Wednesday, April 13, 2016

Mambo 15 Yakuyajua Kuhusu Christiano Ronaldo "CR7"


Mkali wa soka Christiano Ronaldo ana miaka 31 kwa sasa ila makali yake uwanjani ni kama kijana wa miaka 20, Tunaweza kuamaini kuwa Ronaldo anaweza kucheza miaka 10 zaidi mbele kutokana na kasi yake alokuwa nayo ukizingatia wachezaji wengi punde wafikishapo miaka 30 kiwango chao hushuka kwa kiasi kikubwa sana. Siri yake ya Mafanikio ilidhihirika siku alipoulizwa baada ya Kushinda Ballon d’Or mwaka 2014 kwamba nini malengo yake yambeleni, Ronaldo akasema ni Kushinda Ballon d’Or nyingine.
Ukweli juu ya uzito gani anaweza kunyanyua na jinsi uwezo wake wa kuruka unavyolinganishwa na chui utakufanya umpende Nyota huyu zaidi na zaidi.

Soka24 inakuletea mkusanyika wa baadhi ya mambo ambayo yatakufanya ufurahi.
1.       Jina ,Christiano Ronaldo alipewa kufuatia jina la Rais wa Marekani bwana Ronald Reagan ambaye alikuwa mwigizaji na kipenzi kikubwa cha baba yake Ronaldo. Alizaliwa mwezi wa pili tarehe 5 mwaka 1985, baba yake alikuwa anaitwa Jose Dinis Aveiro na mama yake ni Dolores Dos Santos Aveiro.

2.       Alikuwa na majina mengi sana ya utani alipokawa mdogo “alipokuwa anarudi kutoka shule nilikuwa namwambia afanye Homework zake lakini alikuwa anajibu hana Homework yoyote ya kufanya, nilikuwa namuandalia chakula na baadae alikuwa anatoroka kupitia dirishani na kwenda kucheza na alikuwa anachelewa kurudi, alikuwa analia kila mara anapofaulu huku rafiki zake wa karibu wakiwa wamefeli jambo lililopekea wenzie wamuite “Crying Baby” yani mtoto wa kulialia, aliitwa pia “little bee” yani nyuki mdogo” alisema mama yake Ronaldo Dolores Aveiro.

3.       Akiwa na miaka 15 Ronaldo aligundulika na Ugonjwa Unaojulikana kama “Racing Heart” yani mapigo ya moyo kwenda kasi. Alifanyiwa upasuaji katika eneo lake la moyo na upasuaji huo ulifanikiwa ukamwezesha Ronaldo kuendelea na Masomo yake na Mafunzo ya mpira.

4.       Kitu cha kushangaza zaidi akiwa bado mdogo, Ronaldo alikuwa anapenda kufanya mazoezi ya mpira akiwa amejifunga vitu vizito miguuni kwake huku akikimbia na mpira kitu ambacho yeye mwenyewe alikuwa anaamini kitamfanya awe mwepesi na mwenye kasi zaidi uwanjani.

5.       Unajua speed ( mwendo kasi ) ya mpira wa adhabu anaopiga Ronaldo!!!!!!, ni speed 130 kilometa kwa saa. Bila shaka mazoezi ya kufunga vyuma miguuni yamefanya kazi.

6.       CR7 ananguvu mara 5 zaidi ya chui, zinazomwezesha kuruka ukilinganisha na chui anaporuka katika kiwango chake cha mwisho. Speed hiyo ya kuruka inamfanya afike urefu wa 44cm angani kutoka aridhini ambayo ni zaidi ya wastani wa mchezaji wa NBA anavyoweza kuruka.

7.       Kama ulikuwa unadhani wewe ndo bora zaidi katika kunyanyua vitu vizito haupo peke yako. Ronaldo ananyanyua kitu chenye uzito wa kilogram 23,055 kila mara anapofanya mazoezi, yani ni sawa na kuyavuta magari 16 aina ya Toyota Prius.

8.       Ronaldo alisaini Mkataba Mnono na Real Madrid, mkataba uliomfanya kuwa mchezaji anaelipwa zaidi duniani.

9.       Inasemekana CR7 alishawahi kumlipia mtoto wa miaka 9 gharama za matibabu ya kansa kitu kinachomfanya aonekane ni mtu mkarimu na mwenye huruma pia.

10.   Tuna majina makubwa ya wachezaji waliovaa jezi namba 7 duniani , Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckam, wapo baadhi ya wachezaji hukataa pindi wanapopewa jezi zenye namba 7, chakushangaza Ronaldo aliikubali jezi hiyo tena kwa kujiamini akiwa na umri wa miaka 18 pekee.

11.   Mwaka 2006 Ronaldo alianzisha duka la nguo mjini Madeira Ureno. Duka ambalo alilipa jina la CR7.

12.   Tofauti na Mastaa wengi wa soka duniani kwa sasa, Ronaldo hana Tattoo yoyote katika mwili wake na hana haja na tattoo, kitu kinachomuwezesha Ronaldo kuchangia damu kila mwaka.

13.   Watu wengi wenye pesa hutumbukia katika starehe kama vile unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara wengine hupitiliza zaidi hadi kuvuta bangi, Ronaldo yeye havuti wala hanywi pombe, akikumbuka baba yake alifariki akiwa na umri wa miaka 52 kwa ulevi wa kupindukia pia anahofu starehe hizo zisije zikaharibu uwezo wake uwanjani.

14.   Mafanikio ya Ronaldo ni pamoja na kuwa Mchezaji bora wa mwaka wa FIFA, Mshindi wa Mchezaji bora wa dunia mara 3, Mfungaji bora ( Golden Boot) na ameshinda pia tuzo ya Mshambuliaji hatari zaidi wa UEFA wa mwaka.

15.   Mwezi wa 11 mwaka 2012 Ronaldo alisaidia Shule ya watoto mjini Gaza, pesa ambazo alizipata baada ya kuuza kiatu chake cha dhahabu alichoshinda mwaka 2011 chenye thamani ya paundi milioni 1.5.

Huyo ndo Mkali wa soka Duniani Chrisitano Ronaldo Dos Santos Aveira almaarufu kama CR7

0 comments:

Post a Comment