Tuesday, August 30, 2016

SIMBA YABADILI GIA ANGANI

Sare ya bila kufunguna waliyoipata Simba dhidi ya JKT Ruvu imemfanya kocha wa klabu hiyo, Joseph Omog kubadili mfumo wa uchezaji na kusisitiza umakini kwa wachezaji katika mechi zijazo.

Katika mchezo huo dhidi ya JKT Ruvu Simba ilionyesha kandanda safi sana licha ya kutofanikiwa kupata goli. Kufuatia matokeo hayo Mcameroon huyo amesema analazimika kubadili aina ya uchezaji (Mfumo) kwa kucheza kwa malengo huku wakitafuta njia za kufunga mabao pale wanapokuwa na mchezo mgumu kama ambavyo ilikuwa kwa JKT Ruvu.

“Tulicheza vizuri lakini hatukupata ushindi siyo matokeo mabaya, lakini pia siyo mazuri kwa sababu ligi ina ushindani unapopata matokeo tofauti na ushindi inakuwa mbaya na sasa nimeona tubadili mfumo wa uchezaji wetu tuache kupiga pasi nyingi na sasa tunatakiwa kwenda mbele kutafuta ushindi na kila mchezaji wangu nataka aongeze umakini awapo uwanjani,” alisema Omog.

Aidha Omog aliongeza kuwa, pamoja na kwamba matokeo hayo ya sare siyo mabaya lakini yeye kama kocha hayajamfurahisha na ndio sababu ya kupanga kubadilisha mfumo katika kikosi chake.
Kocha huyo pia amewataka mashabiki wa Simba watulie na kuondoka shaka kwa matokeo hayo ya sare kwani ligi ndo inaanza huku akisisitiza kwamba kuna safari ndefu hadi kufikia mwisho wa kumpata bingwa.

=============
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;
Aubameyang Aitamani Real Madrid

Nyota Wa Zamani Wa Man U Aitabiria Ubingwa Chelsea


Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi


"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm

Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA


0 comments:

Post a Comment