Tuesday, January 31, 2017

Kocha Mwadui Aitabiria Ubingwa Yanga

Kocha wa klabu ya Mwadui FC, Ali Bushiri ameitabiria ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara (VPL 2016/17) klabu ya Yanga kufuatia kandanda safi liliopigwa na vijana hao wa Jangawani wakati timu yake ya Mwadui FC ilipolala kwa jumla ya mabao 2-0 katika uwanja wa taifa jijini Daresalaam.

Kocha huyo alisema kikosi chake kilizidiwa katika sehemu kubwa na mabingwa hao watetezi kitu kilichowalazimu kucheza kwa kujilinda zaidi kwa kuhofia kufungwa mabao mengi.

“Ukweli tuliingia kwenye mchezo huu tukihitaji angalau sare, lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda wenzetu walizidi kuja kutushambulia hatimaye wakapata walichokuwa wanakitaka,” amesema Bushiri ambaye ameichukua timu hiyo kwenye mzunguko wa pili akiziba nafasi ya Jamhuri Kihwelo.

Aidha kocha huyo alieleza kuwa, katika mchezo huo, timu yake ilizidiwa kimbinu na kibaya zaidi asilimia kubwa ya wachezaji wake hawana uzoefu mkubwa ukilinganisha na wale wa kikosi cha Yanga.

0 comments:

Post a Comment