Wednesday, July 13, 2016

AZAM MEDIA YAZIMWAGIA VILABU VYA VPL MAMILION

Kampuni ya Azam Media imeongeza mkataba wa kurusha mechi za ligi kuu Vodacom msimu ujao 2016/17.

Mkataba huo umesainiwa jana kati ya TFF na klabu ya bodi ya Ligi na Uongozi wa Azam, huku mkataba huo ukiwa umeboreshwa kidogo kwa klabu kupata kiasi cha Sh. Milioni 126 kwa mwaka.

Awali kila klabu ilikuwa inapata sh. milioni 100. Hata hivyo klabu ya Yanga imezisusia klabu hizo kwa kile wanachodai kuwa hawawezi kupata sawa na klabu nyingine kutokana na ukubwa wa klabu yao na kwamba wana uwezo wa kuingiza zaidi ya fedha hizo kwenye mchezo wao mmoja dhidi ya Simba.

Katika mkataba huo kila klabu itapata sh. milioni 42 kwa awamu tatu ambapo jumla yake inakuwa milioni 126, Lakini awamu ya tatu ambayo ndio ya mwisho itatolewa kwa mfumo tofauti ambao utakuwa timu inayoshika nafasi ya juu katika msimamo wa ligi itafaidika kwa kupata zaidi na itakuwa hivyo hadi kwa klabu inayoshika nafasi ya chini.

Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tan zania (TFF), Selestine Mwesigwa alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kunakuwa na ushindani katika ligi.

“Kila timu inatakiwa kujiandaa vya kutosha na kuleta ushindani, kuona umuhimu wa kukaa kileleni, kila timu iwe na hamu ya kushinda mechi zake ili mwisho wa siku ifaidike,” alisema.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa Azam Tiddo Muhando alisema kampuni yake imeamua kuongeza zawadi na kubadilisha mfumo wa utoaji ili kuongeza ushindi na kampuni yake itaonesha ligi hiyo kwa kiwango cha juu tofauti na msimu uliopita.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment