Thursday, May 26, 2016

HAWA NDO WACHEZAJI 3 ANAOWAKUBALI ZLATAN IBRAHIMOVIC DUNIANI

Mshambuliaji anayeihama PSG Zlatan Ibrahimovic amesema kwa sasa ni wachezaji 3 tu duniani ndo wakali.


Zlatan ambaye ameweka wazi kuwa anaondoka PSG huku pia tetesi zikimhusisha na kujiunga na United amejipa kick kwa kusema katika ulimwengu wa soka kwa sasa duniani ni wachezaji watatu tu ndo wenye uwezo mkubwa, katika orodha yake kawataja Christiano Ronaldo wa Real Madrid, Lionel Messi anayecheza Barcelona na yeye mwenyewe Zlatan Ibrahimovic.


Iliwahi kuripotiwa kuwa Mke wa Zlatan hapendi mumewe ajiunge na mashetani wekundu na badala yake anataka ahamie katika ligi kuu ya Nchini Marekani, na mpaka hivi sasa bado haijajulikana kama atajiunga na United au ataafikiana na maamuzi ya Mkewe.


0 comments:

Post a Comment