Klabu ya Simba imetekeleza agizo la FIFA la kumlipa pesa zake zote Donald Mosoti na kuepukana na adhabu ya kushushwa daraja ambayo FIFA walitishia kuitoa.
Uongozi wa Simba umekamilisha malipo ya fedha taslimu kiasi cha Sh. za Kitanzania milioni 62.4 kwa aliyekuwa mchezaji wao Donald Mosoti.
Awali FIFA ilitoa agizo kwa klabu ya Simba kumlipa mchezaji huyo ndani ya siku 30 vinginevyo wangeshushwa daraja. Barua ya FIFA kwa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF iliwapiga faini klabu ya Simba kwa kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo kutokana na sakata hilo la Mosoti.
Mosoti amekiri kupokea fedha zake zote kutoka kwa Simba na kusema anashukuru na sasa hakuna anayemdai mwenzie.
"Nashukuru Simba imenilipa changu, siwadai, hawanidai" alisema Donald Mosoti.
Simba ilipewa siku 30 tu kuhakikisha wanamlipa Mosoti Stahiki zake zote kuanzia tarehe ambayo walipokea barua kutoka kwa FIFA ambayo ilikuwa ni Mei 3 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment