Thursday, May 19, 2016

HABARI KUBWA ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO MEI 19

Arsenal Imetenga Euro Milioni 65 Kumnasa Morata
Klabu ya Arsenal imetenga kitita Cha Euro Milioni 65 kuhakikisha wanapata saini ya Morata anayetumikia klabu ya Juve kwa sasa.

Sessegnon & Anichebe Kuondoka West Brom
Kocha wa West Brom amewapongeza wachezaji wake kwa mchango wao katika timu huku akiwatakia kila la kheri katika maisha yao ya soka baada ya kuachwa na klabu hiyo Jana Jumatano.

Fabregas Ampogeza Terry
Nahodha wa Chelsea John Terry ameongeza mkataba na klabu yake na hatua hiyo imepongezwa na mchezaji mwenzie Fabregas.

Ben Arfa Anatakiwa Na Vilabu 18
Baada ya kuonyesha kiwango bora katika ligi kuu nchini Ufaransa msimu huu, vilabu vingi vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ikiwemo Barcelona.

Celtic Wanataka Kumsainisha Brendan Rodgers
Mabingwa wa Ligi kuu nchini Scotland, Celtic wapo katika hatua za kumsajili kocha mpya na Rodgers ameonekana kuwa ni chaguo sahihi kwa klabu hiyo.

Man UTD Washauriwa Kumsajili Staa Wa Leicester City
Drinkwater (26) ambaye alianza maisha yake ya soka katika kituo cha kukuzia soka kwa vijana cha Man United kabla hajaondoka mwaka 2012 amekuwa na mchango mkubwa sana katika ubingwa waliouchukua Leicester City msimu huu na Man Utd wameshauriwa kumchukua mchezaji huyo.

James Rodriguez Yupo Tayari Kujiunga Na Man Utd
Mchezaji wa kimataifa wa Colombia James amekuwa katika wakati  mgumu katika klabu ya Madrid kwa kuwekwa benchi na kocha wake, James amesema atakuwa na furaha zaidi endapo atajiunga na United.

Fenerbache Wanamtaka Mourinho
Kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kujiunga na United lakini Fenerbache wao wanaamini watamnasa kocha huyo kwa mshahara wa Euro milioni 15 kwa mwaka mshahara ambao Fenerbache wanaamini utamshawishi Mourinho kujiunga na klabu yao.

Yaya Toure Katika Mazungumzo Na Inter-Milan
Manchester City wako tayari kumwachia Midfied wao katika dirisha la usajili huku kukiwa na uwezekano wa kuungana na kocha  wake wa zamani Roberto Mancini katika dimba la San Siro.

Related Posts:

  • MAROUANE FELLAINI:"HIKI NDO ALICHONIAMBIA MOURINHO"Marouane Fallaini ameweka wazi kuwa Kocha Jose Mourinho alimtumia ujumbe alipowasili Man United. Kiungo huyo wa Ubelgiji amesema Mourinho alimtumia ujumbe akimkaribisha United huku pia akimtakia kila la kheri katika michua… Read More
  • TAARIFA YA MOURINHO YAWAGAWA MASHABIKI MAN UKlabu ya Manchester United ilitangaza majina ya wachezaji wake ambao wataendelea kuitumikia United huku pia wakithibitisha kuwa nyota wanne hawana nafasi tena klabuni hapo. Kiungo Nick Powell ni miongoni mwa wachezaji amba… Read More
  • USAJILI YANGA NI MWENDO MDUNDOKlabu ya Yanga imesema bado ina mipango ya kusajili wachezaji wa kimataifa kwa ajili ya kukisaidia kikosi chao kufanya vizuri katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC). Yanga imeshawanasa wachezaji wann… Read More
  • HUKU NDIKO SIMBA WANAKOSAKA NYOTA WAPYA Klabu ya Simba ipo katika pilikapilika za kuhakikisha wanaimarisha kikosi chao lengo likiwa ni kutwaa ubingwa wa ligi msimu ujao. Katika kuhakikisha wanafanya usajili wa uhakika Simba imeelekeza nguvu zake nchini Uganda,… Read More
  • KIFAA KIPYA CHAAHIDI MAKUBWA SIMBAKiungo mshambuliaji aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni Jamali Mnyate amesema kusaini kwake Simba mkataba wa miaka 2 ni kujiendeleza kimpira na kuisaidia Simba kupata mataji. Mnyate aliyejiunga na Simba akitokea Mwadui F… Read More

0 comments:

Post a Comment