Friday, June 24, 2016

KIBARUA CHA LAURENT BLANC CHAOTA NYASI PSG

Klabu ya PSG imemtimua kocha wake Laurent Blanc, kwa mujibu wa jarida la la L'Equipe la nchini Ufaransa.

Taarifa za kutimuliwa kwa kocha huyo bado hazijawa rasmi kwani mpaka hivi sasa klabu ya PSG haijatoa tamko rasmi lakini kwa mujibu wa L'Equipe  tayari kocha huyo ashafungishwa virago.
Kwa mujibu wa gazeti hilo ni kwamba PSG walilazimika kumlipa Blanc Euro milioni 22 kwa kukatisha mkataba wake.

Kocha huyo ameshinda mataji 2 ya kombe la Ufaransa pamoja na makombe matatu ya ligi kuu katika misimu yake mitatu aliyoitumikia PSG, lakini rekodi zake mbaya katika michuano ya Klabu bingwa ulaya ndiyo iliyomfanya awashiwe taa za kijani klabuni hapo.

Wamiliki wa timu hiyo raia wa Quatar tamaa yao ni kuona PSG wakitwaa ubingwa wa Uefa Champions League kitu ambacho kocha Blanc ameshindwa kuwapa.

Habari za chini ya kapeti zinasema huenda kocha Unai Emery anaweza kurithi mikoba ya Blanc kwani kwa sasa hana klabu yoyote tangu abwage manyanga katika klabu ya Sevilla.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

0 comments:

Post a Comment