Mchezaji wa Simba Abdi Banda anasema hajui mustakabali wake katika Klabu hiyo kufuatia tamko la adhabu aliyopewa kutokana na kupishana kauli na kocha wake Jackson Mayanja katika mechi dhidi ya Coastal Union.
Anasema hawaelewi viongozi wa simba nini wanaplan juu yake yeye kwani wako kimya na yeye hajui lolote linaloendelea.
“Nilipeleka barua yangu ya maelezo Machi 28 (mwaka huu), mpaka sasa sijaambiwa chochote. Wamenifungia vioo hawaniambii chochote. Nasikia wameamua kulipeleka suala langu katika Kamati ya Nidhamu ila kwa upande wangu sina hofu yoyote kwa kuwa naendelea kufanya mambo yangu mengine,” alisema Banda.
0 comments:
Post a Comment