Timu ya Ndanda Fc imewaongezea mkataba wa mwaka mmoja wachezaji tisa kwa ajili ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho msimu ujao wa Ligi Kuu Vodacom 2016/17.
Msemaji wa Ndanda Fc, Idrisa Bandali aliwataja wachezaji walioongezewa mkataba kuwa ni golikipa Jackson Chove, Jeremia Kisubi, na Paul Ngalema.
Wengine ni Hemed Khoja, Kigi Makasi, Omary Mponda aliyepewa miaka miwili, Salum Minelly, Riphati Hamis na Ben Sylvesta. Bandali alisema timu hiyo yenye makazi yake Mtwara imewaacha Omega Seme, Masoud Ally na Asili Mnkondya baada ya kumaliza mikataba yao.
“Huo ni usajili wa mwanzo bado tunaendelea na harakati za kuangalia wachezaji kwa mujibu wa ripoti ya Kocha, tunategemea tutasajili wengine ambao watasaidia timu kufanya vizuri,” alisema. Msemaji huyo alisema kikosi hicho kinatarajia kuanza mazoezi wiki ijayo.
Katika kuimarisha kikosi hicho, timu hiyo imesajili mchezaji mmoja Ibrahim Isihaka kutoka Geita Gold Mine.

0 comments:
Post a Comment