Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania limeitupilia
mbali rufaa ya timu ya polisi Dar es salaam waliokata kutaka wapewe ushindi
katika mchezo wao wa raundi ya tano ambao simba ilishinda kwa 2 -0,
Mchezaji Novalty Lufunga aliekatiwa rufaa alipata kadi nyekundu
katika mchezo wa mwisho kwa simba wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016 ambapo
simba ililala katika mchezo huo wa 11april 2016 kuondoshwa mashindanoni.
Kanuni za Azam Sports
Federation Cup zinaweka wazi kuwa kadi ya njano au nyekundu inaisha pale tu
mashindano husika yanapoisha labda itokee kadi hiyo imeongezewa na adhabu nyingine,
kama itakuwa imeongezewa adhabu basi klabu na mchezaji watataarifiwa kwa maandishi.
Hivyo basi kwa kanuni hiyo ya mashindano polisi Dar itakuwa
imetupwa nje rasmi katika mashindano hao ya Azam Sports Federation Cup
0 comments:
Post a Comment