Friday, July 15, 2016

PAUL POGBA AWAAGA MARAFIKI ZAKE JUVENTUS

Licha ya kiwango kidogo alichoonyesha katika michuano ya Euro 2016 katika ardhi ya nyumbani, Paul Pogba anabaki akihusishwa sana na kujiunga na klabu ya Manchester United chini ya kocha Mourinho.

Manchester United wanaonekana kupania kuinasa saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ameng'aa tangu ajiunge na mabingwa wa Seria A klabu ya Juventus akitokea Manchester United alikokatolewa kama mchezaji huru.

Kumsajili Pogba sio tu kutaongeza uwezekano wa United kunyakua ubingwa wa ligi kuu msimu ujao na kurudi kwenye ushiriki wa klabu bingwa Ulaya, bali pia kutaiongezea United mapato.

Ripoti zinaonyesha kwamba makubaliano ya mkataba wa miaka mitano yamefikiwa kati ya Mashetani Wekundu na Paul Pogba. Kiungo huyo kinda anaripotiwa kukusanya jumla ya pauni milioni 13 kwa mwaka na pauni milioni 65 kwa kipindi chote cha mkataba wake na United kama ilivyoripotiwa na Marca.

Pogba amecheza mechi 49 akiwa na klabu ya Juventus msimu uliopita huku akichangia upatikanaji wa magoli yasiyopungua 26, magoli 10 akifunga mwenyewe na kutoa pasi zilizozaa magoli (assist) 16.
Kwa ujumla Pogba amecheza mechi 178 akiwa na wababe hao wa Turin na kuisaidia timu hiyo kubeba mataji nane (8) makubwa.

Marca imeripoti siku chache zilizopita kuwa Manchester United ipo mbioni kumsajili tena mchezaji huyo raia wa Ufaransa kwa thamani ya Euro milioni 120 na kwamba kiungo huyo amewajulisha marafiki zake wa karibu kuwa anataka kujiunga na Manchester United.

Sasa hivi inaonekana kuwa lilikuwa ni kosa kwa United kumwachia mchezaji huyo kama mchezaji huru wakati huo anaondoka United na kwenda kujiunga na Juventus, lakini kufanya kosa ni jambo moja na kukubali kosa na kulisahihisha ni jambo jingine.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment