Mashabiki wa Klabu ya Dar Young Africans wameonyesha kutokufurahishwa na kiwango kinachoonyeshwa na mshambuliaji wao Amis Tambwe siku za hivi karibuni.
Tambwe ambe ana magoli 18 katika orodha ya wafungaji bora msimu huu anaonekana kupwaya katika mechi alizocheza siku za karibuni.
Baada ya mechi ya juzi Yanga dhidi ya Mwadui Fc mashabiki wa Yanga walionekana kumpigia kelele kocha wa timu hiyo Hans wakimwambia kuwa kwa sasa Tambwe anapaswa kukaa benchi na nafasi yake kuchukuliwa na Malimi Busungu.
"Sijui ni kwanini ila nitakaa na washambuliaji wangu waniambie wana matatizo gani kwani siyo kawaida yao,” alisema Pluijm ambaye pia alisema haridhishwi na kiwango cha sasa cha mshambuliaji wake mwingine, Donald Ngoma.
0 comments:
Post a Comment