Klabu ya Manchester United imejikuta ikishuka thamani yake katika soka la hisa kwa zaidi ya paundi
Milioni 400 katika msimu wa mwaka 2015/2016 kutokana na mwenendo mbovu wa klabu
hiyo kwa sasa.
Kushuka huko kwa thamani kumechangiwa pia na kichapo cha
hivi karibuni walichokipata mashetani wekundu hao kutoka kwa Tottenham
Hotspurs.
Ripoti inaonyesha kwa kipindi cha miezi nane Manchester
United imeshuka kutoka Paun za Uingereza Bilioni 2 hadi kufikia Paun Bilioni
1.58. Imekuwa ni bahati mbaya zaidi kwa kocha Louis Van Gaal kwani tangu
anachukua timu mwaka 2014 thamani ya Manchester United katika soko la hisa
ilikuwa ni Paun Milioni 650 kiwango kikubwa zaidi ukilinganisha na hali jinsi
ilivyo kwa sasa.
Hali hiyo inayoikumba Manchester United kwa sasa imetokana pia na Kuondolewa kwao katika mashindano ya UEFA Champions League mwezi Disemba
mwaka jana.
United wana Mlima
mrefu wa kuupanda kama wanataka kutetea nafasi yao katika Ligi Kuu Nchini
Uingereza na kumaliza katika nafasi nne za juu. Kipigo cha 3-0 kutoka kwa
Tottenham kimewaacha United pointi 4 nyuma ya Manchester City huku zikiwa
zimebaki mechi sita tu kumaliza msimu.
Robo fainali ya FA wikendi hii huenda ikawapa United nafasi ya
Kwenda Wembly endapo watafanikiwa kuwaondosha wagonga nyundo West Ham United.
0 comments:
Post a Comment