Messi alitolewa katika dakika ya 63 ya mchezo baada ya kuumia wakati akiitumikia timu yake ya Taifa ya Argentina.
Nahodha huyo wa Argentina alipewa matibabu kwa muda wa dakika tatu kabla kocha Gerardo "Tata" Martino hajaamua kumtoa nje kabisa.
Ripoti ya Madaktari wa timu hiyo imesema Messi alipata maumivu ya mbavu lakini majeraha hayo sio makubwa ya kumfanya Messi ashindwe kushiriki mashindano ya Copa America yanayotarajiwa kutimua vumbi siku chache zijazo.
Katika mchezo huo Argentina iliibuka na ushindi wa goli 1 - 0 dhidi ya Honduras goli lililofungwa na Gonzalo Higuan.
0 comments:
Post a Comment