Home »
Fa
,
Kitaifa
» KILIO CHA DENIS KITAMBI BAADA YA KIPIGO CHA MAGOLI 3 - 1 KUTOKA KWA YANGA
Kocha Mkuu wa Muda wa Azam Fc Denis Kitambi amesema kilichowaponza jana hadi kukubali kipigo cha magoli 3 - 1 kutoka kwa Yanga ni kushindwa kuyazuia mashambulizi ya Yanga yakiyopitia pembeni.
Azam ilipoteza mchezo wa fainali kombe la shirikisho jana dhidi ya Yanga kwa kukubali kipigo cha goli 3 - 1,Magoli ya Yanga yakifungwa na Amissi Tambwe aliyefunga mawili kwa upande wa Yanga na Deus Kaseka akitupia la tatu huku lile la Azam Fc likifungwa na Didier Kavumbagu.
Akizungumza baada ya mchezo huo kocha Kitambi amesema Yanga walifanikiwa kutumia eneo la pembeni kupitishia mashambulizi yao kitu kilichowasaidia kupata magoli 2 kupitia eneo hilo.
“Kwa hiyo kutokuwa makini kuzuia mashambulizi yao pembeni ya uwanja hiyo ndio ilikuwa udhaifu, wakati wa mapumziko tulijitahidi kusema lazima tutumie njia yoyote ile ya wao kutushambulia kupitia pembeni ya uwanja, hasa hasa krosi ambazo kipindi cha kwanza zilikuwa zikitupa matatizo.
“Lakini napenda kuwapongeza wachezaji wangu walifanikiwa kupambana vizuri hata Yanga walipotangulia kutufunga bao la kwanza dakika ya tisa hata kipindi cha pili tulipofungwa bao la pili bado waliweza kujibu mashambulizi, lakini hatukuweza kutengeneza nafasi nyingi za kutosha za kuweza kushinda mchezo,” alisema.
Uongozi wa Azam FC umeshaingia mkataba Makocha kutoka nchini Hispania, Zeben Hernandez (Kocha Mkuu), Jonas Garcia (Kocha wa Viungo), huku wengine wakitarajia kuongezeka Julai mwaka huu katika eneo la Kocha wa Makipa, Kocha Msaidizi atakayesaidiana na Kitambi pamoja Daktari wa timu.
0 comments:
Post a Comment