Wednesday, April 13, 2016

Yanga Na Azam Fc Zasusia Ratiba Kombe La FA

Hili ndo Kombe La ASFC
Yanga na Azam Fc zimesusia Ratiba ya michuano ya Azam Sports Federation Cup hatua ya nusu fainali iliyopangwa kufanyika  April 24 mwaka huu. Timu zote zimetoa sababu ya kushiriki michuano ya kumataifa, Michuano ambayo imekaribiana na ratiba hiyo ya ASFC. Azam Fc imepangwa kukutana na Mwadui ambapo mechi ya kwanza itapigwa Mkoani Shinyanga huku Yanga ikisafiri kuifuata Coastal Union Jijini Tanga.

Kiongozi wa Azam Fc Kawemba alisema watacheza mechi Tunisia tarehe 20 kwa maana hiyo wataondoka huko tarehe 21, hivyo itakuwa vigumu kufika Tanzania na kusafiri tena kwenda Mwadui kucheza mechi hiyo ya nusu Fainali.
Aliongeza kwa kulishauri shirikisho la mpira Tanzania TFF kuangalia uwezekano wa kuisogeza mbele michuano hiyo ili kila timu ipate nafasi ya kujiandaa vizuri.

Fainali ya michuano hiyo ya Kombe la shirikisho inatarajiwa kufanyika wiki moja baada ya ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom kumalizika.

0 comments:

Post a Comment