Mkataba wa Miraji na Simba unaelekea kumalizika na ameamua kuzungumza hayo baada ya kuona viongozi wa klabu hiyo wapo kimya kuhusu hatima yake wakati huu ambapo dirisha la usajili tayari limeshafunguliwa.
"sijajua kama nitarejea Simba, maana viongozi hawaeleweki na mkataba wangu unaelekea ukingoni, hivyo nipo tayari kuchezea timu yoyote isipokuwa ya ligi Daraja la kwanza" alisema Miraji.
Aidha beki huyo alisema kuandamwa andamwana na majeraha kulimuathiri na kushindwa kucheza vizuri kutokanan na uoga wa kuumia tena.
Miraji ameongeza kuwa endapo viongozi wa Simba watakuwa tayari kufanya nae mazungumzo yeye yupo tayari kuichezea klabu hiyo akitoa sababu kuwa mpira ni kazi yake na malengo yake ni kucheza mpira wa kulipwa.
0 comments:
Post a Comment