Friday, July 15, 2016

KAULI ZA WACHEZAJI YANGA KUELEKEA MECHI DHIDI YA MEDEAMA

Mabingwa wa Ligi kuu Vodacom na Wawakilishi pekee Afrika Mashariki katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika klabu ya Yanga inatarajiwa kushuka dimbani kesho kumenyana na Medeama SC kutoka nchini Ghana mchezo wa tatu hatua ya makundi kombe la shirikisho Barani Afrika ( CAF CC)

Yanga imeshacheza michezo miwili katika michuano hiyo na kushuhudia ikiruhusu vichapo katika mechi zote mbili kitu kinachowafanya washike mkia katika kundi lao linaloongozwa na TP Mazembe aliyejikusanyia alama zote sita katika michezo yote miwili waliyocheza.

Hali ya kupoteza mechi zote mbili imepokelewa vibaya si tu kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo bali pia hata wachezaji nao wanaonyesha kuumizwa matokeo hayo.



Akizungumzia mchezo wa kesho mshambuliaji wa Yanga raia wa Zimbabwe Donald Ngoma amesema, kitendo cha kupoteza michezo yote miwili si jambo jema kwao na kwamba wanahitaji kupata ushindi katika mechi ya kesho ili kufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatau inayofuata.

"“Hatujafunga na hatuna pointi yoyote jambo ambalo siyo zuri kwetu, nafikiri tukifanya vizuri katika mechi ya kesho itatufanya tufufue matumaini. Tutapambana kwa muda wote,” alisema Ngoma.

Aidha kwa upande wake Nahodha  wa klabu hiyo Nadir Haroub Cannavaro, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo huku akiwaomba kutokukata tamaa kwani wao wamejiandaa kupambana kadri wawezavyo kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo.

"Tunamshukuru mungu tumemaliza mazoezi salama ila tu nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutushangilia kesho . Tunaomba wasife moyo tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho tutapambana ila tu watuombee dua tuweze kufanya vizuri "

Ili kuleta matuamaini ya kusonga mbele hatua ijayo Yanga inatakiwa kushinda katika mchezo huo vinginevyo mambo yatakuwa sio mazuri endapo watakubali kufungwa au hata kutoa sare katika mchezo huo, kwani hadi hivi sasa imekwishacheza michezo miwili na kufungwa yote, Baada ya mechi ya kesho Yanga itabakisha michezo mitatu ambayo itakuwa ni ya marudio kwa timu zote tatu, yani, MO Bejaia, TP Mazembe na Medeama SC.

KILA LA KHERI YANGA
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment