoo wa Anfield jana walikuwa kibaruani kuikabili klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani katika mchezo wa pili wa robo fainali wa kombe la Europa League.
Mechi hiyo iliyokuwa ya kasi ilishuhudia Liverpool ikichapwa goli mbili hadi kufikia dakika ya nane ya kipindi cha kwanza cha mchezo magoli yaliyofungwa na Mkhitaryan na Aubameyang. 

Vijana hao waliochini ya kocha machachari Klopp walienda mapumziko wakiwa nyuma kwa goli mbili kwa bila.

kipindi cha pili kilianza kwa kasi Dortmund wakihitaji kuongeza bao la tatu ili kujihakikishia ushindi Liverpool nao wakihitaji kusawazisha magoli hayo na kuongeza mengine. Jitihada za Liverpool zilizaa matunda baada ya Divock Origi kuipatia Liverpool goli la kwanza dakika ya 48, lakini goli hilo halikudumu sana baada ya Reus kuiongezea Dortmund goli la tatu goli ambalo lilipoteza matumaini ya ushindi kwa mashabiki wa Liverpool waliokafurika uwanjani hapo huku wakiimba nyimbo yao maarufu ijulikanayo kama YOU'LL NEVER WALK ALONE.
Lakini Jurgen Klopp alizidi kuwahamasisha vijana wake huku akiwaaminisha kuwa wanaweza kushinda mechi hiyo endapo tu watatulia na kucheza mpira vizuri. Gafla mambo yakabadilika katika dimba hilo la Anfield baada ya Mshambuliaji hatari kutoka Nchini Brazil Coutinho kuifungia Liverpool goli la pili dakika ya 66 . Liverpool waliendelea kupambana huku Mshambuliaji wa Dortmund Emeric Aubameyang akipoteza nafasi nyingi za wazi langoni kwa Liverpool ilipofika dakika ya 77 beki wa Liverpool Sakho akaipatia Liverpool goli la kusawazisha kufuatia mpira wa kona. Tukiwa tunaamini mechi itaisha kwa sare ya 3 - 3, Beki Lovren aliipatia Liverpool goli la ushindi dakika za nyongeza  kufuatia mpira wa adhabu ndogo. hadi mechi inaisha Liverpool 4 - 3 Dortmund.

Mechi hiyo haijatofautiana sana na mechi ambayo Liverpool walicheza mwaka 2005 fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya AC Milan ambapo hadi timu hizo zinaenda mapumziko Liverpool ilikuwa nyuma kwa goli 3 kwa bila lakini waliingia kipindi cha pili wakarudisha magoli hayo na hatimaye kutoka na ushindi uliotokana na mikwaju ya penati.
hivyo Liverpool inafuzu kucheza hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment