Baada ya uvumi mwingi kuwa Christiano Ronaldo anataka kuondoka Real Madrid, wengine wakimuhisha kujiunga na PSG na wengine Man United, Ronaldo ameamua kufunguka na kuweka wazi timu atakayomalizia soka lake.
Christiano Ronaldo amesema atamalizia soka lake Real Madrid, Ronaldo ameyasema hayo zikiwa zimebaki saa chache tu Madrid kucheza na Atletico katika fainali ya Champions League kesho Jumamosi itakayochezwa Stadio Giuseppe Meazza huko Milan.
Kulikuwa na hofu miongoni mwa mashabiki wa Real Madrid kuhusu uimara wa Ronaldo katika kuikabili fainali hiyo lakini taarifa za hivi punde zinasema kwamba Supastaa huyo raia wa Ureno ataanza katika mchezo huo, huku Ronaldo mwenyewe akisisitiza kuwa mchezo huo hautakuwa wa mwisho kwake klabuni hapo.
"Paris Saint-Germain na Manchester City wasahau kuhusu mimi, nastaafu mpira Real Madrid" alisema Christiano Ronaldo.
"Nimekuwa na wakati mzuri na mbaya katika maisha yangu ya soka, kwa miaka 4 nyuma sikuwa na furaha lakini hakuna sehemu bora zaidi ya hapa Madrid" aliongeza Ronaldo.
Akizungumzia uwepo wa kocha zidane kikosini hapo Ronaldo amesema, Zidane ndio sababu ya yeye kutaka kuendelea kubaki hapo na kufanya kila awezacho kwa ajili yake.
"Hana uzoefu mkubwa lakini ameshafanya mambo makubwa hadi sasa"
Presha kubwa sasa imebaki kwa Real Madrid ambayo haijashinda taji lolote msimu huu, hawajachukua La Liga wala Copa Del Rey, hivyo UEFA ndo inabaki kuwa taji lao pekee wanalolipigania.
0 comments:
Post a Comment