Thursday, July 14, 2016

HATIMAYE TFF YAMKALISHA JERRY MURO

Hatimaye Ofisa Habari wa Yanga Jerry Muro, amekubali kutumikia adhabu iliyotolewa na TFF.

Awali Muro alipinga adhabu hiyo kwa kutoa kauli nyingi zikionyesha kuwa TFF walikiuka taratibu za kutoa adhabu hiyo. Licha ya kauli zote kuwa yeye si mwajiriwa wa TFF na kwamba TFF haina mamlaka ya kumfungia, Muro amekubali yaishe na kuitumikia adhabu aliyopewa.

Habari zaidi zinadai kuwa uongozi wa Yanga ni kama haukumtuma Muro kutoa lugha za kashfa kuhusu TFF kwenye vyombo vya habari.

Ofisa habari huyo jana alipost kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa “Nikifikiria figisu za soka la bongo, aisee nachoka kabisa, acha nijiweke pembeni kwa muda, nitawamiss mashabiki wangu wa kimataifa, acha nikae mbali kwa mbali”.

Kwa upande mwingine Katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdetit amesema "Barua ya Jerry kashaipata, uongozi wa Yanga kupitia kwa mwenyekiti wetu umemwambia atulie, akae pembeni kidogo, mwenyekiti kwa sasa yupo nje ya nchi".

TFF ilimfungia Jerry Muro kujihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja na kutoa faini ya Sh. milioni 3.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment