Thursday, March 2, 2017

Liverpool Vs Arsenal, historia, uchambuzi na utabiri


MUDA: 20:30

UWANJA: ANFIELD,LIVERPOOL

Liverpool wanawaalika Arsenal katika dimba la Anfield wikiendi hii wakiwa na rekodi nzuri ya mechi mchezo wa kwanza uliofanyika Emirates ambapo walishinda 4 – 3 dhidi ya Arsenal kwa magoli ya Coutinho (45'+1, 56’), Lallana (49'), ManĂ© (63') wakati yale ya Arsenal yalifungwa na Walcott (31'), Oxlade-Chamberlain (64'), Chambers (75').



Liverpool pia wanaingia uwanjani jumamosi wakiwa na kazi moja tu ya kuhakikisha wanashinda Kutokana na shinikizo la Manchester United ambayo inaonekana kuimarika ikiwa nyuma kwa alama 1 tu.

Mchezo wa mwisho wa Liverpool ilikubali kipigo kikali toka kwa bingwa mtetezi wa ligi hiyo Leicester City cha goli 3 – 1.

Mchezo wa jumamosi unakuwa na hamasa ya aina yake kwani timu hizo mbili zinapishana pointi moja tu Liverpool wanapointi 49 baada ya michezo 26 katika nafasi ya 5 huku Arsenal wakiwa na pointi 50 katika michezo 25.

Liverpool na Arsenal tangu mwaka 2010 wamekutana mara 13, Arsenal wameshinda mara nyingi zaidi mara 4 wakati Liverpool wameshinda mara 3 na kutoka suluhu mara 6.

Jumla ya magoli 45 yamefungwa katika michezo hiyo na vipigo vikubwa ni 08 Feb 2014 Liverpool 5 Arsenal 1 katika dimba la Anfield.

04 Apr 2015 Arsenal 4 Liverpool 1katika dimba la Emirates.

Zifuatazo ni rekodi za Liverpool na Arsenal katika ligi kuu tangu 2010

15 Aug 2010   Liverpool v Arsenal    1-1       Premier League 2010/2011
17 Apr 2011    Arsenal v Liverpool    1-1       Premier League
20 Aug 2011   Arsenal v Liverpool    0-2       Premier League 2011/2012
03 Mar 2012    Liverpool v Arsenal    1-2       Premier League
02 Sep 2012    Liverpool v Arsenal    0-2       Premier League 2012/2013
30 Jan 2013     Arsenal v Liverpool    2-2       Premier League
02 Nov 2013   Arsenal v Liverpool    2-0       Premier League 2013/2014
08 Feb 2014    Liverpool v Arsenal    5-1       Premier League
21 Dec 2014    Liverpool v Arsenal    2-2       Premier League 2014/2015
04 Apr 2015    Arsenal v Liverpool    4-1       Premier League
24 Aug 2015   Arsenal v Liverpool    0-0       Premier League 2015/2016
13 Jan 2016     Liverpool v Arsenal    3-3       Premier League
14 Aug 2016   Arsenal v Liverpool    3-4       Premier League   2016/2017

4 March 2017  Liverpool vs Arsenal      ?       Premier League   

0 comments:

Post a Comment