Home »
Kimataifa
,
Usajili
» DANI ALVES AMECHEZA MECHI YAKE YA MWISHO BARCELONA...HII NDO KLABU ANAYOKWENDA
Imeripotiwa kuwa Superstaa wa Barcelona Dani Alves yupo mbioni kujiunga na Miamba ya soka nchini Italia.
Taarifa zinasema kuwa Alves Tayari ameshakubali mkataba wa miaka mitatu kuitumika Juventus, Alves amekosa muda mwingi wa kucheza msimu huu na inaonekana wazi kuwa anahitaji sehemu ambayo atapata changamoto mpya, sehemu hiyo ikitajwa kuwa Turin, akiwa anaondoka Barcelona kama mchezaji huru.
Ingawa Barcelona hawatapata pesa yoyote kuondoka kwa Alves klabuni hapo, lakini wataokoa zaidi ya Euro milioni 8 kutoka katika mkataba wa Alves, kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa radio wa Caden Ser ni kwamba dili hilo litakamilika siku chache zijazo.
0 comments:
Post a Comment