Saturday, May 28, 2016

ROBERT LEWANDOWSKI KUTUA REAL MADRID

Wakala wa Robert Lewandowski, Cezary Kucharski amethibitisha kuwa Real Madrid walimfuata kuhusu uwezekano wa Lewandowski kutua Bernabeu.




Lewandowski aliye katika kiwango cha hali ya juu kwa hivi sasa anamaliza mkataba na klabu yake ya Bayern mwaka 2019, lakini licha ya yeye mwenyewe kusema anafuraha katika klabu hiyo ya Mabavaria, hajakanusha kutaka kuondoka klabuni hapo na kwenda kutafuta changamoto nyingine katika klabu zingine.

"Real Madrid walizungumza na sisi wiki chache zilizopita" alisema Cezary.

"Tuliwasikiliza na tulipeleka ripoti kwa uongozi wa Bayern kuhusiana na tulichokakijadili na Madrid" aliongeza Kucharski alipohojiwa na gazeti la habari la Ujerumani Der Spiegel.

Kwa mujibu wa ripoti ya Gazeti hilo, uhamisho wa Lewandowski kwenda Madrid utamfanya Straika huyo raia wa Poland kujikusanyia kiasi cha Euro milioni 25 kwa mwaka, kiwango kikubwa zaidi ukilinganisha na anachokipata kwa sasa akiwa Bayern.

Tangu awasili katika ligi ya nchini Ujerumani Budesliga mwaka 2010, Lewandowski amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 121 akiwa na klabu za Borussia Dortmund na Bayern.

0 comments:

Post a Comment