Saturday, June 18, 2016

HUYU NDO ANAYETARAJIWA KUWA KOCHA MPYA SIMBA

Baada ya kumkosa Kalisto Pasuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zimbabwe Simba walielekeza macho yao kwa kocha raia wa Ghana Sellas Tetteh Teivi

Simba wanakaribia kumpata kocha huyo baada ya mazungumzo kwenda vizuri, Sellas ni kocha maarufu sana Afrika na kutua kwake Msimbazi kunaweza kukaleta matumaini mapya katika klabu hiyo.

Zacharia Hans Poppe amesema wameshafanya mazungumzo ya awali na kwamba muelekeo ni mzuri na kama mambo yataendelea kwenda hivyo basi taratibu za kumsainisha kocha huyo anayeifundisha timu ya Taifa ya Sierra Leone kwa sasa zitakamilika.

"Tumefanya naye mazungumzo kwa wiki moja na mambo yanaelekea kuwa sawa pengine tukamtangaza kabla ya kumaliza zoezi la usajili na yeye akatusaidia kufanya usajili wa kikosi chetu cha msimu ujao." alisema Hans Poppe.

Sellas amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Ghana na alifanikiwa kuingoza timu ya vijana ya Ghana chini ya umri wa miaka 23 kucheza kombe la Dunia mwaka 2013.

Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

Related Posts:

  • Asante Kwasi Kujiunga Na Yanga SC Beki wa timu ya Mbao FC, Asante Kwasi amesema angetamani kuichezea Yanga katika msimu ujao wa ligi. Beki huyo wa kati wa Mbao ameyasema hayo kutokana na kuvutiwa na kiwango na mafanikio ya klabu ya Yanga mabingwa mara ta… Read More
  • TAARIFA ZA USAJILI: Barani Ulaya Mancini Atua Zenit Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amekabidhiwa rasmi mikoba ya kuinoa klabu ya Zenit ya nchini Urusi. Mancini anachukua nafasi ya Mircea Lucescu. Rasmi: Huntelaar arudi Ajax … Read More
  • Rasmi:Samir Nasri Atua Sevilla Manchester City imetangaza kuwa Samir Nasri amejiunga na klabu ya Sevilla kwa Mkopo. Endelea Kuungana Na Soka24 kwa habari za papo kwa papo za Soka kote Ulimwenguni............. ================== Stori Kubwa Zinazotikisa… Read More
  • Man City Yaweka Rekodi Ya Dunia Kwa Usajili Huu Klabu ya Manchester City imefikia makubaliano ya kumsajili mlinda mlango Ederson Moraes kutoka katika klabu ya Benfica ya nchini Ureno kwa kitita cha paundi milioni 35.  Uhamisho wa kipa huyo mwenye umri wa miaka 23… Read More
  • VIKOSI SIMBA, YANGA BAADA YA USAJILI DIRISHA DOGO Dirisha Dogo la Usajili limefungwa rasmi jana Alhamisi Disemba 15 majira ya Saa 6:00 usiku. Soka24 imefanikiwa kuvinasa vikosi vya miamba ya soka Tanzania Bara, Yanga na Simba baada ya kufungwa kwa dirisha hilo la usajili h… Read More

0 comments:

Post a Comment