Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF limeiondoa klabu ya ES Setif kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika 2016.
Hatua hiyo inakuja kufuatia vurugu zilizosababishwa na mashabiki wa timu hiyo kwenye mchezo kati yao na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Mashabiki hao walianzisha vurugu baada ya Tiyani Mabunda na Biliat Khama kufunga magoli mawili yaliyoifanya ya Mamelodi kuwa mbele kwa 2 - 0 katika mechi hiyo.
"(Maamuzi yamefanyika kufuatia vurugu zilizotokea katika mchezo namba 98 wa mwaka 2016 mechi ya klabu bingwa kati ya ES Setif (Algeria) dhidi ya Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), ambapo mwamuzi wa kati alilazimika kuahirisha mchezo huo kabla ya dakika tisini kumalizika" iliandikwa katika maelezo ya CAF.
Maofisa wa mchezo huo walisema waliona mashabiki wakirusha vitu uwanjani hapo kama vile, chupa, mawe na vitu vingine ambavyo vilisababisha majeraha kwa watazamaji wengine waliokuwepo uwanjani hapo kushuhudia mtanange huo pamoja na polisi waliokuwa wanalinda usalama wa mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment