Monday, August 29, 2016

WEST BROM YAVUNJA REKODI YA KLABU USAJILI WA CHADLI

Klabu ya West Bromwich Albion imevunja rekodi ya klabu hiyo kwa kumsajili Winga wa Tottenham Spurs kwa kitita cha Pauni milioni 13.

Chadli alijiunga na Spurs akitokea FC Twente kwa uhamisho wa pauni milioni 7 Julai 2013 na amefanikiwa kufunga magoli 15 katika michezo 88 ya ligi kuu Uingereza aliyowahi kucheza.
Hata hivyo Winga huyo alicheza michezo 10 tu msimu uliopita chini ya kocha Mauricio Pochettino huku Tottenham ikionekana kuvutiwa na Winga wa Crystal Palace Wilfred Zaha.

Rekodi kubwa ya usajili katika klabu ya Albion ni ile ya usajili wa Pauni milioni 12 walioufanya kwa mchezaji wa Zenit St Petersburg, Salomon Rondon.

West Brom inakuwa klabu ya 11 kuvunja rekodi ya usajili wake yenyewe huku klabu zingine zikiwa ni Southampton waliotangaza kumnasa Sofiane Boufa kutoka Lile kwa kitita cha pauni milioni 16.
 Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

 

Related Posts:

  • MBUYU TWITE NDANI ISSOUFOU BOUBACAR NJE YANGA Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba Kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda Mbuyu Twite ameongeza mkataba katika klabu hiyo. Ikiwa tayari Yanga imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili golikipa Beno Kakolanya kutoka Ta… Read More
  • HUYU MWINGINE ALIYENASWA NA WEKUNDU WA MSIMBAZI Simba imemsainisha beki wa Mwadui Emmanuel Semwanza. Semwanza ameichezea Mwadui kwenye mzunguko wa pili baada ya kununuliwa kwenye kipindi cha usajili wa dirisha dogo akitokea African Lyon, tayari Beki huyo amesaini mkata… Read More
  • MAROUANE FELLAINI:"HIKI NDO ALICHONIAMBIA MOURINHO"Marouane Fallaini ameweka wazi kuwa Kocha Jose Mourinho alimtumia ujumbe alipowasili Man United. Kiungo huyo wa Ubelgiji amesema Mourinho alimtumia ujumbe akimkaribisha United huku pia akimtakia kila la kheri katika michua… Read More
  • KIPA YANGA ASAKA KLABU YA KUHAMIABaada ya Yanga kufanikiwa kumsajili mlinda mlango kutoka timu ya Tanzania Prisons, Ben Kakolanya, Mlinda mlango wa siku nyingi wa klabu hiyo, Benedictor Tinoco amesema ni wakati wake kuangalia sehemu gani atacheza msimu ujao.… Read More
  • USAJILI SIMBA NI TISHIOMwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope ametamba kuwa wamejipanga kufanya usajili wa kisayansi zaidi lengo likiwa ni kupata kikosi imara kitakachowapa ubingwa msimu ujao. Kwa miaka mitatu mful… Read More

0 comments:

Post a Comment