Tuesday, January 31, 2017

Hivi Ndivyo Nusu Fainali AFCON Itakavyotimua Vumbi

Michuano ya Mataifa ya Afrika inayoendelea huko nchini Gabon imefikia hatua ya nusu fainali, hatua ambayo mechi zake zitachezwa katika siku za Jumatano na Alhamisi wiki hii.

Mitanange ya hatua hiyo ya nusu fainali itazikutanisha timu za Burkina Faso watakaokipiga na Misri kesho Jumatano huku Ghana wakimenyana na Cameroon siku ya Alhamisi.

Burkinafaso iliwaondosha Tunisia hatua ya robo fainali, Misri wao wakiifungisha virago Morocco wakati, Ghana iliwarudisha nyumbani Wakongo na Cameroon ilifuta ndoto za kutwaa ubingwa za timu ya taifa ya Senegal ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa huo wa AFCON mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment