Magoli mawili ya Mavugo 67' na Kichuya 81' yameiwezesha timu ya simba kuibuka na ushindi wa goli 2 - 1 dhidi ya watani wao wajadi simba.
Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata goli 5' ya mchezo kufuatia uzembe wa beki wa simba Lufunga kuzembea kuhamisha mpira na kuzidiwa ujanja Chirwa wakati chirwa anaenda kufunga lufunga alimkwatua na kusababisha pigo la penati na kuzawadiwa kadi ya njano.
Msuva alipiga penati kiufundi na kuiandikia yanga goli la kuongoza.
simba walionekana kupotea na kushindwa kabisa kufika langoni mwa Yanga na Yanga walifika zaidi langoni mwa Simba lakini kukosa umakini kwa Safu ya ushambuliaji ya yanga kuliwanyima uongozi wa goli nyingi.
mpaka mapumziko yanga 1 - 0 simba na umilikaji wa mchezo ukiwa 49 kwa simba 51 kwa yanga.
kipindi cha pili dakika ya 51 simba walifanya mabadiliko yaliyoshtua baada ya kumtoa beki wa kati Lufunga na kuingia mshambuliaji Shiza Kichuya.
55' chirwa alimzidi ujanja beki Bukungu na kumzidi mbio lakini beki huyo alikubali yaishe alimkwatua chirwa na kuzawadiwa kadi nyekundu.Yanga walipata faulo ambayo haikuzaa matunda.
mabadiliko ya kumtoa Ibram Mo na kuingia Mkude yaliwarudisha simba mchezoni na kusababisha kulimiliki vilivyo eneo la katikati na kuifanya yanga kupotea kabisa.
Mavugo alimalizia kazi nzuri toka wingi ya kulia iliyochongwa na shujaa wa mchezo wa leo Shiza Kichuya kwa kuunganisha kwa kichwa na kuifanya Simba kusawazisha goli hilo.
dakika ya 81 Shiza kichuya alishindilia msumari wa mwisho baada ya juhudi binafsi na kumchungulia kipa wa yanga Munish kisha kuupiga mpira upande wa kulia na kumshinda mlinda mlango huyo na kuipa simba ushindi huo mnono kwenye ligi ambao haijawi kuupata tangu 2015.
ikumbukwe 2016 simba ilikubali kupoteza michezo yote miwili na msimu huu mchezo wa kwanza waligawana pointi baada ya goli lililoleta utata la Amis Tambe na Kichuya kuiokoa simba dakika za lala salama.
Simba sasa imefikisha point 54 baada ya michezo 23 wakati Yanga wao wanapoint 49 baada ya mechi 22.
Yanga iliwakilishwa na:
1. Deogratius Munishi
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Vicent Andrew
5. Kelvin Yondani
6. Justine Zulu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Haruna Niyonzima
Akiba
- Ali Mustafa
- Hassani Kessy
- Nadir Haroub
- Geofrey Mwashuiya
- Deusi Kaseke
- Juma Mahadhi
Simba iliwakilishwa na:
1. Daniel Agyei
2. Besala Janvier Bkungu
3. Mohammed.Hussein
4. Novati Lufunga
5. Abdi Banda
6. James Kotei
7. Yassin Muzamiru
8. Mohammed Ibrahim
9. Ibrahim Ajib
10. Laudit Mavugo
11. Juma Liuzio
#Akiba
- Peter Manyika
- Hamad
- Saidi Ndemla
- Jonas Mkude
- Mwinyi Kazimoto
- Pastory Athanas
0 comments:
Post a Comment